Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Nili quote ka sehemu ako peke kurahisisha suala langu kwako, kwakuwa msingi mzima wa section na sub one yake inajenga preamble ya hicho nilichocopy na closure yake ni msisitizo wa hoja ya mamlaka ya rais.

Ndio maana nauliza tena je? Kuzuia mikutano ya siasa ni mambo yanayohusiana na vita?
 
Mkuu soma vzr nilichokiandika usikurupuke!
Nimesema pamoja na katiba kutoa haki kadhaa ikiwemo kuandamana, lkn pia imetoa limitations, and one of the limitations ni readons of public interest.
Kwamba there are tymes when those rights can be taken away for reasons of public interest, na nikasema bahati mbaya katiba na sheria zingine hazija define what amounts into public interest hivyo kitu hiki kinatoa room kwa watu Ku limit hizo haki ikiwemo haki ya kuandamana kwa muamvuri wa public interest, na ni katiba imetoa loophole hiyo.
Kwahiyo kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara inapata baraka chini ya kifungu hicho cha 30(1) mkuu.
It is for public interest, what are they?! No body knows bcoz katiba haisemi wala hakuna sheria inayosema!
 
Hebu ona sasa umekuja mzima mzima. Kwikwi. Rudi sasa kwenye mada tukadili.
Kwanza haki zako unazijua? Je mbele ya rais wewe una haki gani kikatiba?
 
Rais akiwa kama amiri jeshi mkuu anaweza kutumia vyombo vya ulinzi kulinda nje au ndani si kutokana na vita pekee bali akiona usalama wa raia unaathiliwa au yeye akiona inavyofaa.

Soma tena using'ang'anie kwenye vita wakati katiba imempa uhuru wa kutumia majeshi anavyoona inafaa.
 
Mjadala huu ni mzuri sana kama utakua umeuvua uchama au wewe unavyojiona na ulivyo katika nafasi yako.
Kuna watu humu mnatamba kua mko vizuri kwenye sheria na mnapiga hela sasa najiuliza wewe ni mwanasheria au jizi tu!
Wengi mnajikita kwenye haki za binadamu katika kujadiri issue iliyo hot leo lkn sheria ya vyama vingi mnaikacha... Tuongelee katiba na sheria ya vyama vingi... UKUTA sio issue ya HR no..
 
Unajua tatizo ni cause of limitations to enjoyment of rights, kwakuwa hakuna clear interpretation of what is/are public interest (s) basi kuwepo na liberty ya kila upande ku enjoy hii b. o. d na kwamba kusiwepo upande wenye kutumia msuli kukandamiza upande mwingine.

Kwa mfano, kwa nini serikali isipeleke hoja hii mahakamani ili ipate ufafanuzi wa kisheria na badala yake inaandaa majeshi kuua waandamanaji?

Au kwanini usiitishwe mdaharo wa kitaifa kujadiri what are the public interests of which the president can intervene in case they are endangered?
 
Hapa ndugu tunaongelea katiba iliyozaa sheria.
Vyama vya siasa na haki zake zipo chini ya haki za jumla kikatiba. Sheria ya vyama vya siasa ni kitabu kingine kabisa ambacho mzazi wake ni katiba.

Hata kama sheria ya vyama vya siasa imetaja kufanya mikutano kwa mujibu wa katiba ibara ya 30(1) mamlaka inaweza kuondoa haki hiyo kwa maslahi ya umma.

Kwahiyo kudai haki ya kufanya mikutano wakati mamlaka imekataa kwa maslahi ya umma ni kuvunja katiba.
 
Ndio maana nasema kuwepo mdaharo/makongamano kama ya kigoda cha mwalimu ili watu tukutane ana kwa ana kwenye jambo la katiba hii hii maana kuna misconceptions za wasomaji wengi wa katiba japo ni kosa la mitaala ya elimu zetu kushindwa kuweka somo la katiba kama elimu ya msingi kwa raia.
 
