SoC02 Jinsi mitandao ya kijamii ilivyokuza kipato changu

Stories of Change - 2022 Competition

frankkilulya

JF-Expert Member
Apr 6, 2022
456
1,166
Kuwepo kwa Teknolojia kumepelekea kutokea mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yamepelekea kurahisisha matumizi ya kazi za binadamu ya kutoka katika ugumu na kuwa katika urahisi.

Mojawapo ya matokeo ya Teknolojia nia kuibuka kwa Mitandao ya Kijamii ambayo inawakutanisha watu mbalimbali kutoka katika pande zote za dunia na kuwaweka pamoja . Mfano wa mitandao hiyo ni Facebook, Instagram, Twitter, JamiiForums, Youtube, WhatsApp, Telegram, Viber na Mingine mbalimbali.

Matumizi ya mitandao hii yana faida na hasara zake Lakini zinatokana na mtumiaji mwenyewe jinsi atakavyoamua kuitumia ndivyo matokeo yake yatatokea faida au hasara.

Kupitia mitandao hii kunapelekea kufanyika kwa urahisi shughuri za kibiashara mbalimbali ambazo watu wanazifanya ili kuwaingizia kipato na hatimae kuwa na maisha bora.

Kupitia nakala hii tutaangalia jinsi nilivyoweza kutumia mitandao hii ya kijamii na kukuza kipato changu pia tutaona na changamoto zilizojitokeza kwa namna moja ama nyingine.


JINSI MITANDAO YA KIJAMII ILIVYOPELEKEA KUKUZA KIPATO/UCHUMI WANGU.

Kipindi naanza kutumia simu janja sikuwa na uelewa mpana sana kuhusu matumizi ya mitandao hii ya kijamii ndio nilikuwa nimetoka kumaliza elimu yangu ya form four. Hivyo wakati nasubiri kuendelea na elimu yangu, mmoja ya marafiki zangu wa karibu zaidi alikuja na kuniambia kwamba ana simu janja mbili anataka kuziuza hivyo nimtafutie wateja, Sikutumia nguvu kubwa sana kutafuta mteja kwani tayari nilikuwa nina marafiki wengi kwenye mtandao wa facebook ambao nilikutana nao na hapo nyumba sikua najuana nao.

Hivyo Nilichukua maamuzi ya kuzituma picha za zile simu janja kwenye mitandao hiyo kupitia ukurasa wangu na kuruhusu watu kutoa maoni yao na kufanikiwa kupata mteja. sikuishia hapo tu kuuza simu hizo mbili niliendelea pia kuuza baadhi ya vitu mbali mbali kama nguo, viatu, n.k

Hivyo nilitumia fursa hii kuona baada ya kuona kwamba kupitia mitandao ya facebook napata wateja kwa muda mchache zaidi nikaanza kutuma na bidhaa nyingine na kufanikiwa kuziuza.

Nilipata uzoefu na hatimae kuingia katika mitandao mingine kama instagram na Telegram na kuendelea na shughuri yangu ya kuuza vitu mbalimbali. mpaka kufikia siku za hivi karibuni bado ninaendelea na shughuri hii Ninafanya biashara yangu pia nina makubaliano na baadhi ya wenye maduka kuwatangazia biashara zao kupitia kurasa zangu za mitandao ya kijamii ambazo zina wafuasi wengi sana . kila bidhaa itakayouzika nita asilimia kadhaa au malipo ya tangazo moja moja.

Kupitia mkasa huu tunaona kwamba unaweza kuingiza kipato kupitia mitandao hii ya kijamii na kukuza hali yako ya uchumi pasipo kutumia nguvu kubwa sana wala pasipo kuwa na mtaji mkubwa sana.

Sio lazima uwe mfanyabiashara ndio ufanye kitu kama hiki ni mtu yoyote tu ata kama huna biashara lakini kama wewe ni mfanyabiashara iwe yoyote ile unapotumia mitandao hii uwezo wakukuza biashara yako na kupata wateja wengi zaidi ni mkubwa.

Kwa wale ambao wangependa kuanza kuitumia mitandao hii na kukuza kipato chao.

Kwanza kabisa chagua ni kitu gani unachotaka au unachopenda kufanya kama biashara. kuna biashara za aina mbali mbali

•Biashara ya bidhaa za kushika zinazouzwa na kusambazwa mfano..Nguo, viatu, vyombo, simu, makochi, vyakula, vinywaji n.k

•Biashara ya hudumua ambazo zinaweza kuwa ubunifu wa logo, ubunifu wa kadi, huduma za kibank, uwakala n.k

Unachotakiwa kufanya ni

fungua account yako ambayo itabeba jina la huduma unazozitoa ili kuwarahisishia wateja wako kuelewa akaunti hii inahusika na biashara gani.

Weka taarifa zako za mawasiliano ambazo muda wote zitakuwa zinapatikana ili kuwarahisishia watu kukupata wewe kwa muda sahihi.

Penda kutumia mitandao hii ya kijamii kwani ndio kunapelekea wewe kujifunza zaidi na kujua muda wa kuwapata wateja na kuwafikia wengi kwa kwa haraka zaidi.

Kupitia mitandao hii ya kijamii unaweza pia kuanza kutuma makala mbalimbali kama

•Makala za kuelimisha

•Makala za Michezo na burudani

•Makala za vichekesho

•Makala za habari

Ambapo vyote hivi vinawafuasi wengi zaidi watakopelekea kuifuata akaunti yako na utakua na wafuasi wengi ambapo utapata wadhamini na utaanza kutangaza biashara zao na kupata kipato chako.

Pia kwa wale Watunzi wa Tamthilia na riwaya mbali mbali Sehemu hii ya mitandao ya kijamii ni fursa pia ambao utaweza kupata mashabiki wengi wa riwaya na tamthilia zako na kuaanza kuwauzia kwani watu wamekuwa wakipendelea sana kusoma vitu kupitia mitandao na kujifunza zaidi. unapokuwa mtunzi una uhakika zaidi wa kuwauzia watu riwaya zako pasipo kutumia gharama ya kwenda kuchapisha vitabu na kuanza kusambaza ila kupitia mitandao utauza kwa urahisi zaidi ata kwa yule mtu ambae atakuwepo mbali zaidi.


CHANGAMOTO ZINAZOWEZA KUTOKEA

Baada ya kuona jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kubadilisha kipato cha mtu. Siku zote kila sehemu kunakuwa na changamoto ambazo zinajitokeza hapa na pale. Zipo changamoto nyingi lakini nitagusia baadhi ambazo Binafsi mimi nilikutana nazo.

• Wateja wengi sana wamekuwa sio waaminifu hasa pale ambapo mnakubaliana ili biashara ifanyike lakini pindi unapompelekea anakuwa hapatikani au sehemu aliyokuelekeza siyo alipo. Hii ni moja ya changamoto inayoweza kujitokeza mara kwa mara.

• Pia mnaweza kukubaliana bei halafu mkikutana na mteja anataka tena apunguziwe bei hii ni kawaida watu wengi hasa watanzania wanapenda sana kupunguziwa bei.

• Vifurushi vya intaneti kupanda na kubadilika mara kwa mara kila kukisha navyo vinaprlekea mtu biashara yake kuwa na changamoto kidogo kwani kufanya biashara mtandaoni unatakiwa mda wote kuwa hewani ili mteja anapokutafuta basi apate jibu kwa wakati huo huo kabla hajafikiria maamuzi ya kubadilisha mawazo yake.

Wapo baadhi ya watu asilimia kubwa wanaichukulia mitandao kama sehemu ya kujifurahisha na kupoteza muda ni kweli upande mwingine ni sehemu ya kujifurahisha lakini tunaweza kuitumia vizuri zaidi ili kuongeza vipato vyetu hasa katika kipindi hiki ambapo ajira zimekuwa chache sana.

Teknolojia imekua sana kila kukisha vitu vimekuwa vikibuniwa na kurahisisha shughuri zetu kwa urahisi zaidi na kwa kutumia mda mchache zaidi ikilinganishwa na zamani kabla ya mapinduzi ya teknolojia.

Mfano siku za hivi karibuni Kampuni ya META kupitia programu yake ya Facebook wananakipengele maalumu kwaajili ya wafanyabiashara ambapo bidhaa yako inauwezo wa kuwafikia watu wengi zaidi walipo eneo lako kwa mda mfupi zaidi na kurahisisha mawasiliano yenu.

Hivyo wakati tukiangaika kutafuta kuajiriwa pia tunaweza kujiajiri wenyewe kupitia mitandao hii ya kijamii na kuongeza kipato chetu cha kila sikua

Tutumie mitandao hii vizuri ili tuweze kukuza uchumi wa Nchi yetu.

Kwa leo naomba niishia hapa.
 
Back
Top Bottom