Jinsi Kesi ya Yesu ilivyovunja Sheria

Asante sana Mshana.

Nimejifunza sana. Biblia imeeleza juujuu mpaka ujue uchambuzi huu si rahisi.

Na uzee wangu wote huu, nilikuwa najua alihukumiwa kwa mahakama ya kidini tu.
 
Hapa kuna jambo linanitatiza kidogo. Maana yake hapa inaonyesha ya kuwa Mayahudi walikuwa wanaujua ukweli kuhusu Mungu kumzidi Yesu mwenyewe, mpaka ikafikia Yesu kudai yeye ni Mwana na huku si mwana ?

Lakini kwanini Yesu akosee jambo ambalo Mayahudi walikuwa sahihi ?

Inakuwaje Mtume wa Mola akosee katika ujumbe na mafundisho ?

Je ni kweli Yesu aliwahi kusema yeye ni Mwana wa Mungu ?

Ukweli wa hili ukoje...?
ಠ益ಠ
 
Yule aliemkana Yesu hadi jogoo akawika pia hana kosa.

Yaani nione mtu anapigwa mijeledi anagongelewa misumari kwenye mikono na miguu anavalishwa miba kwenye miti na ananing'inizwa juu ya mti kama nyama buchani na askari halafu askari haohao wananifuata wananiuliza

" unamjua huyu mtu ?"

Ndugu msomaji embu tuacheni unafiki pembeni we ungejibuje?

Mbona alimkana hatakabla hawajafika huko kwenye kuhongeleama misumari
 
Herode (Antipas) alikuwa Mtawala wake wa Kimila. Huyu ndiye aliyemkata Kichwa Yohane Mbatizaji (John the Baptist) kwasababu ya Ahadi aliyoitoa kwa Binti wa Herodia.
Kuna Herode aliyetaka kumuua Yesu akiwa kichanga, je ni huyu?
Je kipindi hiki Yohana alikuwa ameshakatwa kichwa?
Je Yesu hakusikia na kumsaidia nduguye asiuawe kikatili?
 
Back
Top Bottom