Jinsi nilivyokaa siku 100 bila kuangalia saa

chai ya rangi

Senior Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
130
Reaction score
405
Kuna kitu nilifanya mwaka jana ambacho watu wengi waliniona kama nacheza mchezo wa ajabu kidogo.

Nilikaa siku 100 nzima bila kuangalia saa.

Hakuna sababu maalum. Sikuamka asubuhi nikasema tu moyoni, “leo naanza.” Nikajiambia nione kama inawezekana kuishi kawaida kabisa bila kujua muda ni saa ngapi.

Kitu cha kwanza nilifanya ni kuacha kabisa kuvaa saa ya mkononi. Ile saa ya ukutani nayo niliiondoa pale sebuleni kwa sababu nilijua macho yangu yataikimbilia tu bila kufikiria.

Simu yangu nayo nilijitahidi sana nisiangalie sehemu inayoonyesha muda.

Mwanzoni ilikuwa inanisumbua kidogo. Unajikuta mkono unaenda mfukoni kuchukua simu halafu ghafla unakumbuka, “hapana, leo siangalii saa.”

Lakini baada ya siku chache nikaanza kuzoea.

Nilianza kuamka tu bila kujua ni saa ngapi. Nikihisi njaa nakula. Nikihisi usingizi nalala. Siku zinaenda tu bila mimi kujua muda umefika wapi.

watu wengi walikuwa wanashangaa.

Mtu anakwambia, “sasa hivi ni saa ngapi?”
namwambia sijui.

Wengine walidhani natania.

Lakini ukweli ni kwamba kwa zile siku 100 sikujua kabisa muda ni saa ngapi kwa siku yoyote.

Na kitu nilichogundua ni hiki: baada ya muda mwili unaanza kujipangia mambo yake tu. Unahisi tu muda wa kula umefika, muda wa kupumzika umefika, au muda wa kwenda nje umefika.

Kuna siku nilikaa na watu wakawa wanabishana muda umeenda haraka au polepole. Mimi kichwani kwangu siku ilikuwa inaenda kawaida kabisa.

Changamoto pekee ilikuwa pale mtu anaponiambia tukutane saa fulani. Hapo nilikuwa namwambia tu anipigie au anifuate maana mimi sina habari na saa.

Baada ya kufika siku ya 100 ndipo nilipoamua kuangalia saa tena.

Nilihisi kama nimeingia tena kwenye ulimwengu ambao kila mtu anaishi akifuatilia namba tu ukutani.

Lakini ukweli ni huu…

Inawezekana kabisa kuishi bila kuangalia saa.

Na saivi nampango wa kukaa siku 300 kwamaana inatuliza akili
 
Obviously wewe ni kula kulala,maana wewe kwa siku zote mia ulikuwa unakula unashiba unalala means haujawahi kuwa na issue siriaz ya kukufanya ujue ratiba ya jambo fulani ulifanye saa ngapi na wapi ili mkono uende kinywani.
 
ni kichaa tu anaweza kuishi bila kuangalia muda
Napata picha unajiamkia tu asubuhi hujui ni saa ngapi hujui kama umechelewa kuamka ili ujue utajiandaa kwa muda gani,kituo cha kazi reporting time ni 08:30 asubuhi wewe uingie pale saa 09:40.

Yaani huyu jamaa sijamuelewa kabisa huyu.
 
ni kichaa tu anaweza kuishi bila kuangalia muda
Napata picha unajiamkia tu asubuhi hujui ni saa ngapi hujui kama umechelewa kuamka ili ujue utajiandaa kwa muda gani,kituo cha kazi reporting time ni 08:30 asubuhi wewe uingie pale saa 09:40.

Yaani huyu jamaa sijamuelewa kabisa huyu.
 
Nimesoma hii habari yako ya kutoangalia saa mbona sioni faida zake? ,

Kwanza saa haina madhara yoyote kiafya zaidi ya faida zake nyingi.
Kama ungegeuza kujinyima kwako kuangalia saa ukajinyima kitu kingine kisichofaa kama chakula,pombe, tabia mbaya ungefaidika sana
 
Next task:
Siku mia bila simu then uje utuletee mrejesho.
 
Ukiweza kuishi bila kutumia smartphone utakuwa umeshinda, mimi kwangu naona faida ya smartphone ni ndogo sana, zaidi ya kupotezeana muda tu.

Najua kuna wengine wana mambo ya muhimu sana kwenye smartphone wanafanya kazi za pesa ndefu.

Ila kwangu mimi tofauti ya smart phone na kiswaswadu ni kuperuzi tu na ndiko kunapo nipotezea muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…