Jinsi Kesi ya Yesu ilivyovunja Sheria

Hapa kuna jambo linanitatiza kidogo. Maana yake hapa inaonyesha ya kuwa Mayahudi walikuwa wanaujua ukweli kuhusu Mungu kumzidi Yesu mwenyewe, mpaka ikafikia Yesu kudai yeye ni Mwana na huku si mwana ?

Lakini kwanini Yesu akosee jambo ambalo Mayahudi walikuwa sahihi ?

Inakuwaje Mtume wa Mola akosee katika ujumbe na mafundisho ?

Je ni kweli Yesu aliwahi kusema yeye ni Mwana wa Mungu ?

Ukweli wa hili ukoje...?

Jibu utakalopewa hapa ni huna ROHO MTAKATIFU huwezi kuelewa haya mambo bila ROHO MTAKATIFU utakuja niambia
 
Ni kweli kabisa,halafu pia,mhanga alijua nini Yuda angefanya na hakuchukua hatua yoyote ili asidhurike.Na hapo kuna maneno kwamba Yuda alisaliti ili neno la Mungu litimie,sasa Yuda yeye alikuwa na nguvu gani ya kuzuia neno la Mungu lisitimie? Labda tuje na principle Actus reus non facit reum nisi mens sit rea
.Yuda ana hatia ama hana.

Hapo sasa wanamuonea
 
Kuna kipindi fulani,Kuna jamaa aliiibua hii kesi ya yesu,na kulishitaji dola la kirumi,jamaa alikuwa anadai fidia dhidi ya uonezi uliofanyika,Sasa sijajua rufaa ya huyu jamaa ilifikia wapi!!.
Wakristo tunatakiwa tuishtaki na kuidai fidia serikali ya Italia kwa makosa yafuatayo.

La kwanza jaji mrumi mwitaliano mwenzao Jaji waliyemuweka Ponsio Pilato aliacha kutumia vitabu vya sheria kumhukumu Yesu akawauliza waliohudhuria mahakamani kuwa nimfanye nini huyu Yesu wakasema asulubiwe akakubali asulubiwe .Toka lini jaji akauliza wahudhuriaji mahakamani kuwa atie hukumu gani? Waitaliano mtuñipe fidia

la pili jeshi la kirumi lilimchapa vibao Yesu alipokuwa mahakamani akijibizana na jaji.Askari akasema unamjibu hivi jaji akamlamba vibao.Kazi ya askari ndani ya mahakama si kupiga vibao mtuhumiwa

Tatu Walipo.sulubisha askari wa kirumi waligawana mali zake yaani mavazi yake bila mirathi kutangazwa .Wao hawakuwa na haki ya kujigawia mirathi kienyeji

Kwa maelezo haya naomba kuwakliisha nikidai fidia kwa kuuawa Bwana wetu kwenye mahakama ya kimataifa

Naomba wabasheria wabobezi wanisaidie kuburuza selikali ya Italia mahakama ya kimataifa kwa kutuulia Bwana wetu Yesu Kristo
 
Yes mkuu ni kweli kabisa..waislamu wanaamini Yesu ni nanii km wengine Tu,Ila Kwa wakristo wameenda mbali zaidi na kumwita MUNGU

Hilo la kuamini alipaa au hakupaa sina uhakika labda tumuulize jurjan atuelimishe zaidi

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Tumuulize Jurjan yeye kama nani!
Yeye ana Imani yake na siye tuna Imani yetu.
Huoni kuwa kitendo cha huyu Jurjan kukubali kuwa Yesu Kristo alifufuka ni kitendo cha kukana Imani yake na kukubali Ukristo? KAMWE hawezi kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom