Jinsi nilivyougua miaka mingi na kunusurika kifo baada ya kurogewa uchawi wa bundi

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau poleni sana na msiba wa jemedari Hayati Magufuli.

Leo nimeamua kuwaletea simulizi ya kweli inayoitwa "jinsi teseka miaka mingi na kunusurika kufa baada ya kurogezewa uchawi wa bundi".

Kwanza niwaombe samahani kwa mwandiko mbaya maana simulizi hii ninapoanza kuiandika inaweza kuonekana fupi ila inaweza ikawa ndefu hivyo basi mniwie radhi kama kutakuwa na kukatishwakatishwa.

Wahusika wa story ni watu wa kweli kabisa wala sio watu wa kufikirika na maeneo ni ya kweli sio ya kufikirika,ila ningeomba kutumia majina ya kufikirika maana sio vizuri kutumia majina yao halisi.

Lengo la kuleta story ni watu wajifunze wajue uchawi na uganga dunia upo na waganga wa kweli wapo,pia kuburudisha hilo ndio lengo.

Twende kwenye story yenyewe...

Ilikuwa mwaka 1975 katika kijiji cha Bunduki kata ya Bunduki wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro ndipo simulizi ilipoanzia.

Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa darasa la tano katika shule moja ya msingi kijijini hapo ambayo sitopenda kuitaja jina.Siku hiyo nilirudi nyumbani mishale ya saa 8 mchana nikiwa nimechoka sana na nilipofika nyumbani nikakuta kuna kasherehe ka kumtoa mwali, kama unavyojua tamaduni zetu za kiafrika hivyo watu walikuwa wamejaa sana huku wakipiga ngoma ijulikanayo kama Mbeta hii ni ngoma maarufu sana kwa wenyeji wa mkoa wa Morogoro hususa wa kabila la waruguru.

Nilifika nyumbani nikaingia ndani kubadilisha nguo za shule ambazo zilikuwa chafu zilizochakaaa na udongo wa kijijini kama wengi tunavyojua udogo wa Morogoro nakukimbia fasta kwenye ngoma.

Mwanamwali alikuwa ni dada yangu aliyenitangulia kwa sasa ana kama miaka 75 (watu wa zamani sana wengi wao hawajui miaka yao halisi ,hususa wale ambao hawakuenda shule .Huwa wanaweza kukutajia tu kipindi ,msimu au matukio ww ndio utang'amua umri wa makadilio wa mtu huyo kama haufahamu kuhusu matukio au vipindi hivyo vilitokea lini unaweza kushindwa hata kukadiria umri halisi).Hivyo basi umri wa dada kama miaka 75 katika simulizi hii ni kama makadirio tu wala visikupe shaka juu ya ukweli na uhalisia wa simulizi hii..

Basi baada ya kubadilisha nguo na kuingia moja kwa moja kwenye uwanjani ambapo mwanamwali ambaye ni dada yangu anachezwa hapo ndipo story, visa, mkasa, simanzi zilipoanzia.

Hapo kutakuwa na mambo ya kuvunja nazi, makafala ya wanyama kama mbuzi au ng'ombe na shughuri zingine pamoja na kufukia vitu au dawa kwenye makabuli au miti mikubwa kama ni matambiko.

Kwa wenyeji wa Pwani wanatambua utamaduni wetu kama kawaida ngoma inapowekwa uwanjani siku au wiki kabla haiawekwa uwanjani lazima watu waende kwa mganga kuzindika au wanaweza wakawaita wazee kufanya matambiko. Matambiko au mazindiko lazima yatanuwiwa kwamba yeyote atakayekuja kwa ubaya siku ya sherehe au shughuri ya kumtoa mwanamwali wetu basi haondoke kwa ubaya.

Nasi tulifuata taratibu zote za zindiko na matambiko kama utamaduni wetu lakini sasa siku hiyo mambo yalikuwa tofauti yaani chuma kilikutana na chuma.

Tukumbuke tupo mwaka 1975 kipindi hicho dini na imani hazikuwa zimeenea sana kivile hivyo hatukuwa na budi katika kuamini mizimu ,matambiko,mazindiko na vinginevyo.

