Kuna kiwanda cha kutengeneza Chupa kinaitwa Kioo Limited, Kipo jijini Dar es Salaam, hiki ni kiwanda kikubwa tu hapa nchini, kinatengeneza chupa, na kinauza ndani ya nchi na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla, kiwanda hiki kinamilikiwa na wahindi, kama ilivyo desturi ya viwanda vyingi nchini mwetu.
Hali katika kiwanda hiki inasikitisha, kama si kukatisha tamaa kabisa.
Nilipewa habari kuhusu mwenendo wa kiwanda hiki na mmoja wa wafanyakazi, ambaye alinieleza kwa masikitiko makubwa kuhusu yanayotokea ndani ya kiwanda hiki, manyanyaso na unyonyaji, nikajitwika jukumu la kuwa kibarua kwa siku kadhaa nijionee yaliyomo usiulize mshahara wangu maana ulikuwa shilingi 3,600/=tshs za kitanzania kwa siku, nikaingia mzigoni kwa takribani mwezi mmoja hivi, niliona mengi, lakini hili kuu ndilo limenifanya niandike na kulifikisha kwenu wanajamvi, awezaye alifikishe kwa wahusika.
Jamani hawa wamiliki wa Kioo wameamua kujenga Plant Mpya ili kupanua kiwanda chao amabalo ni jambo la heri lakini kwao tu si kwetu kwa jinsi system ilivyo hapo kiwandani! Naamini mpaka sasa bado ujenzi unaendelea, kilichonisikitisha ni kuletwa vibarua kama 50 au chini ya idadi hiyo kutoka India, hawa jamaa, wanafanya kazi zile ambazo watanzania wanazifanya kila leo nchini humu, wahindi hawa ni wengi na sijui walipewaje viza, walipewa kama kina nani? Mamlaka zetu katika uhamiaji zinafanya kazi gani, wizara ya viwanda na biashara, wizara ya kazi, wizara ya mambo ya ndani inafanya nini? Je wakaguzi wa wizara husika hawalijui kweli hili?
Waziri Mkuu Pinada alisema wakati akifungua Mkutano wa watafiti, alisema kuwa hajui kwa nini umasikini unazidi kukithiri japokuwa kuna tafiti kibao.
Ukifika Kioo, utaona jinsi watanzania wanavyonyimwa fursa kwa maana kila kitu kipo kwa wageni, menegiment yote ni ya kwao, Hivi kweli tanzania ya leo, unaajiri Marketing Meneja Kutoka Ulaya eti kwa kisingizio kuwa watanzania ni wazembe!
Watu wetu wanaosomeshwa kwa kodi zetu wanakuwa underultilize, Engineer anawekwa kuwa Supervisor, wakati technician anaeletwa kutoka India anapewa cheo cha Engineer, inasikitisha.
Kwa mtindo huu maandamano na migomo haitaisha nchini, na serekali kwa kuzembea huku isilaumu watu kwa utovu wa nidhamu, uchochezi na sababu zingine.
Uwekezaji ni lazima ulete tija kwetu sote na si kwa wageni tu.
Wanasiasa nao wasijiegemeze tu kwenye migodi, na chaguzi, tembeleeni watu viwandani muone wanavyoumia.Ukifika kioo huna haja ya kuuliza sana kwani mambo yanazungumza yenyewe "RES IPSA LOQUITUR"