SoC03 Jinsi mafunzo ya elimu kwa vitendo yanavyochochea uwajibikaji kwa wahitimu na wasomi kazini hapa nchini

Stories of Change - 2023 Competition

Wichoka Son

New Member
Jun 23, 2023
1
2
JINSI MAFUNZO YA ELIMU KWA VITENDO (FIELD/INTERNS) YANAVYOCHOCHEA UWAJIBIKAJI KWA WAHITIMU NA WASOMI WA ELIMU YA JUU KAZINI HAPA NCHINI.

Nchini Tanzania kutokana na ongezeko la vyuo vikuu kumekuwapo pia na ongezeko kubwa la wahitimu wa elimu ya juu kitu kinachopelekea upungufu mkubwa wa ajira nchini, hivyo kusababisha vijana wengi waliomaliza vyuo kubaki mtaani bila kazi.

Pamoja na changamoto hio ya ajira nchini bado kumekuwa na idadi ndogo ya wahitimu hao wanaopata nafasi ya kuingia kwenye soko la ajira kupitia sekta binafsi na hata serikalini kwa ujumla.

Hata hivyo pamoja na changamoto hio ya idadi ndogo ya wahitimu hao kuingia kwenye soko la ajira,bado kuna lawama nyingi toka kwa waajiri binafsi na hata serikali kuwa bado hata hio idadi ndogo bado hawana ujuzi na uzoefu wa kutosha kuweza kupambana na kuwajibika kwenye kazi kama wahitimu toka nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Hali hiyo hutokana na kiwango kikubwa cha vyuo vingi hapa nchini kutoa elimu ya juu kwa nadharia (theories) zaidi kuliko elimu ya vitendo (practical) na kupelekea wahitimu wengi wa elimu ya juu kupata elimu ambayo inashindwa kuwawezesha kuwa na weledi na ufanisi wa kutosha katika kutimiza majukumu yao ya kazi na hivyo kupelekea kutowajibika kwa kiwango cha juu kutokana na kutokuwa na ujuzi na uzoefu wa kazi kwa kiwango kinachotakiwa kwenye soko la ajira nchini.

Hivyo hivyo, kutokana na tatizo hilo la elimu na mitaala yetu kuegemea zaidi kwenye elimu ya nadharia kuliko vitendo,hali hio imepelekea hata wale wahitimu wachache wanaopata nafasi za kazi katika hizo kampuni,taasisi,idara na wizara kufanya kazi zao kwa mazoea na hivyo kupelekea uwajibikaji wao katika hizo nafasi zao kuwa mdogo na hafifu na kusababisha tatizo la uzalishaji mali kuwa mdogo kwenye hivyo vyombo,taasisi wanazoziongoza na kupelekea kampuni na hizo taasisi kupata hasara na nyingine kushindwa kujiendesha,mfano,mashirika mengi ya Umma yamekuwa yakipitia sana tatizo hilo linalotokana na kuongozwa na watu ambao sio wawajibikaji katika majukumu yao, kutokana na wengi wao kutokuwa na uzoefu na ujuzi unaotokana na kupata mafunzo ya elimu kwa vitendo toka vyuoni kwao.

Katika andiko hili tutaangalia kwa kina jinsi mafunzo ya elimu kwa vitendo yanavyoweza kuchochea wahitimu wengi wa elimu ya juu kuwa na uwezo wa kuwajibika katika majukumu yao na kwenye kazi zao,kwa undani zaidi tutaangalia zaidi katika vipengele vifuavyo, elimu inayotolewa na vyuo vikuu, ,mitaala ya elimu,Uhaba wa nafasi za kufanya mafunzo ya elimu kwa vitendo sehemu mbalimbali,na mapendekezo ya suala hili la umuhimu wa mafunzo ya elimu kwa vitendo kuchochea uwajibikaji.

Elimu inayotolewa na vyuo vikuu nchini, bado hadi leo imejikita kwenye nadhria zaidi kuliko vitendo kitu kinachosababisa wahitimu wengi kumaliza elimu zao wakiwa na uelewa mdogo katika fani zao walizo hitimu,.hivyo kupelekea kuingia kwenye soko la ajira bila kuwa na ujuzi wa fani alizosomea vya kujitosheleza kukidhi majukumu ya kazi wanazofanya hali inayopelekea uwajibikaji wao kwenye kazi hizo kuwa mdogo na hafifu,mfano kwenye fani za ualimu,udaktari,uhandisi na sheria.

