Mimi sina hamu na vodacom , nakumbuka juzi kati kipindi wananidai 1450 ya nipige tafu nikabofya *149*42# ili nijiunge na bando la mb 500 kwa sh 500 kwa wiki nikaweka pesa m pesa kila nikitaka kununua naambiwa mchakato umezuiliwa ile napiga huduma kwa wateja muhudumu wa voda ananiambia heti huwezi kununua bando hili kwa m pesa (kumbuka hapo wananidai ) nikaona isiwe tabu nikanunua jumla vocha ya 2000 ile naweka tu majamaa yakakata 1450 hapo hapo nikabakiwa na 550 haya nikajaribu tena kujiunga naambiwa huduma hii haipatikani kwa sasa jaribu tena baadae, nikapiga huduma kwa wateja kakapokea kamdada flan nikakauliza mbona kila nikijaribu kujinga na bando la net la wiki kwa 500 sifanikiwi naambiwa huduma hii haipatikani kwa sasa ,
Kakanijibu "SASA WEWE UMEAMBIWA HUDUMA HII HAIPATIKANI KWA SASA UNATAKA NIKWAMBIE NINI ZAIDI?"
Kumbuka hapo nimeshaingia mkenge nimelipa deni lao lote la nipige tafu , nikaona isiwe inshu nikakata simu,
BALAA likaja nilipoingia katika kuperuzi tovuti za bure kwenye
www.internet.org mzee nikafungua facebook ya bila malipo kama dakika 1 nikatoka nikaenda goal dot com kuangalia matokeo kama sekunde 50 hivi ile nakuja kuangalia salio nakuta limebaki 508 majamaa yameshakula sh 42 wakati yananadi tovuti yoyote inayopatikana kwenye internet.org ni ya bure kumbe ukiwa na salio yanang'amua salio kimya kimya ,
Nikaona huu ni upuuzi huu nikanunua tu bando la siku la internet napo nashangaa napewa mb 70 kwa tsh 500 wakati halotel mb 120 ni 499 aisee kwa kifupi VODACOM TANZANIA ni mafisadi sugu .