Jinsi nilivyounganishwa na dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi nilivyounganishwa na dunia

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Nov 7, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 7, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  NIMEUNGANISHWA NA DUNIA

  Sikuwahi kuota hata sikumoja kama kuna siku nitakuja kuungishwa na dunia kama ilivyo sasa hivi , lile neno la dunia kuwa kijiji kimoja sasa limeanza kutimia kwa kiasi kikubwa zaidi bila kujali mipaka , rangi , lugha wala utamaduni .

  Nimeshasajili namba yangu ya Zain kama kila mtanzania anavyotakiwa kusajili namba zake za simu zote kwa taarifa ambazo ni sahihi , unapoenda hapo unatakiwa kwenda na kitambulisho chako chochote nakala ya kitambulisho unaacha hapo uliposajili .

  Namba yangu hiyo ndio huwa naitumia pale ninapotaka kuangalia salio la pesa zangu kwenye benki , ninapotaka kutuma pesa siendi tena benki namtumia kwa njia hii ya simu kwa urahisi zaidi na gharama ndogo .

  Na sasa kwenye anuanu za barua pepe ninazotumia mimi nimetakiwa kuthibitisha kwa kuweka namba za simu ambapo nimetumiwa namba za siri kwenye namba hiyo kama mhalifu akijaribu kuingilia ataulizwa namba za simu ambayo ninayo mimi .

  Kwa maana nyingine sasa nikifanya uhalifu wowote kutumia barua pepe hizo za gmail ni rahisi wenye kampuni kunitambua kwa sababu wataangalia namba za simu , kwa kutumia vyombo vya dola wanaweza kwenda kwenye kampuni yangu ya simu wakapatiwa taarifa zingine za ziada .

  Moja ya huduma wanazotoa google ni kuhifadhi taarifa za mambo yote unayoyafanya kutumia anuani yao na popote ulipo , kuanzia vile unavyo search kwenye mtandao huo wakati ukiwa kwenye anuani hiyo mpaka wale unaowasiliana nao mpaka vikundi ambavyo umejiunga navyo

  Kuna hili suala la vitambulisho vya uraia , inawezekana ninapotakiwa kwenda kupata kitambulisho hicho taarifa ninazotoa zinatakiwa kuendana na zile zilizokuwa kwenye namba ya simu yangu au barua pepe yangu na kufuatilia hili ni rahisi tu kama nilivyoeleza huko juu .

  Kwa sasa niko makini sana siachi taarifa zangu kwenye mitandao tena na zile zilizokwepo nimeziondoa au kuondoa baadhi ya vitu manake mtu anaweza kutumia taarifa hizo kwa kuunganisha na kupata jawabu la kufanya uharamia , Huu ndio aina ya uhalifu unaokuja kwa kasi zaidi duniani .

  Nimeshaunganishwa na kijiji cha dunia sina wasiwasi wowote , hata wewe umeshaunganishwa kwa njia moja au nyingine .

  Wale waliokuwa wanasikia kitu kinachoitwa NEW WORLD ORDER huu ndio mfano wake .
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Uko sahihi Mkuu.

  Kwa watu ambao ni wakamilifu kimienendo wana kila sababu za kufurahia hii NEW WORLD ORDER kama ulivoiita! Ukiona mtu anasitasita na kupinga mabadiliko haya ujue ana yake mambo!

  Kwa kweli sasa simu imekuwa na maana kuliko mwanzo!

  Ukiwa na Salio kwenye simu, au huko Benki ndo umemaliza kila kitu!...Kwahiyo mduara unarudi palepale, kwamba Pesa yako inakurahisishia mambo yako...SO MAKE SURE YOU HAVE MONEY ALWAYS!
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  nyie mlidhani Biblia inadanganya? "No man shall be able to trade without the mark of the beast - 666". Sasa imebaki kidogo tu..game iishe. Moving from this step to the next is very easy! Wazungu wanasema we take incremental steps instead of huge leaps. Ndo hiyo sasa. Kesho utasikia hauhitaji pesa ya makaratasi tena. Mimi ninapoishi, unaweza usitumie pesa ya makaratasi kabisa! Na sio useme tunatumia credit card!! Card zao ni design ya debit card, kwa hiyo pesa inatoka kwenye account yako directly. Yep...ndio wanaita maendeleo, huku hawajui ndo tunafika mwisho!!
   
 4. S

  Senghor Member

  #4
  Nov 7, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  SHY
  hongera kwa kuunganishwa moja kwa moja na KUZIMU maana wanacontroo kila kitu chako ulichosajili kupitia namba yako.

  wanaposema 666 wanamaanisha muunganisho wa code namba ambao hauzidi tarakimu tatu. utakuta ni mbili au moja au tatu ila inaweza kugawanyika kwa witiri au shufwa ndo maana wakaleta 666. mwenye akili na afunguke sasa
   
 6. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mwisho umekaribia maandiko lazima yatimie mpinga kristo at work
   
Loading...