Jinsi Mc wa Ifakara alivyonipa fedheha mbele ya umati

Jinsi Mc wa Ifakara alivyonipa fedheha mbele ya umati

pole sana, hawa ma mc sio watu wazuri niliwahi kuikimbia sherehe baada ya kudharilishwa, mchango nilitoa kabsa TZS 5000
ata msosi sikuusubili!
ma mc sio watu wazuri!!
 
Nimecheka kama mwehu.

Mm nilicheka pale ulivyopanga utatoa elfu mbili baadae kiwewe kikakushika ukaitaja kuitoa yote. But then ukaamua kutoitoa kabisa
 
Kosa ni lako mwenyewe ,hapo ulitakiwa uahidi tu kisha kitaa mtajuana na wahusika kimyakimya sasa wewe ukasema una buku 4 kwa nini usichekwe?
 
Kama ni kweli basi ulikosea pale ulipoulizwa jina ungetaja jina la yule rafiki yako uliyetumia kadi yake, na hata baada ya kuitwa pale mbele ungeendelea kutumia jina lile lile na ungetoa ahadi hata ya sh milion moja ungepigiwa makofi na pengine ungeng'oa demu mkali ukaenda kuchakata mbususu kimasikhara
 
Kama ni kweli basi ulikosea pale ulipoulizwa jina ungetaja jina la yule rafiki yako uliyetumia kadi yake, na hata baada ya kuitwa pale mbele ungeendelea kutumia jina lile lile na ungetoa ahadi hata ya sh milion moja ungepigiwa makofi na pengine ungeng'oa demu mkali ukaenda kuchakata mbususu kimasikhara
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana ndugu...

Ila seriously hii nchi tumekuwa na utamaduni mbovu sana yaani ni omba omba kuanzia Rais wa nchi mpaka raia..., ni mambo ya Harambee kila kona
 
Nilienda Kwa jamaa yangu Ifakara kusikilizia harakati zinavyoenda ikiwezekana na mimi nijichanganye area hizo ili niweze pata chochote so ikawa tunadamka asubuhi tunaenda ofisini kwake then jioni tunageuka.

jamaa yangu ni mtu wa kujifutafuta(smart) na mimi ikabidi nijitahidi Kuwa Smart nikawa napiga kicorporate kasoro tai tu shingoni kumbe kuna majirani zake wamezimia mziki. ule usmart ukawaaminisha kuwa pesa zipo kumbe ni vile umaridadi uficha umasikini.

Kipindi nafanya field bank nilipewa form six na t-shirt za benki zakutosha nilikuwa na utamuduni wa kuvaa zile t-shirt wikiendi basi wale majirani wakaconclude kuwa Mimi ni muajiriwa wa benki kumbe nilikuwa jobseeker.

Jamaa yangu alipewa kadi ya mualiko kwenye sherehe ya kipaimara ya moja wa mtoto wa jirani zake badluck hiyo siku jamaa alienda Morogoro akanipatia ile kadi nikamwakilishe.

Kama kawaida Mzee nikatinga t-shirt langu la benki nikaenda kuwakilisha kwenye sherehe nilipokelewa na bashasha za kiwango cha juu nikaonyeshwa sehemu ya kukaa na kupewa msosi na kinywaji.

Kumbe Ifakara sio kwetu Namtumbo, kumbe huku utaratibu wao ni kuwa Kila tukio mnaitwa kuchangia pesa tena unasema kiwango unachotoa ile sherehe ilikuwa ina matukio kama manne hivi kwanza kuchangia mavazi ya mwali, pili keki, tatu shampeni na nne zawadi.

Mzee mfukoni nina Tanzania shillingi 4000, elfu mbili ndio nilikuwa nimepanga kumpa mwali zawadi alafu buku mbili inayobaki nikomae nayo mwenyewe.

Mc akaanza kuita watu Kwa mbwembwe yule mama shughuli akaja kuniuliza unaitwa nani nikamtajia jina nikamuona anampelekea Mc kikaratasi.

Baada ya dk Tano Mc akaanza namnukuu "Sasa anakuja mtu mwenye hatimiliki na pesa bila Saini yake yeye pesa haingii kwenye mzunguko Kwa heshima yake nyote msimame tusije kumuudhi si unajua pesa hainuniwi si mwingine ni.. akanitaja Mimi kutokea benki ya(ile t-shirt niliyokuwa nimevaa)" mheshimiwa karibu sana" nikapewa mic kiukweli nilipata mshituko sana na mfadhaiko kabla sijatulia mc ananiuliza unamchangia mwali wetu shilling ngapi? Mi nikasema elfu nne watu wakashtuka na kuanza kucheka mc akaropoka wewe tajiri wa mchongo unatuangusha.

Nikampa mic yake ikabidi nipitilize hadi geto kwenda kulala maana walikuwa tayari wamekill vibes na hata ile elfu nne niliyosema nikadhira kuitoa sababu ya dharau zao.

Yule Mama shughuli na mc wake niliwamaindi sana sema nilipata fursa ya kutoa hasira zangu kwa mama shughuli.
Mamashughuli ulipita naye?
 
Back
Top Bottom