Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

Mimi waliniunganisha na huduma ambayo hata sijaiomba (tigo hao) , dah walikuwa wananikata, nilikaa we nikajaribu kuwauliza wenzangu, nao wakawa wanalalamika kama mimi, nikaona isiwe tabu, nikawapigia simu wakaniambia eti Kuna huduma nilijiunga ya kusikiliza hadithi, nikawaambia mm sijawahi kujiunga na huduma yyt Ile, nilibishana nao, baadaye wakaniambia jinsi ya kujitoa, hii ilikuwa kama miezi miwili iliyopita. Sasa wiki iliyopita nilinunua vocha ya elfu mbili, nikajiunga na kifurushi cha buku jero, mia tano ikabaki,naamka asubuhi nijiunge na kifurushi cha jero, inashindikana kumbe wamekata mia tatu, nikaona haina haja nikachomoa line yao nikaweka kabatini, nikaweka line ya mtandao mwengine. Tigo badilikeni ndio wenye tabia za kihuni, ningeitumia TTCL ila tatizo vocha zao tabu ila karibia mitandao yote ni wahuni wamekaa kiwiziwizi, wanaziendekeza njaa za kipumbav. u.
 
Kampuni zote za simu wana michezo hii ila Vodacom ndio kinara wao, tatizo kubwa ni kwamba wakuu wetu na ofisi zao wanategemea sana kampuni hizi pindi chaguzi zinapofika hivyo sidhani kama wana uwezo wa kukomesha uhuni huo kama Kagame alivyofanya
 
Duuuh...kumbe bado wapo watu hupenda vya bure...! Dezo gharama...!
Hapa haviongelewi vya bure tu ndg yangu,kinaongelewa kitu kinacho gusa nyanja zote ktk sekta ya mawasiliano. Mfano ninao hata mimi. Wiki jana nilikuwa na bando kwenye akaunti yangu na pia nikawa na kiasi cha 7,000/= kama salio kwenye akaunti kuu. Niliperuzi kama dk.3-4 hivi kisha nikatumiwa sms kuwa nimetumia sh.100 kutoka ktk kiwango cha 50,000/= cha matumizi ya internet. Kuona ujumbe huo nikajua kuna uwezekano bando limefyekwa hivyo nikakimbilia kuangalia salio kama hiyo 100 imekatwa kwenye 7,000/= ili ninunue bandle lingine. Nilicho kikuta ni salio kusomeka 0. Nikalazimika kutafuta salio jingine. Kama una salio taarifa ya bando haitolewi pindi bando liishapo mpaka na salio la akaunti kuu likiisha ndiyo unataarifiwa kuisha kwa bando. Jana mida ya mchana wakati nasafu bandle likaisha hapo sijaacha salio lolote ndiyo wananitumia ujumbe tena eti umetumia kiasi cha 7,000/= kutoka ktk kiwango chako cha 50,000/= cha matumizi yako ya internet kana kwamba ndiyo niliyo kuwa naitumia kumbe kiasi hiki nilisha kwapuliwa siku nyingi zilizo pita. Ushahidi huu hapa kwenye kiambata. Sasa kwa mfano hapo kuna cha bure kipi kilicho niponza mimi?
1479156098200.png
 
Hapo kwenye Facebook bure, maelezo yako yanapishana na uzoefu wa miaka 10 kwasababu Facebook wenyewe wanaoption ya huduma Bure lakini huku tunaambiwa ni hisani ya makampuni ya Simu
 
Nimefanya kazi kwenye kampuni mbali mbali za simu hapa nchini kwa muda wa zaidi ya miaka 10, kabla ya kuamua kujiajiri mwenyewe. Katika muda wote huo nimeshuhudia kampuni hizi zikiwaibia wateja kwa namna mbalimbali.

Nimekaa na huu ushahidi kwa muda sasa lakini naona roho inanisukuma niuanike hadharani mbele za watanzania ili wafunguke macho na kufahamu UFISADI huu unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini. Nitaanika wizi wote kadri nitakavyoweza kuukumbuka hapa:

Huduma za bure.

Kuna hizi huduma ambazo wanaziita huduma za "BURE" kana kwamba zinapatikana bure wakati si kweli! Kwa mfano, wateja hutumiwa SMS zinazowadanganya kwamba wanaweza kupata huduma za bure na ili wazipate wanaelekezwa kutuma ujumbe kwenda kwenye namba fulani.

Na mteja akisharogwa akatuma ujumbe kwenda kwenye namba husika, imekula kwake! Nyingi ya huduma hizi zinazoitwa za bure hugharimu fedha na mara ujiungapo hujikuta unakatwa salio lako kimya kimya.

Ni mara nyingi mtakuwa mmewahi kusikia mtu akilalamika kwamba salio lake limepungua&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.unaweka airtime ya Tsh 1000 leo bila kuitumia, ikifika kesho unakuta zimebaki sh 350! Tsh 650 zimeenda wapi? Zimekatwa kwenye zile huduma za "BURE" ulizotangaziwa.

Promosheni feki.

Promosheni nyingi zinazoanzishwa na makampuni ya simu zinalenga kuwanyonya na kuwakandamzia wateja. Mfano halisi ni pale wateja wanapotangaziwa kwamba huduma ya FESIBUKU inapatika bure! Thubutuuu! Hakuna kitu cha bure nchi hii, ndugu yangu.

Huu ni wizi wa mchana! Kupona kwako ni pale utakapotumia hiyo huduma ukiwa hauna salio kwa kuwa huwezi kupata access ya huduma husika (kama vile fesibuku, twita, nk).

Ikiwa utafungua huduma hiyo ukiwa na salio, salio lako lote litakombwa sawia! Kuna mtandao mmoja wa simu unajinadi kwamba unatoa huduma ya fesibuku bure wakati ni uongo mtupu. Ingia kwenye hiyo fesibuku uone utakavyoliwa fedha! Aidha kuna mtandao mmoja uliwahi kuwa na fesibuku ya bure siku za nyuma (kama mtakumbuka).

Kwa muda fulani huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa. Kumbe ilikuwa ni janja ya nyani&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];..baadaye ile "bure" ilifutwa kimya kimya, wateja wakaendelea kukamuliwa kama kawaida na mpaka leo hawajawahi kuwataarifu wateja wao kwamba hiyo "bure" imesitishwa! Kuna wateja wengi sana, hasa wa kule vijijini, ambao wanaendelea kukamuliwa kwa kujidanganya kwamba huduma ni ya bure hadi leo, kumbe ilishasitishwa kitambo sana!

Ulaghai wa Kimangungo.

Kuna wakati ambapo makampuni ya simu hupandisha tariffs kimya kimya bila kuwataarifu wateja wake na kuendelea kuwaibia bila kujua.

Mwaka 2006 gharama za kupiga simu, kutuma sms na kutumia data zilipandishwa kinyemela na wateja wakaendelea kukamuliwa fedha kimya kimya hadi pale baadhi yao waliposhtukia dili na kuja juu. Aidha, prosheni fulani zinapoanzishwa, kama vile punguzo la gharama za kupiga simu nyakati za usiku, pindi zinafikia tamati wateja hawapewi taarifa na kujikuta wakitumia fedha zaidi ya matarajio yao.

Promosheni inapoisha kampuni hizi huwakataza wafanyakazi wake wasiwaambie wateja ili waendelee kukamuliwa fedha kilaghai. Huu ni wizi, tena wa mchana na hauna tofauti na ufisadi wowote ule.

Kutotoa taarifa kwa wateja kwa makusudi.

Wateja wanapojiunga kwenye vifurushi mbalimabli huletewa taarifa immediately via SMS kwamba wamefanikiwa kujiunga lakini kifurushi kikiisha ama wateja huchelewa kutumiwa meseji ya taarifa au hawatumiwi kabisa. Hili tatizo huwakumba zaidi wale wateja wanaopenda kubaki na salio kubwa kwenye simu zao.

Kwa mfano, mtu unanunua vocha ya Tsh 2000 kisha unanunua kifurushi cha Tsh 500 na kubakiwa na Tsh 1500 kwenye simu. Pindi kifurushi cha 500 kikiisha hutatumiwa ujumbe wowote hadi utapokuwa umekausha 1500 zilizosalia kwenye simu.

Huu pia ni wizi wa mchana na unaofanywa kwa makusudi na kampuni za simu hapa nchini. Ninao ushahidi usiokuwa na mashaka katika huu wizi wa makusudi.

Njia nyingine inayotumika kuiba hapa ni kutotoa call details pindi upigapo simu. Ukimaliza kupiga simu ukiangalia call details unakuta inasoma 00:00:00! Details hizi zinafichwa kwa makusudi ili kujenga mazingira ya wizi.

Kwa mfano mtu unaongea kwa dakika 3, wao wanakata dakika 4.30 na kukuibia dakika 1.30! Matokeo yake unakuta muda wa hewani uliopewa wakati wa kujiunga umeibiwa na kampuni kwa maslahi yake binafsi. Lakini pia kuna wizi mwingine huu hapa: &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];

unaponunua kifurushi hupewa dakika ambazo ungetegemea zitozwe kwa sekunde (per second billing) lakini badala yake hutozwa kwa dakika (per minute billing) kinyume cha mkataba kwa lengo la kumkamua mteja kiujanja. Huu ni wizi na haukubaliki hata kidogo.

Kuvuruga mawasiliano kwa makusudi.

Kuna wakati wahandisi wa kampuni husika hupewa jukumu la kuvuruga mawasiliano ya wateja ili watumie muda mwingi na pesa nyingi kwenye maongezi. Inakuwaje hapa? Inakuwa hivi: Ukimpigia mtu yeye anakuwa anakusikia lakini wewe humsikii au vice versa.

Hii husababisha kutumia muda mwingi kuelewana wakati huo salio likinyonywa kama kawaida &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hata kama mkichukua muda mwingi kuelewana salio hutafunwa sawia! Njia nyingine inayotumika hapa ni kuvuruga access to customer care ili unapokuwa umepatwa na tatizo usiweze kuwafikia watu wa huduma kwa wateja kupata msaada.

Hii ndio sababu 90% ya wateja wenye matatizo genuine hawaipati namba 100. Mtu unaweza kupiga siku nzima na usiunganishwe kuongea na mshauri. Hatimaye wengi wao hukata tamaa na kuamua kukubali "kuliwa"!

Hii ni sehemu ya ushahidi ambao nimeukusanya while working with different mobile companies in Tanzania. Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Nawasilisha.
Pamoja na yote mazuri uliyoyaandika na kufafanua vizuri na kuyafahamu kwa miaka kumi halafu eti unayatoa Leo basi na wewe kama ilikuwa inakuuma ungeacha kazi Mara moja 10 yrs back na kutoa taarifa hii kwa Mamlaka husika.

Lakini kwa kutuambia Leo baada ya kufanya kazi miaka 10 basi ulikuwa miongoni mwao ktk huo wizi.

Na hapo ndiyo napesema kujua uzalendo wa watz ni ngumu sana,Leo tunamuona huyu mtoa mada wa maana sana wakati ametuibia kwa miaka 10.

Wewe bwana ni miongoni mwa mliowaibia watz ktk mitandao ya simu unatakiwa ukiri hayo kwani ulikuwa unapokea mshahara wa kampuni inayowaibia ndugu zako na wewe ukaendelea tu sasa aidha umeshiba pesa au umepunguzwa kazi ndiyo unatoa taarifa kwa umma kuhusu wizi sijakupenda.
 
makampuni ya simu ni sumu kwa wanyonge....hushirikiana na TCRA kuwaibia wanyonge mshabara bila chenga.
 
Swala LA kifurushi cha bure lilioanzoshwa na kampuni moja jana tu limenikamua vi mb vyangu nikajua si mzigo wa bure fb basi nikafungua mipicha ya wadau kuja kucheck kile kimnara cha bure kimetokea nikajua nimeshaumia,so ukweli ni kuwa wanakula data zako zote zikiisha ndio wanakuunga bure fb pekee,ila jambo lililonikera zaidi ni pale nilipotumia reminder msg ya kuwa mb zako za bure zimebaki 8 ilihali nimezima data Muda huo nikaona haya mbona maluweluwe baada ya masaa manne ikaja msg salio lako LA kifurushi cha bure limekwisha

Ajabu wanakulaje data wakati data bundle iko off?
 
Nimefanya kazi kwenye kampuni mbali mbali za simu hapa nchini kwa muda wa zaidi ya miaka 10, kabla ya kuamua kujiajiri mwenyewe. Katika muda wote huo nimeshuhudia kampuni hizi zikiwaibia wateja kwa namna mbalimbali.

Nimekaa na huu ushahidi kwa muda sasa lakini naona roho inanisukuma niuanike hadharani mbele za watanzania ili wafunguke macho na kufahamu UFISADI huu unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini. Nitaanika wizi wote kadri nitakavyoweza kuukumbuka hapa:

Huduma za bure.

Kuna hizi huduma ambazo wanaziita huduma za "BURE" kana kwamba zinapatikana bure wakati si kweli! Kwa mfano, wateja hutumiwa SMS zinazowadanganya kwamba wanaweza kupata huduma za bure na ili wazipate wanaelekezwa kutuma ujumbe kwenda kwenye namba fulani.

Na mteja akisharogwa akatuma ujumbe kwenda kwenye namba husika, imekula kwake! Nyingi ya huduma hizi zinazoitwa za bure hugharimu fedha na mara ujiungapo hujikuta unakatwa salio lako kimya kimya.

