Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Rafiki yangu hapa mtandaoni, #Fareed_S. Al - Abeid ameniandikia kisa kifuatacho;
Ndugu Mtatiro, soma kisa cha mechi ya Yanga na Simba 1975 Nyamagana, Mwanza. Msafara wa Yanga uliposhuka Dodoma ulikua Mkubwa wa Kihistoria. Inasemekana Mwalimu alikuwapo Dodoma ...ulimshtua.
Mzee Mangara aliekuwa Mwenyekiti alikua pia Rafiki wa Mwalimu. Yanga walipofika Dar Es Salaam mapokezi yalikua makubwa sana..zaidi ya Dodoma.
Haikuchukua mwezi, Yanga ikaingizwa katika mgogoro mkubwa ambao haujawahi kutokea. Ilikua vita, Tambwe Leya aliyekuwa kocha aliyeleta ubingwa akatimuliwa na Yanga ikakatika vipande viwili, kipande cha Yanga na cha Pan Africa. Juhudi za Mangara kumuona Mwalimu kuokoa jahazi ziligonga mwamba! Yanga ikashuka daraja!
Simba nao wakafika Nusu Fainali kombe la Afrika na kutolewa na Mehhala El Kubra kwa penalti kule Cairo. Baada ya mechi hiyo Simba ilikua jina kubwa Afrika nzima na Afrika Mashariki, Umaarufu wa Simba ukawa mkubwa ukishindana na TANU, hawakuchukua muda ukatokea mgogoro mkubwa, kukawa na Simba ya King Kibaden na Haidar Abeid na Maulid Dilunga ikakatika vipande na kuzaliwa Red Star au Nyota Nyekundu
Kuanzia wakati huo soka la Tanzania halijaimarika mpaka leo. Haya pia yaliwatokea Coastal Union na Africa Sports za Tanga, timu pinzani ambazo zilikua na ushindani mkubwa kwenye soka la Tanzania, timu hizi zilidhibitiwa na dola kwa kuhusishwa na Yanga na Simba.
Mikoa iliyokuwa ikitoa wachezaji wengi makinda waliokuwa wanachukuliwa au kukimbiliwa na Simba na Yanga - ambayo ni Morogoro, Mwanza na Tanga ikafa kisoka, haikuwa bahato mbaya. Ni mipango tu.
Haya hayapo Simba na Yanga tu, hata FAT na Sasa TFF, zote zimekuwa zikitumiwa kwa maslahi ya dola na CCM na siyo uhalisia wa kukuza soka.
Na mara nyingi ukiangalia chanzo cha migogoro hakionekani ila kuna nguvu ya nje inayotumia Vyombo vya Habari kukuza migogoro hiyo.
Ni kweli, mfano umati kama ule ulio tokea kuwapokea Simba baada ya Kuwatoa Al Ahly ya Misri huwa unawatisha sana wanasiasa, wanaanza kuhofia kwamba vyama vyao vitaporwa utii na mamlaka na njia ya pekee inakuwa kuzitumia timu hizi kwa mbinu za hali ya juu na wakishindwa kuzitumia huziingiza kwenye mgogoro au mpasuko mkubwa.
Mzee Masonga wa Morogoro na Fareed, wanazidi kunitafakarisha sana.
[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J