Deva
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 1,237
- 1,819
- Thread starter
- #61
Wewe ulikuwa unafanya kazi gani mkuuKInachokupa shida sio kuoa, ni kupenda ... ona ilivyokuwa kwangu ...
Nilipomaliza masomo (nikiwa na miaka 22) tayari nilikuwa na mchumba ambaye naamini tulikuwa tunapendana sana. Alipenda kunitembelea nyumbani jambo nililoliona kama ni kero; hivyo niliamua kupanga chumba. Ili mambo yaende sawa ilibidi nimfanyie mpango wa kazi ili aweze kutoka nyumbani kwao moja kwa moja. Na hiyo ndo ilikuwa staili yangu ya kuoa. Mambo mengine niliyarekebisha wakati tunaendelea kuishi.
Kwa sasa nafurahia kuwa na watoto wakubwa ambao tunasaidiana kwa mambo mbalimbali.
Kuoa mapema kuna raha yake.