Ni mara nyingi mtakuwa mmewahi kusikia mtu akilalamika kwamba salio lake limepungua&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.unaweka airtime ya Tsh 1000 leo bila kuitumia, ikifika kesho unakuta zimebaki sh 350! Tsh 650 zimeenda wapi? Zimekatwa kwenye zile huduma za "BURE" ulizotangaziwa.

Promosheni feki.

Promosheni nyingi zinazoanzishwa na makampuni ya simu zinalenga kuwanyonya na kuwakandamzia wateja. Mfano halisi ni pale wateja wanapotangaziwa kwamba huduma ya FESIBUKU inapatika bure! Thubutuuu! Hakuna kitu cha bure nchi hii, ndugu yangu.

Huu ni wizi wa mchana! Kupona kwako ni pale utakapotumia hiyo huduma ukiwa hauna salio kwa kuwa huwezi kupata access ya huduma husika (kama vile fesibuku, twita, nk).

Ikiwa utafungua huduma hiyo ukiwa na salio, salio lako lote litakombwa sawia! Kuna mtandao mmoja wa simu unajinadi kwamba unatoa huduma ya fesibuku bure wakati ni uongo mtupu. Ingia kwenye hiyo fesibuku uone utakavyoliwa fedha! Aidha kuna mtandao mmoja uliwahi kuwa na fesibuku ya bure siku za nyuma (kama mtakumbuka).

Kwa muda fulani huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa. Kumbe ilikuwa ni janja ya nyani&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];..baadaye ile "bure" ilifutwa kimya kimya, wateja wakaendelea kukamuliwa kama kawaida na mpaka leo hawajawahi kuwataarifu wateja wao kwamba hiyo "bure" imesitishwa! Kuna wateja wengi sana, hasa wa kule vijijini, ambao wanaendelea kukamuliwa kwa kujidanganya kwamba huduma ni ya bure hadi leo, kumbe ilishasitishwa kitambo sana!

Ulaghai wa Kimangungo.

Kuna wakati ambapo makampuni ya simu hupandisha tariffs kimya kimya bila kuwataarifu wateja wake na kuendelea kuwaibia bila kujua.

Mwaka 2006 gharama za kupiga simu, kutuma sms na kutumia data zilipandishwa kinyemela na wateja wakaendelea kukamuliwa fedha kimya kimya hadi pale baadhi yao waliposhtukia dili na kuja juu. Aidha, prosheni fulani zinapoanzishwa, kama vile punguzo la gharama za kupiga simu nyakati za usiku, pindi zinafikia tamati wateja hawapewi taarifa na kujikuta wakitumia fedha zaidi ya matarajio yao.

Promosheni inapoisha kampuni hizi huwakataza wafanyakazi wake wasiwaambie wateja ili waendelee kukamuliwa fedha kilaghai. Huu ni wizi, tena wa mchana na hauna tofauti na ufisadi wowote ule.

Kutotoa taarifa kwa wateja kwa makusudi.

Wateja wanapojiunga kwenye vifurushi mbalimabli huletewa taarifa immediately via SMS kwamba wamefanikiwa kujiunga lakini kifurushi kikiisha ama wateja huchelewa kutumiwa meseji ya taarifa au hawatumiwi kabisa. Hili tatizo huwakumba zaidi wale wateja wanaopenda kubaki na salio kubwa kwenye simu zao.

Kwa mfano, mtu unanunua vocha ya Tsh 2000 kisha unanunua kifurushi cha Tsh 500 na kubakiwa na Tsh 1500 kwenye simu. Pindi kifurushi cha 500 kikiisha hutatumiwa ujumbe wowote hadi utapokuwa umekausha 1500 zilizosalia kwenye simu.

Huu pia ni wizi wa mchana na unaofanywa kwa makusudi na kampuni za simu hapa nchini. Ninao ushahidi usiokuwa na mashaka katika huu wizi wa makusudi.

Njia nyingine inayotumika kuiba hapa ni kutotoa call details pindi upigapo simu. Ukimaliza kupiga simu ukiangalia call details unakuta inasoma 00:00:00! Details hizi zinafichwa kwa makusudi ili kujenga mazingira ya wizi.

Kwa mfano mtu unaongea kwa dakika 3, wao wanakata dakika 4.30 na kukuibia dakika 1.30! Matokeo yake unakuta muda wa hewani uliopewa wakati wa kujiunga umeibiwa na kampuni kwa maslahi yake binafsi. Lakini pia kuna wizi mwingine huu hapa: &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];

unaponunua kifurushi hupewa dakika ambazo ungetegemea zitozwe kwa sekunde (per second billing) lakini badala yake hutozwa kwa dakika (per minute billing) kinyume cha mkataba kwa lengo la kumkamua mteja kiujanja. Huu ni wizi na haukubaliki hata kidogo.

Kuvuruga mawasiliano kwa makusudi.

Kuna wakati wahandisi wa kampuni husika hupewa jukumu la kuvuruga mawasiliano ya wateja ili watumie muda mwingi na pesa nyingi kwenye maongezi. Inakuwaje hapa? Inakuwa hivi: Ukimpigia mtu yeye anakuwa anakusikia lakini wewe humsikii au vice versa.

Hii husababisha kutumia muda mwingi kuelewana wakati huo salio likinyonywa kama kawaida &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hata kama mkichukua muda mwingi kuelewana salio hutafunwa sawia! Njia nyingine inayotumika hapa ni kuvuruga access to customer care ili unapokuwa umepatwa na tatizo usiweze kuwafikia watu wa huduma kwa wateja kupata msaada.

Hii ndio sababu 90% ya wateja wenye matatizo genuine hawaipati namba 100. Mtu unaweza kupiga siku nzima na usiunganishwe kuongea na mshauri. Hatimaye wengi wao hukata tamaa na kuamua kukubali "kuliwa"!

Hii ni sehemu ya ushahidi ambao nimeukusanya while working with different mobile companies in Tanzania. Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Nawasilisha.
Unayosema ni kweli kabisa na mimi yamenikuta Vodacom ila niliwakoromea haswa eti unanunua kifurushi leo kesho au muda huohuo unatumiwa ujumbe kifurushi kimeisha
 
Inakuaje kampuni ya simu inakwambia, inaomba imei ya simu yako pamoja na number yako?
ilikuwaje hadi ukaombwa hivyo vitu mkuu? ulipotelewa simu? fafanua.
 
Hapa haviongelewi vya bure tu ndg yangu,kinaongelewa kitu kinacho gusa nyanja zote ktk sekta ya mawasiliano. Mfano ninao hata mimi. Wiki jana nilikuwa na bando kwenye akaunti yangu na pia nikawa na kiasi cha 7,000/= kama salio kwenye akaunti kuu. Niliperuzi kama dk.3-4 hivi kisha nikatumiwa sms kuwa nimetumia sh.100 kutoka ktk kiwango cha 50,000/= cha matumizi ya internet. Kuona ujumbe huo nikajua kuna uwezekano bando limefyekwa hivyo nikakimbilia kuangalia salio kama hiyo 100 imekatwa kwenye 7,000/= ili ninunue bandle lingine. Nilicho kikuta ni salio kusomeka 0. Nikalazimika kutafuta salio jingine. Kama una salio taarifa ya bando haitolewi pindi bando liishapo mpaka na salio la akaunti kuu likiisha ndiyo unataarifiwa kuisha kwa bando. Jana mida ya mchana wakati nasafu bandle likaisha hapo sijaacha salio lolote ndiyo wananitumia ujumbe tena eti umetumia kiasi cha 7,000/= kutoka ktk kiwango chako cha 50,000/= cha matumizi yako ya internet kana kwamba ndiyo niliyo kuwa naitumia kumbe kiasi hiki nilisha kwapuliwa siku nyingi zilizo pita. Ushahidi huu hapa kwenye kiambata. Sasa kwa mfano hapo kuna cha bure kipi kilicho niponza mimi?View attachment 434327
Kaz nikwakooooo......hawawez kukutumia sms yakumalizika mbs kweny bundle lako wakat unasalio lakawaida wanachofanya nikukuacha utiririke uwape faida
 
Huu wiz had kwa ndugu zetu HALOTEL, ukiacha salio kila siku lapungua. Sometimes ukituma sms unarudishiwa sms kuwa umetumia dakika kadhaa, mtandao wa internet kwa baadh ya sehem unakata Hadi week na wala hawaoneshi kujali
 
Kuna wizi mwingine huu,unanunua vocha ya mia tano lakini ukijiunga kifurushi unaambiwa umejiunga kifurushi cha sh 499.Hii shilingi moja inaenda wapi?Piga hesabu sh 1×wateja milioni 4 mwezi ×mwaka.
 
Tigo hayo mambo wanaweza sana. Sasa hivi tunakaribia mwezi eti mitambo yao inasumbua.

Unafungua youtube,inaload tu bila kuona chochote. Ila mwisho wa siku Mb zinaenda.

Msg unatuma sasa hivi,inafika baada ya nusu saa.

Jamaa ananipigia simu anaambiwa simu yangu inatumika,wakati mimi simu ipo charge.

Shame on you tigo Tanzania.
 
Back
Top Bottom