Jinsi nilivouza simu ya mtu kwa TSH 500 (2006)

Jinsi nilivouza simu ya mtu kwa TSH 500 (2006)

Sambinyakwe kitololo

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2022
Posts
2,429
Reaction score
2,970
Habari za muda huu mabibi na mabwana

Asee nimekumbuka mbali Sana, nakumbuka mwaka 2006 wakati naenda mafundisho kwa ajili ya kupata ubarikio nilikuwa huwa naongozana na mdada mmoja majirani tunasoma nae huko mafundisho ila shule ilikuwa Ni paka na panya kwa maana nilikuwa nasoma St kayumba na yeye anasoma English medium

Sasa siku moja wakati tunaenda mafundisho mdingi flani anauza au kusambaza nyama na Toyota pickup kwenye mabucha yeye pia ana bucha alikuwa amevaa buti nyeupe, koti jeupe na suruali Sasa akiwa anashuka kwenye gari akashushe nyama akadondosha simu ndogo sikuweza itambua kwa wakati ule ,

Yule dada na yeye aliona akanambia ikabidi nivuke Barabara nikaichukue nimpe , wakati nasubiri magari yaishe akapita mtu akaichukua nikamfata tukaenda nae mbali kweli nikamwambia umechukua simu sio ya kwako nimpe nimrudishie jamaa akasema nitakupa twende nisindikize Hadi pale tukaenda wee kufika sehemu akatoa jero la noti akanishikisha mkononi kidogo hiace hi hapa kapiga mkono kadandia akaambaa na Mia nikabaki na jero yule dada aliona na alikasirika Sana

Toka miaka hio yule mdingi wa kimasai huwa habadiliki Wala hazeeki hapa enyewe nimemuona Kama majuma mawili Sasa toka nimuone Mara ya mwisho na shughuli yake ile ile na pick up no A old sana anasambaza nyama mabuchani

Natamani nimwambiage sijui Kama atakumbuka hata
 
Back
Top Bottom