Mitaala ya elimu kutotilia mkazo utolewaji wa elimu kwa vitendo, bado mitaala yetu ya elimu imebaki na imeendelea kukumbatia elimu ya nadharia kuliko vitendo kwa muda mrefu bila kubadilishwa kulingana na nyakati tulizonazo kwa sasa na kuangalia mazingira husika,jambo linalopelekea vyuo vikuu vingi kuendelea kutoa elimu ya nadhria zaidi kitu kinachopelekea vijana wengi waliohitimu masomo ya elimu ya juu kuendelea kuteseka kwenye soko la ajira kwa kukosa ajira na pia kukosa ujuzi,ukamilifu na ubobevu wa kazi wa kiushindani na unaoleta uwajibikaji kwenye majukumu na kazi zao.

Uhaba wa sehemu za kufanyia mafunzo kwa vitendo (Field/Intern),kwa miaka ya hivi karibu hapa nchini kumekuwa na ugumu na uhaba mkubwa wa kupata nafasi kwenye sehemu mbalimbali kwajili ya kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na wahitimu wa elimu ya juu katika taasisi, kampuni binafsi, idara, mashirika binafsi na mashirika ya Umma, halimashauri za miji,na majiji na hata serikalini kwa ujumla, jambo linalowakatisha tamaa wahitimu wengi na kusababisha kuendelea kukosa ujuzi, uzoefu na kupunguza hali ya kujitegemea, hali inayopelekea ujuzi wao mdogo kuwa duni kwa kukosa mafunzo halisi ya kazi kwa vitendo,mfano siku hivi kupata nafasi hata ya kujitolea bure kwenye hivyo vyombo au taasisi zilizotajwa hapo juu, ni ngumu sana hali hii inayochangia uwajibikaji kazini kuwa mdogo.


Mapendekezo, kwenye makala au andiko hili ili kuboresha suala la elimu ya juu na kuchochea uwajibikaji kwenye nyaja ya ajira na kazi ninapendekeza yafuatayo.

Kuangiliwa kwa kina mitaala ya elimu hasa kwa kuiboresha na kuibadilisha ili kujikita zaidi kwenye kutolewa zaidi kwa vitendo zaidi (Field/Interns) haswa kwenye elimu ya juu ambayo kwa kiwngo kikubwa ndio inayozalisha wafanyakazi na wafanyabiashara ambao ndio wanatakiwa kuwa wawajibikaji kwenye kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi kwajili ya maendeleo na ustawi wa taifa kwa ujumla.

Pia suala jingine la kutilia maanani ni kwa elimu yetu ya juu kutilia mkazo suala la elimu kwa vitendo kuwa la lazima, ikiwezekana kila fani kuwa na ulazima kila mwaka husika wa masomo wanafunzi kufanya mafunzo kwa mwaka mzima,mfano kama Fani husika ni ya miaka mitatu (3) basi ule mwaka wa mwisho (wa 3) kabla ya kumliza masomo uwe ni kwaajili ya mafunzo kwa vitendo na kama fani ni ya miaka (4 au 5) basi hivyo hivyo mwaka wa mwisho uwe ni maalumu kwajili ya mafunzo kwa vitendo tu, hii itawasaidia sana wahitmu kuwa na elimu,ujuzi na uzoefu bora wa kazi na fani kwa kazi watakazo enda kufanya baada ya kuhitimu na kongeza suala la uwajibikaji kazini,kwenye familia, na taifa nzima kwa ujumla.

Pendendekezo la mwisho, ni kwa serikali kuhakikisha jambo hili la mafunzo ya elimu kwa vitendo ni la lazima vyuoni na pia kupatikana kwa nafasi za kutosha kwenye taasisi zake, mashirika yake ya Umma, na mashirika binfsi ili kuwawezesha wahitimu wengi kupata ujuzi na uzoefu sahihi na halisi wa kazi wanazosomea ili kukuza
na kuchochea uwajibikaji katika kazi.

Kwa ufupi mafunzo ya elimu kwa vitendo ndio umfanya mtu kuwa mwenye elimu bora, ujuzi, ukamilifu, kujua vitendea kazi husika vya kazi, kuwa mbobevu, kuwajibika kazini, kuondoa hofu pia ukuza kujitegemea na uzoefu halisi kwenye kazi anayoifanya, wazungu usema “Practices makes Perfect”, hivyo ili uwajibikaji kuwa ajenda ya msingi ni muhimu elimu yetu haswa elimu ya juu kutolewa kwa vitendo zaidi
 
Back
Top Bottom