Jinsi Bikra Maria alivyompa mtihani kiongozi wa Kanisa, Nabii Zakaria..

Sio kweli! Maria alikuwa mke halali wa Mzee Joseph. Kugundulika kwa mimba changa ya Yesu hakukuzuia mahusiano ya kindoa baina ya Maria na Joseph. ..Jiongeze!
Yote yanawezekana! Though inaelezwa kuwa Joseph alimsaidia Maria kutoroka ili watu wa mji wasimuue. Alihisiwa kuzini.

Hii story sijui niiendeleze? Inaonekana kuna school of thoughts mchanganyiko..
 
Hili swali nimeshalijibu mara mbili hapo juu. Soma vizuri Injili ya Luka na Isaiah kidogo.. Pita pita kwenye maandiko yahusuyo nyakari na vizazi kisha unganisha dots..

Mimi nimechukua muda kukusanya na kuweka pamoja tu, sio mawazo yangu binafsi.
Ungekuwa unaweka reference kutoka hizo sehem ulizokuwa unaunganisha hio historia ingetusaidia sana sisi tusio soma biblia Mara kwa mara
 
Pale watu wanapotaka kulazimisha kubalance mambo baada kuona upande wao haujakaa vizuri.
 
Mkuu hiyo stori naweza kuiendeleza lakini haitokuwa na jipya kivile.. Ni yale yale ya Malaika Gabriel kuleta ujumbe kuhusu Maria kupata mtoto kwa uwezo wa roho mtakatifu n.k.

Badala yake, nafikiria kuleta simulizi yenye topiki tofauti though bado najiuliza nilete simulizi ipi.. Zipo nyingi lakini ambayo niko nayo tayari ni ile ya Maria Magdalena na maisha yake ya ukahaba kabla hajakutana na Yesu na kutubu..

Zipo nyingi sana mkuu..
asante kwa historia hii, ila ingependeza zaidi ukija na rejea za hizi historia chief.
 
Yote yanawezekana! Though inaelezwa kuwa Joseph alimsaidia Maria kutoroka ili watu wa mji wasimuue. Alihisiwa kuzini.

Hii story sijui niiendeleze? Inaonekana kuna school of thoughts mchanganyiko..
mkuu umejitahid kuandika sana ila sioni mantiki sana ya hichi unachojaribu kutetea...........

historia ya maria baada ya kumzaa Kristo haijaandikwa popote kwenye biblia, na sidhan km kuna mahali imeandikwa as hakuna interest yoyote ndani yake

mhimu tumwamini huyu Kristo, maria nae alikua mtu, nae aliokolewa kwa msalaba huo huo tunaookolewa sisi..........

NB
nimenusa harufu ya kuhalalisha ibada ya Maria!
 
Hii sio historia ya Maria baada ya kumzaa Yesu. Ni kabla.

Suala la Imani naliacha kama lilivyo. Sijagusia huko kabisa.

NB: Sio lengo kuhalalisha ibada yoyote.
 
Wadau wa fikra,
Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.
So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini kwenye jukwaa hili makini.
Kupitia historia fupi ya Maria, nitaeleza mtihani wa Bikra Maria kwa Mkuu wa Kanisa/Hekalu alimolelewa, ambaye alikuwa ni Nabii Zakaria. Ni matarajio yangu tutaulizana maswali na kurekebishana kwa uungwana ili sote tuweze kuelimika na kufahamishana mambo mengi tusiyoyajua.
Hebu tuipitie historia hiyo kidogo..
Wazazi wake
Maria alizaliwa na Mzee Joachim na Bi. Anna ambao walikuwa ni wachamungu haswa. Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachamungu wa enzi hizo, Mungu aliwapa mtihani wa ugumba Mr. & Mrs Joachim kiasi cha kudharaulika katika jamii kabla ya kuwainua kwa kuwapatia msichana mtakatifu Maria, baada ya kuzidisha kwao ibada na maombI.
Malezi yake
Watakatifu zamani walikuwa wakiweka nia kwa watoto wao watakaowazaa. Familia hii ya mzee Joachim na mkewe waliweka nadhiri kwamba endapo Mungu atawajaalia mtoto, basi watamtoa wakfu - yaani atatumika kwenye kazi za Mungu (utumishi). Hivyo, baada ya uzao wa Maria na kufikisha umri wa miaka 2/3 baada ya kuacha ziwa, walitekeleza ahadi yao kwa kumpeleka hekaluni kulelewa na Kiongozi wa hekalu ambaye alikuwa ni mzee Zakaria, mume wa Elizabeth (mama yake Yohana Mbatizaji).
Hekaluni palikuwa pakilelewa mabinti bikra kwa kuwa walizingatiwa kuwa wasafi na watakatifu zaidi. Kwahiyo binti Maria aliishi humo pamoja na mabinti bikra wengine na kufundishwa maadili mema pamoja na sheria za Mungu. Wazazi wake walikuwa wakimtembelea mara kwa mara mpaka alipofikia umri wa miaka 10 wakafariki dunia.
Ndoa
Alipofikisha umri wa miaka 13, yaani miaka mitatu baada ya wazazi wake kufariki, uongozi wa Kanisa uliamua Maria atoke hekaluni ili aweze kupata mume. Kwa mila na desturi za hekalu enzi hizo, binti akishavunja ungo anakuwa sio msafi tena hivyo hahitajiki kubaki hekaluni kwa sababu atalichafua. Hata hivyo, Maria alijenga hoja kwamba yeye wazazi wake waliamua kumtoa wakfu hivyo ameamua ataitunza bikra yake na kumtumikia Mungu maisha yake yote.
Jambo hili lilileta mtihani kidogo kwa mzee Zakaria kwa sababu ni unprecedented. Akalazimika kuitisha baraza la ushauri namna ya kudeal nalo ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa aende altareni akiwa pekee aombe hekima ya Mungu. Usiku wake, alifanya hivyo na Malaika akamtokea na kumpa Muongozo kwamba aitishe mkutano wa wagane wachamungu ambapo mmojawapo atateuliwa na Mungu kwa ishara kwa kuwa bado Mungu ana kusudi maalum na Maria.
Basi, ndipo katika kusanyiko la wanaume hao wagane, alikuwemo mzee wa miaka takribani 80 aitwaye Joseph. Fundi seremala mchamungu haswa, ambaye mkewe Salome alifariki mwaka mmoja uliopita na alijaaliwa naye watoto 7.
Kufupisha story, mzee huyo alifanikiwa kuteuliwa kwa ishara ya mng'ao wa kitambaa. Naye binti Maria (13) hakuwa na pingamizi kwenye uamuzi wa Muumba. Akakubali kuolewa.
Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!
 
Ila yaonekana kuwa tuyajuwayo ni kidogo mno. Mambo mengi yalifichwa kwa sababu maalum.
 
mkuu umejitahid kuandika sana ila sioni mantiki sana ya hichi unachojaribu kutetea...........

historia ya maria baada ya kumzaa Kristo haijaandikwa popote kwenye biblia, na sidhan km kuna mahali imeandikwa as hakuna interest yoyote ndani yake

mhimu tumwamini huyu Kristo, maria nae alikua mtu, nae aliokolewa kwa msalaba huo huo tunaookolewa sisi..........

NB
nimenusa harufu ya kuhalalisha ibada ya Maria!
Sio vyote vimeandikwa bibliani maana isingetosha ila maandiko mengine yapo na hayawekwa kama biblia unayoijua
 
Nina maswali mengi ila ngoja niulize haya.
1. Mara baada ya Yesu Issah bin Mariam kuanza kuhubiri, ni sehemu ngapi au mara ngapi tukasikia habari za Yosefu???
2. Kama kweli Yosefu alikuwa na miaka hiyo je ilikuwaje mpaka akamchukua mchumba aliye sealed???
Nipo.....
 
Interest hebu nieleweshe, baada ya Mama Bikira Maria kumzaa Yesu, alijaliwa tena kuzaa watoto wengine? If yes, ni akina nani hao
 
Heshima yako mkuu Katavi.

Nitajitahidi kufanya kazi ya ziada kukusanya vifungu kadhaa vinavyosapoti hayo niliyoyaeleza. Ningependa uainishe ni eneo lipi zaidi ungependa nikupatie vielelezo vyake.

Naamini hii ni kiu ya wengi pia so nitajitahidi kutafuta wasaa wa kuviweka pamoja hapa..

Asante.

Mi nadhani umetoa mwanga fulani ambao nimejaribu kuupima kwenye Torati naona sioni mgonangano wa torati na haya maelezo yakol. kwa hiyo kwa kuwa hayana direct conflict na Torati nadhani nimejifunza kitu fulani hasa hao ndugu zake Yesu nilijiuliza sana walipatikana vipi lakini sasa naona picha kabisa.

Hata bikra Maria kama alikuwa chini ya nadhiri ya wazazi wake na kwa kuwa torati ilimkataa matokeo yake alibaki anaelea mpaka mpango wa Mungu ukamkuta hapo. Kwa maana kwa jinsi ya torati mwanamke hana cha kufanya hasa madhabahuni. atakuwa mwombaji na waombaje walikuwa ni wajane yeye hajawa hata mjane na torati haijawalinda mabikra na kuolewa na pia kuolewa kumeachwa kuwa uamuzi wa muoaji na wazazi, yeye hakuwa na say yoyote pale ispokuwa hiyo ya nadhiri ya wazazi

Pia ukija kwa ndugu zake Yesu, Kwanza unaweza kuona walikuwa wakubwa kuliko yeye kwa maana isingewezekana wao wawe wadogo yeye aisende Jerusalemu kwenye pasaka halafu wao wadogo wende kula pasaka Jerusalemu. kwa namna moja au nyingine yeye alikuwa mdogo kuliko ndugu zake. na kama alikuwa mdogo kuliko ndugu zake? Bikra maria angewezaje kuwa bikra?

Jambo lingine wale ngudu zake walikuwa kampani moja na Petro kwa maana walikuwa wavuvi, na kwa jinsi inavyoonekana Petro alikuwa mkubwa kiumri kuliko Yesu alikuwa mtu mzima sana maaana walikuwa na miji wale wakati wanachaguliwa walishakuwa wavuvi senior wenye familia zao. Kama hivyo ndivyo na ndugu zake Yesu kama walikuwa kampani ya Petro ni dhahiri hata Yakobo na ndugu zake Yesu wengine walikuwa wakubwa kuliko Yesu vinginenvyo na Yeye Yesu angekuwa mvuvi kwanza kitu ambacho hakukifanya.

Biblia inasema isingewezekana kuandika kila kitu katika maandiko
 
Hakika. Hakika. Hakika!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom