Abuunuuman
Member
- Sep 11, 2021
- 20
- 29
Wazazi ni watu pekee wanaopitia ugumu wa maisha ya watoto wao wawapo vyuoni wakitafuta elimu
Matarajio ya Kila mzazi ni mafanikio Kwa mtoto wake juu ya kile kilichompeleka chuoni kama egemeo la utafutaji wake hapo Baadae
Bahati mbaya iliyoje ni mtoto huyu ambaye anajulikana kama mwanachuo kutowajibika ipasavyo katika kusoma na Baadae huona ndio nafasi ya yeye kuishi maisha yake
Miaka kadhaa iliyopita katika chuo Cha afya kimoja hapa tanzania macho yangu yalishuhudia mwanadada mwenye asili ya mikoa ya kati ya Tanzania aliyekwenda Jiji la kibiashara la bongo kusomea taaluma Fulani
Dada mweledi na mwenye maadili mazuri ya kitamaduni za huko kwao aliyelelewa vema na wazee wake akiwa ni mwanachuo rasmi katika chuo hicho
Aliamka asubuhi Moja kuyasaka maji ya kupikia na hatimaye kuyakosa ikambidi akaazime maji Kwa wanachuo wenza wa maeneo hayo
Ni bahati mbaya sana Kwa yaliyomsibu Binti huyu
Haikuwa rahisi macho yangu kuvumilia mkasa huu na kamwe Hadi leo sitousahau
Katika kata hiyo yenye adha ya maji na ukame ambapo Kwa kipindi hicho ndoo ndogo ya maji chumvi iliuzwa Kwa shilingi mia mbili huku ya maji tamu ikiuzwa Kwa shilingi mia nne
Haikuwa rahisi Kwa Binti huyu kumudu gharama ya shilingi mia nne ya maji tamu ambapo ilimlazimu kuyapata maji hayo Kwa sharti dogo sana lakini lenye gharama kubwa
Binti huyo aliyapata maji Kwa kustarehesha mwili wake kama sehemu ya malipo huku akisahau gharama kubwa iliyotolewa na wazazi wake Kwa malipo ya ada ya masomo usafiri na gharama za chakula na malazi
Gharama zilizokuwa mara dufu ya ndoo ndogo ya maji iliyopoteza thamani ya utu wake
Kibaya zaidi aliibuka Binti huyo na mahusiano yasiyo rasmi na kuyapupia Mapenzi zaidi kuliko masomo yaliyomtoa nyumbani kwao
Bahati haikuwa kwake wala familia kwani kusoma kuliishia njiani baada ya kutendwa na kijana aliyekuwa naye katika mahusiano hayo na kuishia kuwa ni dada wa mtaani asiyemaliza masomo Hadi leo
Napenda kutoa wito Kwa vijana waliovyuoni hasa wakike kujua umuhimu wa yaliyowapeleka vyuoni huko na kuyaacha yasiyo wahusu kwani mtaka nyingi nasaba hupata miiingi misiba
kijana wewe leo ndio haji manara wa kesho unayetegemewa katika taifa stars ijayo
Maendeleo ya kila taifa katika uchumu na biashara hata elimu yanategemea sana athari za vijana wetu
Daima mbele nguvu moja