Inandelea...
images.jpeg
 
Aisee umevunja rekodi ya watoa story wote mkuu hii yako ni fupi hatari yaani aya mbili tu.
Ushauri: Andika ndefu kidogo pembeni (kwenye app ya notepad au computer) afu upaste hapa mkuu.
Baba simu yangu mtoto kavunja kioo jana, hapa naingia JF kupitia sim ya wife ndio tatizo hilo nikishika simu anajua naikagua.
 
Endelea...

Basi bwana goma lilipigwa pale watu walicheza wakanywa pombe mpaka wakalewa.

Labda nikupe picha ndugu msomaji tu jinsi tukio linavyokuwa yaani wakati mwali anachezwa anakuwa kifuani yupo mtupu yaani chuchu nnje chuchu konzi na anakuwa anazungushwa uwanja mzima kila mtu amuone.

Hii inafanyika baada ya binti ambaye amefikisha umri wa kubarehe au kuvunja ungo kuwekwa ndani zaidi ya miezi kadhaa.Ikiwa ndani upatiwa mafunzo ya kuishi na muwe pamoja na walimwengu (kufundwa). Kunakuwa hakuna mwanamme yeyote anayeruhusiwa kwenda kumuona wakati yupo ndani.

Wakati ngoma inaendelea walikuwa watoto kadhaa ambao ni wa rika langu wakiwa na kanga na kunifunika kichwani tukawa tunacheza huko nikiwa nimefunikwa.

Ngoma au sherehe ilidumu kwa mda wa siku mbili huku watu wakiendelea kunywa na kufurahi, lakini baada ya siku ya kwanza ya ngoma kuisha nilianza kujihisi vibaya yaani kama kichwa kinaniuma ila niliona itakuwa ni uchovu tu. Baada ya siku kadhaa tatizo la kuumwa na kichwa liliendelea nikajikuta nashindwa hata kuona mbele hivyo ilinilazimu kupelekwa hospital kuchunguzwa ili kubaini tatizo.

Nilipofika hospital nikaambiwa nina malaria hivyo nikapatiwa dawa za kutuliza homa na nikarudi nyumbani.

Licha ya kupatiwa dawa za kutuliza homa na kumeza yaani hata baada ya wiki nzima kupita bado sikuona mabadiliko yeyote.

Hapo ndio bibi akashauri kutokana na mila na desturi ikitokea kijana akaumwa kwa muda kidogo na njia za hospital kushindikana wao huwa wanaamini inaweza ikawa ni "jina" .Nini maana ya "jina" jina utokea pale mtu aliyekufa zamani (mzimu) kwa upande wa kike au wa kiume anapoitaji akumbukwe katika ulimwengu wa dunia hivyo anachagua mtu ambaye ataitwa kwa jina lake hata kama teyari mtu huyo alishapewa jina hivyo anafinywa (anaumwa) mpaka atakapoenda kwa wazee kuuliza chanzo cha kuumwa nao wazee upiga ramli na kuwezeshwa kwa uwezo wa mizimu kugundua ni mzimu wa nani unataka kukumbukwa .Ikibainika jina la mzimu mtoto aliyekuwa anaumwa utambikwa na kupewa jina la mzimu huo (ndugu aliyekufa zamani) hivyo basi hata kama mtoto aliumwa kwa kiasi gani pindi tuvanapolipokea hilo jina kama jina lake upona papo papo.

Baada ya bibi kushauri tuangalie jina huwenda likawa ndio chanzo cha tatizo ndugu hawakusita walifanya kama walivyoagizwa .

Hapo tulilazimika kusafiri kwenda kijiji cha jirani kijulikanacho kama Chienzema,nikiwa nimebebwa mzobe mzobe yaani nusu hai nusu kaputi mpaka kwa wazee wa mizimu ila baada ya kufika katika kijiji cha Chienzema wazee waliniagua lakini ramli zao hazikuona jina lolote la upande kiumeni wala kikeni (yaani upande wa kwa baba wala kw mama).

Hapo ndipo mambo yalipoanza kuwa magumu na wanafamilia walipoanza kukata tamaa wasijue nini cha kufanya.

Itaendelea...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom