Jinsi nilivyonusurika kutapeliwa!

Hawafai mkuu, wakiona umesanuka wanatoka nduki kubwa..

Tuwe macho jamani..
Kweli hii dunia tunatofautiana kufikiri. Yaani mtu anafedha za kubadilisha na humjui, anakuja anakuomba umsindikize halafu akugawie milioni 1 na wewe unaona kila kitu kipo sawa!!!!!!! Ujinga ilioje! Kwanza alipokufuata kukuomba eti mambo ya kujaza kwani umeajiriwa benki? Just ungemwambie aone wahusika! Jifanye kuzoea watu haraka haraka kuna siku utafanyiwa kitu kikubwa kuliko hicho!
 
Na ungeibiwa ingekuwa vizuri sana kwasababu wewe ndio ulitaka kuiba. Kwa kifupi wewe na huyo mwanzisha thread ni wezi! Mtu atakuja akuambie umwonyeshe sehemu halafu upate malipo makubwa namna hiyo bila kufanya kazi? Eti ametoka shamba! Kwa hiyo wewe ulijiona ni mjanja na utumie ushamba wake kufaidi siyo?
 
Pole na hongera kwa kufuatilia mpaka ukaujua mchezo wote! Naamimi utakuwa umesaidia wengi. Nikishauri tu uitaje hiyo benki ili hata wao watoe tahadhari stahiki kwa wateja wao.
Asanteh mkuu,

Benki yenyewe inapendeleaga rangi ya kijani nadhan utakuwa umeifaham mkuu..!
 
Duh! Mkuuu kumbe nawewe walikutoa nje ya benki kama mimi!
 
Ni sawa mkuu,
 
Mimi nikiwa bank au kwny ATM huwa sitaki maongezi na mtu nisiyemjua
 
Futa hiyo kauli yakusema mimi ni MWIZI tafadhari mkuu

Lengo langu ni kuwajuza watu yalonisibu ili wachukue tahadhar sababu haya ni maisha ofcorse hakuna anayejua kila kitu.... ila wewe unajiona much know
...ok it's up to you
 
Mimi nikiwa bank au kwny ATM huwa sitaki maongezi na mtu nisiyemjua
Mkuu uko kama mimi. Dunia ya sasa sio ya kuzoeana na watu kirahisi namna hii. Unakuta mtu anakuambia nina fedha nabadilisha na wewe humjui unaunga tela. Kama ni jambazi ameua na anafuatiliwa mkikamatwa utamwambia hakimu ''alikuokota'' benki wala hamjuani akuelewe?
 
Ngoja waje wanitokee mm tena nikiwa bank nawakomalia wasitoke had kwa mapolisi wale wa bank! Hapo ndio watakoma kuingia bank.
Hahaaa
Nooo! Usiweke ukaribu nao hata zero distance sababu wengine sio watu wazuri wana madawa wanakupulizia utatoa bila kupenda....
 
Futa hiyo kauli yakusema mimi ni MWIZI tafadhari mkuu

Lengo langu ni kuwajuza watu yalonisibu ili wachukue tahadhar sababu haya ni maisha ofcorse hakuna anayejua kila kitu.... ila wewe unajiona much know
...ok it's up to you
Mkuu mimi nikuulize swali? Hiyo milioni moja aliyokuahidi na wewe ukakubali kwenda unaona ilikuwa ni haki yako kuipata? Si inaonekana ulimwona jamaa kama ni zoba hivyo uka-take advantage?
 
Da! Nilikutana na hii kitu mwaka 2013.hawa jamaa wananusa Sana hela.

Jamaa alikua Anatokea stendi kashika Bahasha akanisimamisha,baada ya salamu, "samahani unaifahamu hoteli(akaitaja) nikamjibu ndio, akaniambia yeye ni Mgeni anaenda kukutana na mtu hapo ampe mzigo(akafungua kidogo ile bahasha) mamaaaaaaaaaaaa vitu vinang'aa hatari. Akasema hizi ni dhahabu natakiwa kwenda kumkabidhi anipe hela,naomba unipeleke.KICHWANI ZIKAWA ZISHACHAJI MDA MREFU NIKAWA NA MCHORA TU! Nikamwambia,me nna kazi zangu saizi ntakuelekeza hutapotea.
Akatokea jamaa mwingine akawa kama anatupita hivi(mwenzake) akamsimamisha,akamuuliza kama ana ijua hiyo hotel, akasema haifahamu, jamaa akasema huyu anapafahamu ila anasema hana muda,akamwambia kama alivoniambia Mimi na akamwonesha madini hewa. Jamaa akatuahidi hela nzuri tukimpeleka. Basi jamaa akaanza kunishawishi balaa.. Kimoyo moyo nikawa nawacheka tu.nikawambia sasa hizo hela utatoa kweli, jamaa akasema ndio, nikawambia sasa nisubirini kidogo(dakika sifuri) niweke huu mzigo (nilikua nimeshika spea ya gari naelekea garage.
Wakanambia poa, SIJUI KAMA BADO WANANISUBIRI MPAKA LEO, mfukoni nilikua na hela moja hivi! Wale jamaa sio watu wazuri,ukiingia Tamaa tu umelia
POLE MKUU KWA USUMBUFU WALIOKUSABABISHIA NA HONGERA KWA KUWATAMBUA
 
Mimi nikiwa bank au kwny ATM huwa sitaki maongezi na mtu nisiyemjua
Yah pengine inaweza kuwa ni dawa but i think it not enough mhimu hapo kuacha tamaa ya pesa tu umeshinda kila kitu
 
Mkuu mimi nikuulize swali? Hiyo milioni moja aliyokuahidi na wewe ukakubali kwenda unaona ilikuwa ni haki yako kuipata? Si inaonekana ulimwona jamaa kama ni zoba hivyo uka-take advantage?
Ni sawa mkuu lakini sio fair kuniita MWIZI

Mwizi anachukua mali ya mtu bila ruksa sasa mimi nilikuwa naiba nini?
 
Hongera ulichomoka blocker hakuwa mzuri ndicho kilicho kuokoa vinginevyo ungelia kwenye biashara yoyote mwangalie sana yule anayeongezeka huyo ni bloke's akikusa umeshinda mchezo
 
Asanteh mkuu,

.. hata mwanzo wazo la kuwa hawa ni matapeli lilinijia lakin nilikuwa nikiwachora tu... nijue wataishia wapi lkn kimoyo moyo niliapa sitawapa hata thumuni yangu shenz zao wale....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…