Msisahau kuwa kila wakati inasema bila kukiuka katiba ama katika hali ya emergency siyo wakati wowote. Hatuna vita sasa hivi. Na pia huwezi kuweka sheria kwa ajili ya opposition ukiacha chama tawala. Hakuna sheria ya namna hiyo.
Nadhani tujadili kwa kufikiria je itakuwaje kiatu kikienda katika upande mwingine? Je bado utatetea? Kama jibu ni hapana basi acha kutetea.
 
Soma katiba wewe hakuna sehemu katiba imesema kama hakuna haki uandamane.
Umeshasoma Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo inaakisi Katiba unayoi quote hapa? Hizi ni Taaluma za Watu, not every Harry Tom n Dick can read, understand, and give the correct construction of Laws! Ulichofanya hapa ni kubwabwaja tu!
 
Hapa hatuongelei vita rafiki. Hapa tunaongelea jinsi haki yako inavyonyima haki wengine.
Kama haki yako inanyima haki wengine kwahiyo mamlaka itaangalia public interest na haki yako itaondolewa ili public ipate haki.
 
Umeshasoma Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo inaakisi Katiba unayoi quote hapa? Hizi ni Taaluma za Watu, not every Harry Tom n Dick can read, understand, and give the correct construction of Laws! Ulichofanya hapa ni kubwabwaja tu!
Mbona unakurupuka tu kama umetoka shimoni!!!. Tulia uelewe watu tunajadili nini hapa.
 
Katika ibara zote hizo ulizo taja ambazo ni limitstion of human rights ni kipengele kipi kimetaja chama cha siasa au maandamano au mikutano ya vyama vya siasa? Kitu gani kinaweza kuweka uhalali wa katazo la mikutano ya siasa kutoka na party three? Je kukataza mikutano ya siasa ni sababu tosha yakuwepo amani nchini? Unaweza ukatupa ushahidi mikutano mingapi, lini na wapi hapa Tanzania iliyosababisha vita na kukosekana kwa amani?
 
Unaifahamu Hali ya Hatari? Utaishia ku quote provisions irrelevant to the situation! Pole, Law is not for every Hary Tom n Dick!
 
Nimekusoma vizuri mkuu ndio maana in contents ume emphasize nilichojibu.
Tuko pamoja hapa kiongozi.
 
Derogation/limitation of human rights.. How is it connected to the rights and freedom of political parties in Tanzania ? Allein
 
Kwa mujibu wa taarifa toka vyombo vya usalama kuna taarifa ya hatari kutokana na mikusanyiko ya kisiasa.
Pili Mambo hayo ya mikusanyiko ya kisiasa yewahi kuathiliwa huko Arusha kutokana na mlipuko wa mabomu.
Matamko ya viongozi wa siasa yanahamasisha uvunjifu wa amani.
Vilevile kulingana na kikao cha juzi cha CUF kimeonesha namna ya vurugu zilivyotokea kwenye vikao vya ndani

Kwa mujibu wa taarifa hizo mamlaka inavizuia vyama vya siasa kutokufanya mikutano ya ndani na nje mpaka mamlaka itakapo toa muongozo. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ibara ya 30(1) mamlaka inaweza kuondoa haki kwa maslahi ya umma.
 
Umemisread hicho kifungu mkuu, ebu ukiwa unasoma weka kituo ili upate comprehensive meaning ya kinachokusudiwa katika maelezo hayo.

Mimi sina ugomvi na mtu hapa nina ugomvi na misinterpretation ya hivi vifungu vya katiba, pale ambapo vinaonekana kukinzana vyenyewe kwa vyenyewe ndipo mkanganyiko wa msomaji unapotokea.

Napendekeza mdaharo wa wazi wa katiba hii iliyopo kabla hata ya hiyo pendekezwa au ya warioba.
 
Derogation/limitation of human rights.. How is it connected to the rights and freedom of political parties in Tanzania ? Allein
Hebu niambie ibara ipi kwenye katiba inaongelea haki ya vyama vya siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…