Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,225
- 219,400
Kwenye nchi ambazo utendaji wa taasisi hauhitaji masihara, mteule mpya hasherehekei uteuzi wake. Mteule hatumii uteule wake kuwasimanga wengine ama kutengeneza mipasuko. Mteule wa huko hutumia uteuzi wake kutafakari namna atakavyotumikia cheo kipya kwa unyenyekevu na kwa mujibu wa sheria.
Msanii wa filamu duni za kuigiza za Tanzania, Jokate, alipoteuliwa kuwa Katibu wa Taasisi ya akina mama wa CCM (UWT), akaamini kwamba uteuzi ule ni wake binafsi na wasanii wenzake wasio na maadili. Akakusanya hao wadada wenye mashaka ya afya na kutengeneza Parade DSM na Dodoma, kuonyesha kwamba wananchi wamefurahishwa na uteuzi wake. Kama kawaida ya magazeti ya Tanzania, yakampamba ili yajipatie maokoto ya bure.
Mara papo hapo, Makonda naye akateuliwa kuwa Katibu wa Uenezi. Mwisho wa sherehe za Jokate ukafika, akapotea na kutoweka (hajulikani aliko hadi leo). Makonda naye akaanza sarakasi za ulimbukeni na kuanza kuandaa matukio yake mwenyewe. Akaanza kukaripia kila aliye mbele yake, as if CCM imezaliwa jana, huku yeye akiwa ndio muasisi wa ukatibu uenezi. Punda, farasi, bajaj, na malori ya kokoto vikatumika kuhadaa wajinga. Yaani, anatumia V8 kwa urefu wa maelfu ya kilomita, lakini anapanda punda mita 500 tu!
Sasa ujio wa Katibu Mkuu mpya nao unahitimisha kabisa maigizo duni ya Makonda. Tusubiri naye ataleta maigizo yale yale ama atatumia akili.