Jinsi gani nitamueleza baba mkwe wangu ili niepukane na karaha za kelele zake za kupiga Mswaki?

Kama hupendezwi mwambie tatizo linalokusibu.

Siwezi nikaishi katika nyumba yangu kwa woga.

Mwambie mzee asipige makelele pindi anaposafisha meno. Hupendi.

Kama haelewi aondoke, kama atataka kuondoka na mwanaye waache waende.

Kuliko kuja kulalamika huku, ni bora umfukuze. Nyumba ni yako, miliki ni yako
Ushauri mbaya usio na busara wala hekima.
 
Walipokuja nikawakaribisha vzr sana, kama wakwe zangu,,hakuna shida yeyote kuwa pamoja nao. Siku ya kwanza kulala ndy tatizo limeanza kujitokeza. Baba mkwe anapiga mswaki mara tatu kwa siku,,na mbaya zaidi akipiga mswaki inakuwa ni kelele nyumba nzima, anapiga sana kelele, sijuwi mswaki wa aina gani anatumia.

Ni kelele kama anatapika,mara kama anakabwa,,,mara kupenga kamasi,,mara kukohoa hadi kubanja,,,mradi ni karaha tupu..hadi nyumba za jirani zinasikika. Akiamka yeye saa 11 alfajiri kwenda msikitini ni lazima apige mswaki, na nyumba nzima lazima iamke, ni kelele tupu, mradi kila mtu atatambuwa ni yeye yumo chooni.

Kumkaribisha vizuri mkwe ni wajibu wako kwakuwa nawe ulikaribishwa vema ulipokwenda kuoa
Je wewe hujawahi kwenda kwao ukasababisha karaha na wao wakakuvumilia?
 
Upigaji Mswaki wa kizamani huo, yaani hapo Ni mpaka atapike na kutoa machozi ndiyo anahisi Raha.

Nahisi atakuwa hanywi Pombe, Kwa hiyo anakuwa na nyongo nyingiiiii, Mchukue umpe K vant au konyagi hiyo Nyongo yote itaisha ataacha hit tabia ya kiswahili.
 
Au siku huyo mzeebaba akianza kufanya yake chooni wewe jifanye kama umeshtuka nenda kamgongee muulize vipi mzee kuna tatizo!!.. hapo siatasema hana..muache atoke, akitoka chooni mwambie "nilishtuka nilidhani umekabwa huko chooni au una matatizo ya koo mzee wangu maana kuna daktari wa masuala ya koo namfahamu anaweza kukusaidia" akisema hana basi mwambie anavyo jikamua koo sana huko chooni sio vizuri kiafya itasamsababishia madhara ya koo. Akisema ana tatizo la koo basi mpeleke hospital yoyote apewe dawa basii imeisha hiyoooo!!!
Watu mna maneno:D:D...... haya mto mada ushauri huo uchukue
 
Wakuu habari zenu,

Natumai mpo powa na mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya maisha. Wakuu nina week sasa nimepokea ugeni toka mkoani,,ambao ni baba na mama wa mke wangu, ambao ni wakwe zangu. Mimi ndoa yangu ina kama miaka 4 hivi, lakini siku zote hizo sikuwahi kubahatika kuishi nao japo siku mbili wakwe zangu hao pamoja nyumbani kwangu.

Hivi juzi kuna Shemeji yangu alijifunguwa kwa operation ikabidi baba na mama yake wakaja mjini kumjulia hali, lakini kutokana na ufinyu wa sehemu ya kufikia ikabidi waongee na mke wangu kuhusu kukaa kwangu kwa muda, sababu nyumba yetu ni kubwa.

Walipokuja nikawakaribisha vzr sana, kama wakwe zangu,,hakuna shida yeyote kuwa pamoja nao. Siku ya kwanza kulala ndy tatizo limeanza kujitokeza. Baba mkwe anapiga mswaki mara tatu kwa siku,,na mbaya zaidi akipiga mswaki inakuwa ni kelele nyumba nzima, anapiga sana kelele, sijuwi mswaki wa aina gani anatumia.

Ni kelele kama anatapika,mara kama anakabwa,,,mara kupenga kamasi,,mara kukohoa hadi kubanja,,,mradi ni karaha tupu..hadi nyumba za jirani zinasikika. Akiamka yeye saa 11 alfajiri kwenda msikitini ni lazima apige mswaki, na nyumba nzima lazima iamke, ni kelele tupu, mradi kila mtu atatambuwa ni yeye yumo chooni.

Mchana na usiku baada ya kula ni lazima apige Mswaki tena, kelele na karaha zipo pale pale. Na tatizo sio baba mkwe kupiga Mswaki wakuu, bali tatizo ni kelele za kutapika au kama kukabwa koo au kupenga kamasi na kubanja, mwanzo nilidhani ana tatizo, nilipoongea na mke wangu ndiyo akanambiya hivyo ndivyo alivyo, hebu fikiria nyumba ya choo ndani halafu kunakuwa na karaha za kelele za kutapika au kukabwa koo, hivi wakuu kunalika hata embe humo ndani?

Wakuu hali ni tete sana,,nataka nipate mbinu ya kumueleza huyu mkwe, kwa anachokifanya sicho, tatizo nitaanzaje? Maana hawa wazee wanaweza wakaniachanisha na mke bado nampenda. Naweza nikamuingia hovyo ikawa nongwa.

Mke wangu yupo kimya sana, japokuwa na yeye ni muhanga wa kuamshwa kwa kelele za mswaki asubuhi na jioni.

Msaada wakuu, mbinu za kumvaa mkwe niepukane na kelele za mswaki asubuhi na jioni.

Namsikitikia sana huyo mzee baba mkwe wako kamtupa binte yake kwa kafiri.

We mwabie tu hizi kelele zako za kujitayarisha kwenda msikini zinanikosesha amani nyumbani kwangu ATAKUELEWA
 
Back
Top Bottom