Jinsi suala la kuoa linavyonipa shida

Jinsi suala la kuoa linavyonipa shida

Deva

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
1,237
Reaction score
1,819
Habari zenu wakuu.

Niende kwenye mada moja kwa moja, mimi ni kijana Miaka 24, ambaye ni mtoto wa kwanza wa kiume kwenye familia yenye watoto wanne, wa kiume nikiwa mimi peke yangu baada ya kufariki mdogo wangu wa kiume mwaka 2017, wazazi wangu ni watu waliokaribia uzeeni miaka 50 wamefikisha, Baba ndio anajishughulisha, mama ni wa nyumbani

Mwaka huu 2018 pia imetokea mtoto wangu wa kiume akafariki, ambaye alikuwa akilelewa nyumbani, kwa hiyo likatokea pengo kubwa sana.

Niliitwa siku moja na mzazi wangu wa kiume akaniambia kuwa ananihitaji nioe kwa lengo la kupata familia maana siyajui maisha yangu ya mbele, pia nizae mapema niweze kuja kuwatunza watoto nikiwa bado nina nguvu, kwa hiyo nianze kuangalia mwanamke ambaye atanifaa ili mwaka kesho ninapomaliza chuo nioe.

Nikamuuliza mbona bado mimi sijaweza kujitegemea wala kuwa na uwezo wa kuanzisha familia? Akasema nisiogope majukumu nioe atanipa msaada wa nyumba ya kuishi na mahitaji madogo madogo, ila sikuridhika kabisa maana sipendi kutegemea mtu sipendi kuwa mzigo ninapenda kufanya maisha yangu isitoshe nimeshakuwa mtu mzima sasa sihitaji fanyiwa kila kitu.

Hilo jambo sikukubaliana nalo sana ila sikumuonesha mzazi kuwa nimepinga ( asiyesikia la mkuu) Nikawapigia ndugu zangu wengine baba mdogo, mkubwa, mashangazi, na wengine wengi kuongea nao ili waweze kumpa wazo la mimi kutofanya hivyo ila waliniambia kuwa inanipasa nioe kwa kuwa mimi ni wa kwanza kwetu na hakuna mwingine wa kiume na ninategemewa kuendeleza kizazi, nilikosa la kujibu.

Ninajiuliza nitaepukaje hili jambo kwa sasa maana sipo tayari kabisa kuoa kwa sasa ikiwa sijajijenga na kuwa imara katika maisha, isitoshe mimi mwenyewe sina mahali pa kuniingizia kipato hata shilingi mia, ninaogopa vya kusaidiwa, masimango, kejeli, na tabu za hapa na pale.

Ninaona kama vile nitanyanyasika sana kwa kitendo hicho cha kuoa bila kuwa na kipato cha kueleweka, kwa kutegemea msaada wa watu, sitakuwa na uhuru kwenye maisha yangu.

Ninashindwa nitakwepaje hili suala maana nimejaribu kupinga kidogo, ninaonekana kama mbishi nisiyesikia ninaloambiwa na wakubwa, ninawafahamu ndugu zangu nikienda kinyume na ushauri wanaonipa itakuwa ngumu kwangu kupata msaada wa aina yeyote hata endapo sijaoa kama wanavyonishauri, je nifanyeje kujinasua kwenye jambo hili, na pia nibaki na amani na ndugu zangu? Kwangu hili suala ni la muhimu kabisa maana sio kwamba sihitaji ila sio kwa sasa.

Samahani wakuu kwa kuandika sana ila ninaomba msaada wa mawazo yenu, nimelitua hili jambo hapa nimesikia kidogo oxygen inapita vizuri kwenye mishipa yangu, nina imani michango yenu itakuwa na msaada mkubwa kwangu.

Asanteni.
 
Ukimpata mke mwema hayo mambo ya kazi na nyumba sio kesi sana.
Kuna watu wameoa walipomaliza darasa la saba na mpaka sasa hivi wanadunda na wake zao
Sawa sawa mkuu.

Mke mwema kwa sasa ni shughuli nzito sana kumpata.

Wengi wako kimaslahi.
 
natamani ningekuwa na huo umri wako nipate hiyo fursa
Fursa hiyo mkuu?

Sijui kwangu ninaiona kwa Jicho gani?

Napenda sana maisha ya kutokuwa mzigo kwa mtu mwingine.
 
Don't be pressured kuoa utajuta. Wewe ndo utakaekuwa ndani ya hiyo ndoa na si wao.

Sometimes you have no other choice zaidi ya kuwa mbishi, tena nunda, hata kwa wazazi na ndugu.

Sema mwambie hivi mzee, ushauri wake umeupokea na unafurahi kwamba he means well, ila wewe kwasasa suala la kuoa bado, unataka ufanye mambo mengine kwanza ukae sawa. Huko mbeleni Mungu akipenda mbona utaoa tu, wasiwe na wasiwasi. Mweleze na hasara za kulazimisha mtu kuoa.You have to be serious, ila respectful unapomkatalia.

Kuhusu kukutenga hawawezi, trust me. Either wanakuchimba mkwara tu, au you have a shit family(sorry) kama watakutenga kwa kitu kama hicho.
 
Badilisha line yako kisha njoo mjini utafute maisha. Ukifika 28 au 30 oa kisha rudi nyumbani ukiwa na pes 7 na mke mzuri 5star. Lazima wkueshimu
 
Ndoa ni tulizo la moyo kwa wenye kujitambua bila kusahau baraka tena,Inapendeza sana kwa umri wako
Sawa mkuu vipi kuhusu hiyo changamoto tajwa niliyoiongelea.

Hata mimi ninapenda kutulia na mtu mmoja ila ndio hivyo.
 
Kwasasa hauna kazi! Je unaonyesha juhudi za kuhangaika! unafanya nini.... hili suala la kuoa halipo kwako ungeshaoa

Utateseka na kumtesa mtoto wa watu I mean mkeo... pigana tafuta shughuli hata ya kuingiza jero kwa siku hata wakikusaidia huku unajisaidia watakuheshimu kidogo.
 
Badilisha line yako kisha njoo mjini utafute maisha. Ukifika 28 au 30 oa kisha rudi nyumbani ukiwa na pes 7 na mke mzuri 5star. Lazima wkueshimu
Daah mkuu wao ndio wanaweza nipa rqmani za mjini hapa pia kwa ukaribu zaidi, nikiwatenga hata hicho nitakachokuja kukitafuta yawezekana nikakikosa kabisa.

Halafu wakabaki wananiangalia tu
 
Don't be pressured kuoa utajuta. Wewe ndo utakaekuwa ndani ya hiyo ndoa na si wao.

Sometimes you have no other choice zaidi ya kuwa mbishi, tena nunda, hata kwa wazazi na ndugu.

Sema mwambie hivi mzee, ushauri wake umeupokea na unafurahi kwamba he means well, ila wewe kwasasa suala la kuoa bado, unataka ufanye mambo mengine kwanza ukae sawa. Huko mbeleni Mungu akipenda mbona utaoa tu, wasiwe na wasiwasi. Mweleze na hasara za kulazimisha mtu kuoa.You have to be serious, ila respectful unapomkatalia.

Kuhusu kukutenga hawawezi, trust me. Either wanakuchimba mkwara tu, au you have a shit family(sorry) kama watakutenga kwa kitu kama hicho.
Sawa mkuu ila nikiwa mbishi kumbuka hawatanitenga ila wataniondoa katika mahesabu ya kunipitisha njia wanazoona zitanifanikisha, kumbuka connection ina msaada mkubwa sana kibongo bongo.
 
Sawa mkuu vipi kuhusu hiyo changamoto tajwa niliyoiongelea.

Hata mimi ninapenda kutulia na mtu mmoja ila ndio hivyo.
Mbona hizo changamoto ni za kawaida,au mashine haisimami?
 
Mbona hizo changamoto ni za kawaida,au mashine haisimami?
Mashine inasimama 4g.

Historia niliyonayo kuhusu mahusiano, ni Mungu tu anisamehe, nimebadilisha wanawake, sitaki kukumbuka kabisa.
 
Kwasasa hauna kazi! Je unaonyesha juhudi za kuhangaika! unafanya nini....

Utateseka na kumtesa mtoto wa watu I mean mkeo... pigana tafuta shughuli hata ya kuingiza jero kwa siku hata wakikusaidia huku unajisaidia watakuheshimu kidogo.
Kwa sasa sina kazi, ninasoma masomo ya afya yanayonihitaji umakini na muda mwingi.

Hivyo basi nina biashara ndogo ndogo ninazofanya online tu nikipata muda, nikipata mteja natuma mtu anakwenda deliver mzigo.
 
Sawa mkuu ila nikiwa mbishi kumbuka hawatanitenga ila wataniondoa katika mahesabu ya kunipitisha njia wanazoona zitanifanikisha, kumbuka connection ina msaada mkubwa sana kibongo bongo.
Then anza kuhustle kivyako na wewe mdogo mdogo anza kutengeneza connection zako taratibu. Lasivyo always watakuwa wanatumia hiyo kama fimbo ya kukuchapia, kwasababu sasahivi itakuwa ni issue ya kuoa, next time pia watataka kwaajili ya issue nyingine. Yaani itaendelea hivyo hivyo. Always using their connections as leverage ya kuku-direct wewe cha kufanya.
 
Kwa sasa sina kazi, ninasoma masomo ya afya yanayonihitaji umakini na muda mwingi.

Hivyo basi nina biashara ndogo ndogo ninazofanya online tu nikipata muda, nikipata mteja natuma mtu anakwenda deliver mzigo.
unasoma... Waambie umalize shule kwanza.
 
unasoma... Waambie umalize shule kwanza.
Sawa hatabwao pia wanamaanisha nikimaliza shule tu.

Ila kama ni mchumba nipate kabla ya hapo na kuchumbia kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom