Jinsi Bikra Maria alivyompa mtihani kiongozi wa Kanisa, Nabii Zakaria..

Ni kweli Joseph was much older than Mary lkn si kwa tofauti hiyo ya miaka. Na Joseph hakuwahi oa wala kuwa na watoto. Soma au sikiliza audio ya kitabu cha "life of virgin Mary".
How much older mkuu? Hebu tafiti ilikuwa ni tofauti ipi exactly kabla hujahitimisha kwa kunipinga. Nasisitiza, kama mtu ananipinga aweke ukweli.
 
How much older mkuu? Hebu tafiti ilikuwa ni tofauti ipi exactly kabla hujahitimisha kwa kunipinga. Nasisitiza, kama mtu ananipinga aweke ukweli.
we umefanya utafiti upi au ndio kusoma ijnili ya luka na isaya kidogo bila kujua vifungu ulivyosoma
 
biblia nayo!!! baba ake joseph alikuwa nani kati ya hawa?

And Jesus himself began to be about thirty years of age, being the son of Joseph, which was the son of Heli, - Luke 3:23
And Jacob begat Joseph the husband of Mary, of whom was born Jesus, who is called Christ. - Matthew 1:16
 
Hiyo Heli ndo nini?
 
Wadau wa fikra,

Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.

So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini kwenye jukwaa hili makini.

Kupitia historia fupi ya Maria, nitaeleza mtihani wa Bikra Maria kwa Mkuu wa Kanisa/Hekalu alimolelewa, ambaye alikuwa ni Nabii Zakaria. Ni matarajio yangu tutaulizana maswali na kurekebishana kwa uungwana ili sote tuweze kuelimika na kufahamishana mambo mengi tusiyoyajua.

Hebu tuipitie historia hiyo kidogo..

Wazazi wake
Maria alizaliwa na Mzee Joachim na Bi. Anna ambao walikuwa ni wachamungu haswa. Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachamungu wa enzi hizo, Mungu aliwapa mtihani wa ugumba Mr. & Mrs Joachim kiasi cha kudharaulika katika jamii kabla ya kuwainua kwa kuwapatia msichana mtakatifu Maria, baada ya kuzidisha kwao ibada na maombI.

Malezi yake
Watakatifu zamani walikuwa wakiweka nia kwa watoto wao watakaowazaa. Familia hii ya mzee Joachim na mkewe waliweka nadhiri kwamba endapo Mungu atawajaalia mtoto, basi watamtoa wakfu - yaani atatumika kwenye kazi za Mungu (utumishi). Hivyo, baada ya uzao wa Maria na kufikisha umri wa miaka 2/3 baada ya kuacha ziwa, walitekeleza ahadi yao kwa kumpeleka hekaluni kulelewa na Kiongozi wa hekalu ambaye alikuwa ni mzee Zakaria, mume wa Elizabeth (mama yake Yohana Mbatizaji).

Hekaluni palikuwa pakilelewa mabinti bikra kwa kuwa walizingatiwa kuwa wasafi na watakatifu zaidi. Kwahiyo binti Maria aliishi humo pamoja na mabinti bikra wengine na kufundishwa maadili mema pamoja na sheria za Mungu. Wazazi wake walikuwa wakimtembelea mara kwa mara mpaka alipofikia umri wa miaka 10 wakafariki dunia.

Ndoa
Alipofikisha umri wa miaka 13, yaani miaka mitatu baada ya wazazi wake kufariki, uongozi wa Kanisa uliamua Maria atoke hekaluni ili aweze kupata mume. Kwa mila na desturi za hekalu enzi hizo, binti akishavunja ungo anakuwa sio msafi tena hivyo hahitajiki kubaki hekaluni kwa sababu atalichafua. Hata hivyo, Maria alijenga hoja kwamba yeye wazazi wake waliamua kumtoa wakfu hivyo ameamua ataitunza bikra yake na kumtumikia Mungu maisha yake yote.

Jambo hili lilileta mtihani kidogo kwa mzee Zakaria kwa sababu ni unprecedented. Akalazimika kuitisha baraza la ushauri namna ya kudeal nalo ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa aende altareni akiwa pekee aombe hekima ya Mungu. Usiku wake, alifanya hivyo na Malaika akamtokea na kumpa Muongozo kwamba aitishe mkutano wa wajane wachamungu ambapo mmojawapo atateuliwa na Mungu kwa ishara kwa kuwa bado Mungu ana kusudi maalum na Maria.

Basi, ndipo katika kusanyiko la wanaume hao wajane, alikuwemo mzee wa miaka takribani 80 aitwaye Joseph. Fundi seremala mchamungu haswa, ambaye mkewe Salome alifariki mwaka mmoja uliopita na alijaaliwa naye watoto 7.

Kufupisha story, mzee huyo alifanikiwa kuteuliwa kwa ishara ya mng'ao wa kitambaa. Naye binti Maria (13) hakuwa na pingamizi kwenye uamuzi wa Muumba. Akakubali kuolewa.

Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!
Point of correction:

Salome alikuwa si mke wa Yusuph. Salome alikuwa binti wa Yusuph kwa mke wake marehemu. Salome huyu aliolewa na Zebedayo ambapo alimzalia watoto wakiwemo mitume wawili wa Yesu Kristo ambao ni Yohana na Yakobo. Salome alikuwa kaka yake Yesu kupitia kwa Yusuph baba yake. Mtume Yohana na Yakobo walikuwa na undugu na Yesu Kristo, ambapo Yesu alikuwa mjomba wao.

Kuna mengine umeandika vzr sana. Nilitaka tu kurekebisha hapo huenda umeandika kwa kuchanganya, lakini hapo ulipofika katika uandishi ninaamini kuwa unakijua unachokiandika.
 
Mkuu nani kasema Maria ni Mungu?Unapo qoute post yangu nakuniuliza kwa hiyo Maria ni Mungu unamanisha maelezo yangu yamesema hivyo.Kama unataka kujua kitu jifunze jinsi ya kuuliza mkuu.
yeye anamzungumzia bikira maria wewe ukamwambia anapoandika mambo ya mungu.! awe makini nikakuuliza kwasababu mada inamuhusu maria je maria ni mungu.
 
Point of correction:

Salome alikuwa si mke wa Yusuph. Salome alikuwa binti wa Yusuph kwa mke wake marehemu. Salome huyu aliolewa na Zebedayo ambapo alimzalia watoto wakiwemo mitume wawili wa Yesu Kristo ambao ni Yohana na Yakobo. Salome alikuwa kaka yake Yesu kupitia kwa Yusuph baba yake. Mtume Yohana na Yakobo walikuwa na undugu na Yesu Kristo, ambapo Yesu alikuwa mjomba wao.

Kuna mengine umeandika vzr sana. Nilitaka tu kurekebisha hapo huenda umeandika kwa kuchanganya, lakini hapo ulipofika katika uandishi ninaamini kuwa unakijua unachokiandika.

Asante kwa nia njema ya kutaka kuweka rekodi sawa. Napenda mwendo huu.

Hata hivyo, Joseph mkewe alikuwa akiitwa Salome na mmoja kati ya mabinti zake watatu naye alikuwa akiitwa Salome pia. Mengineyo uliyoeleza nakubaliana nayo isipokuwa hapo kwa Yohana.

Kama unamaanisha Mtume Yohanna Mbatizaji, wazazi wake walikuwa ni Zakariya na Elizabeth. Hawa walimpata uzeeni baada ya Mzee Zakaria kushuhudia neema ya Mungu kupitia kwa Maria aliyekuwa akimlea ambapo naye akafanya sala ya kuomba apatiwe moto na Mungu kukubali ombi lake.

Na hapo ndipo inaonesha umri wa Maria kuozwa ulikuwa mdogo sana kiasi kwamba Maria anaenda kuolewa huku nyuma mlezi wake Mzee Zakaria naye anapata mtoto wa uzeeni. So mimba ya Yesu na Yohana hazikupishana sana. Ndio maana wote walikuwa vijana na walishiriki mission pamoja.

Story ya Zakaria nayo inasisimua. Alifanyiwa ishara ya ububu kumjulisha kuwa mkewe amenasa ujauzito. Anyway, hii sio mada kuu.

Ila kama ulimaanisha Yohana tofauti, basi sawa.

Shukrani kiongozi.
 
Nilimaanisha Yohana aliyekuwa miongoni mwa mitume wa Yesu Kristo. Aliyeandika kitabu chenye jina lake YOHANA, UFUNUO, WARAKA WA 1,2 & 3 WA YOHANA.
 
Duuh! wapi kaandika Maria ni Mungu au unatafuta mada?
Utalihusishaje jambo LA maria na mambo ya Mungu au huoni.Anamwambia mtoa mada awe makini anapozungumzia mambo ya Mungu na kwasababu hapa tunamzungumzia maria nikauliza Maria ni Mungu.
 
Hiyo umeitoa kwenye injili ya Bikira maria.
Ila sijaelewa ni yapi madhumuni ya uzi wako!
 
kwahiyo wakati Yesu anaanza kazi ya kutangaza ufalme wa Mungu akiwa na umri wa miaka 30 Yosefu alikuwa ameshagonga miaka 100?
Kwahesabu za jamaa ndio hivyo, na kibaya zaidi mama yake alikuwa 14 wakati akimzaa
 
Similar Discussions

24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom