Jinsi Bikra Maria alivyompa mtihani kiongozi wa Kanisa, Nabii Zakaria..

Maria hakufa mkuu,, alipalizwa Binguni...!

Sent using Jamii Forums mobile app

Kupalizwa kwa Maria ni Dogma ya Wakatoliki ila kuna maandiko na simulizi zinazosema kuwa alifariki pia tena kwa kufatwa na mwanaye na kupewa chaguo (kumbuka Maria hakuwa na dhambi ile yetu ya asili so hakuwa na ulazima wa kufa) akamjibu kuwa “Bwana, nataka kupitia kila ulichopitia” hivyo mwili na roho yake vikatengenishwa.

Kuna ushahidi wa sanda aliyozikiwa pia uko kwenye museum huko walipokuwepo. Ngoja nikutafutie hizo simulizi
 
Hapa si kweli. Yohana ambaye baba yake ni Zakaria na mama yake ni Elizabeth ndiye aliyekuja kumbatiza Yesu, yaani ni Yohana Mbatizaji, naye huyu aliuawa na Herode na kichwa chake kikatolewa kama zawadi kwa binti wa Herode siku ya birthday yake (Mathayo 14:1-12 na Marko 6:14-30). Kumbuka kuwa hata Yohana Mbatizaji alikuwa na wanafunzi wake (Luka 7:18-28) na hakuna popote katika Biblia ambako Yesu alimchukua Yohana Mbatizaji kama mwanafunzi wake.
Yohana aliyeandika Injili ya Yohana, zile nyaraka 3 na Ufunuo SIYO yule Yohana Mbatizaji mwana wa Zakaria na Elizabeth, kwani wakati hayo yanaandikwa Yohana Mbatizaji alishauawa na Herode. Yohana mwinjili na mwandishi wa nyaraka 3 na kitabu cha Ufunuo ni mwana wa Zebedayo (Luka 5:10). Yohana huyu alikuwa na nduguye aitwaye Yakobo. Vijana hawa wawili mama yao aliwaleta kwa Yesu akamwomba wakae mmoja kulia na mwingine kushoto kwa Yesu katika ufalme wake (Mathayo 20:20-28), na hawa walikuwa miongoni mwa mitume 12 wa Yesu kama walivyoorodheshwa katika Marko 3:13-18.
Tumsifu Yesu Kristo.
Madini haya jamani
 
Sipendi kuharibu hii mada nzuri ya muhusika pia najua lengo ni kuwa na uelewa mkubwa wa mambo kwa ujumla ikiwa pamoja na imani zetu

Lkn kwa sie ambao hatuamini hizi Hadith za Wayahudi na jamaa zao wa mashariki ya kati tunapita kimya hapa kwa huzuni kuu ya kwamba mtu mweusi itachukua muda sana kujisimamia

Kuna Mwanamalunde,Mkwawa , kinjekitile,Shaka , Nzinga mbandi, na kadhalika wanatakiwa kupewa heshima kubwa kuliko mtu mweupe mmoja eti ndo ‘muokozi’ wetu dah haya
Sisi weusi tunazidiwa na weupe kwa idadi.Nadhani tuko moja ya saba hivi.

Utropicana umetufanya tukawa na akili zubaifu,jiografia imetukinga sana na majanga kwa hivo Bongo ya mtu mweusi haitumiki ipasavyo.Halafu pia upatikanaji wa mahitaji ni abundantly, akili inazubaa!
Ila wakati umeshawasili na tutapanda upesi sn kwenye daraja la juu.

Kuhusu Mada ya Bikira Maria,its amazing....coming soon!
 
Umeandika kitu kikubwa sana hizo sentensi za mwanzo mkuu
 
Kupalizwa kwa Maria ni Dogma ya Wakatoliki ila kuna maandiko na simulizi zinazosema kuwa alifariki pia tena kwa kufatwa na mwanaye na kupewa chaguo (kumbuka Maria hakuwa na dhambi ile yetu ya asili so hakuwa na ulazima wa kufa) akamjibu kuwa “Bwana, nataka kupitia kila ulichopitia” hivyo mwili na roho yake vikatengenishwa.

Kuna ushahidi wa sanda aliyozikiwa pia uko kwenye museum huko walipokuwepo. Ngoja nikutafutie hizo simulizi
Zurie kama Zurie
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom