Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Wanangu wa Arsenal tuko pamoja, ushindi lazima leo,
IMG_3122.jpg
 
Simulizi ni nzuri Sana na inavutia kwakweli kuisoma na kuifuatilia..lkn jambo Moja tu linanishangaza ni matumizi ya pesa ya INSIDER MAN yalivyomakubwa mpaka najiuliza, icho kilikuwa ni kipindi Cha Jk au Mjomba Magu..maana 50,000 unamtowa mlinzi wa geti tu...mmmmh...
Kweli pesa matumizi...
afu usafiri wako na mkeo ni ndege tu, wakati umetoka familia ya kawaida Sana, uwo ujasiri unaupata wapi kwa hizi aina za familia zetu ..
Kazi ya uhakika ni Uber....No Bado sijapata connection...endelea kutupa story bro labda uko mbele ntakusoma.
Lkn hongera Sana kwa kuteka minds zetu kupitia story Yako.

Mkuu wewe unaona 50k ni hela kubwa sana? Hio nikienda samaki samaki napata heineken 7 pesa imeisha
 
Umesahau alimpa Masai wa wavuvi laki 2 mammae kwa maisha gani

Broh laki 2 kwaajili ya mtoto unaona ni kubwa? Maana kwa Junior nikiingia shopping inanitoka si chini ya laki 3, bila shaka huna mtoto.

Pampas kwa mtoto mchanga kwa mwezi si chini ya 60k

Mama watoto kula kwa mwezi bajeti andaa 100k

Ungekua na mtoto usinge comment shit kama hii,
 
EPISODE 62
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

PREVIOUS
Baada ya kufika kwake alishuka kwa haraka sana na alikwenda ndani kwa upande wangu sikuwa na choice wala sikujua nifanye nini, maana hata mimi nilikuwa nimevurugwa hivyo niliamua kuondoka.

CONTINUE
Muda huu ilibidi niende tu kwa Manuel mapema maana nilimkaribisha home kwaajili ya dinna, lakini wakati niko njiani niliwaza kwa hili tukio la leo kuna uwezekano mkubwa sana wa Iryn kumwambia mama J na mambo yakaja kuwa mabaya zaidi. Kwa upande mwingine niliona haitakuwa na nguvu sana kama atasema sababu ya ushahidi, niliwaza pale lakini hili jambo si la kupuuza inabidi nichukue hatua mapema.

Baada ya kuwasili pale Ramada niliwasiliana na Manuel na alinambia niende room yake hakuna shida na nilimkuta anachezea laptop yake. Tulianza kupiga story pale na Manuel na kubwa aliuliza kama nina mahusiano na Iryn maana alisema kwa jinsi alivyomuona jana anaonekana kunipenda sana.

Nilimwambia Manuel ukweli kuwa hatuna mahusiano yoyote na nina muheshimu kama Bossy wangu, na yeye ndo ambaye aliniokoa kipindi biashara ya Uber imekuwa ngumu, Manuel aliishia kumsifia Iryn kuwa ni mwanamke mzuri.

Manuel alikwenda kujiandaa na tulikwenda home kwaajili ya kupata dinna ya pamoja, baada ya kuwasili nyumbani kama kawaida Junior alikuwa kwenye gari yake ambayo amenunuliwa na Iryn na Manuel akamyanyua.

Kwa upande mwingine wife alikuwa ameandaa dina nzuri sana pale mezani kwa haya masuala wife kwakweli hajawai niangusha maana jikoni yuko vizuri sana. Baada ya kupata dinna tuliendelea kupiga story pale seblen na muda huu wife alikuwa anapanga nguo zake kwaajili ya safari ya kwenda Moshi.

Wife alimuaga Manuel kuwa anaondoka kwenda Moshi kwaajili ya kutoa pole ya msiba na mimi nilimwambia kama atakuwa free tumpe kampani wife afu tukitoka Airport tutapititia Cocobeach tukatembee, Manuel hakuwa na shida na alifurahi sana.

Wakati tukiendelea na story pale simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Lucy ilibidi nitoke nje nikaipokee maana nilijua lazima kuna jambo anataka kunambia muda huu.

MIMI: “Hey Lucy mambo!”

LUCY: “Salama Insider, mshikaji wangu umezingua sana Bossy amenichana kila kitu, kumbe yule dada (Prisca) ana mimba yako?”

MIMI: “Lucy ni long story nafikiri tutaongea kesho rafiki yangu, siko sehemu salama.”

LUCY: “Insider just know that Iryn amesema hataki tena kuiona sura yako na kazi anakuachisha this time, nafikiri utabiri wangu unakwenda kutimia”

MIMI: “Daah mbona Iryn anataka kutumia hisia kuliko akili?”.

LUCY: “Insider umemuumiza sana Iryn hata kama hampo kwenye mahusiano kwa jinsi mnavyoishi akikuona na mwanamke mwingine anaumia isitoshe anakupenda ndo sisi wanawake tulivyo. Hata ningekuwa mimi ningeumia kwa haya mambo unayo fanya, una kumbuka sakata la Sumaiya? Asmah? na leo kajua umemjaza mtu mimba, atleast ungekuwa unafanya hata kwa siri. Insider una muumiza sana Iryn kumbuka ni yatima anahitaji ukaribu wako hata kama hamdate lakini kuwa makini, mambo yote uliyokuwa unafanya alikuwa anakusamehe. Unakumbuka wewe ulivyomuona na kaka yake ile siku ni kiasi gani uliumia? sasa yeye anaprove kabisa unafikiri nini?”Lucy aliongea kwa uchungu sana hata mimi nilianza kuona nina hatia,

Ipo hivi kuna matukio yalitokea ambayo sikutakaga andika ili kufanya mambo yasiwe mengi. Kuna kipindi Rebecca mfanyakazi wa kule Masaki alishaniotea nina mla mate Sumaiya, kwa upande wake aliumia sana hivyo alimwambia Iryn maana Rebeca na Sumaiya walikuwa hawapatani kabisa. Lile sakata Iryn alimind sana yakaisha, kuna sakata lingine kuna dada mfanyakazi anaitwa Asmah (Code) ana asili ya uchotara huyu ni kama receptionist, anapokeaga wageni, kupokea na kujibu simu za wateja nk. Huyu dada nilipitaga naye, sasa ilijulikanaga lakini haikuwa na ushahidi na Iryn baada ya kupata hizi taarifa alimind sana lakini yaliisha. Kwa upande wangu nilikuwa nazingua sana, Iryn alikuwa halali yake kunichukia hata hivyo alinivumilia sana. (Nilikuja kujua baadae Rebecca ndo alikuwa spy wa Iryn hata simu alipewa kwa masharti ya kumpa umbea Iryn, unaweza kurefer Episode No. 56 maongezi yetu kati ya mimi, Iryn & Lucy niliandika kwa code)

Turudi kwenye story sasa,

MIMI: “Lucy kweli nimezingua naona kwasasa siwezi toboa tena na wasiwasi anaweza kumwambia hata mama J.”

LUCY: “Rafiki yangu nimekutetea sana lakini this time Iryn amesema hawezi kuendelea kuwa karibu na mtu anayemuumiza hisia zake, maana anasema unashindwa kumuheshimu.”

MIMI: “Lucy unanishauri nini sasa rafiki yangu maana mwenyewe hapa hata sijui nafanyaje.”

LUCY: “Mpigie simu omba muongee labda atarudisha moyo kwako.”

MIMI: “Sawa rafiki yangu haina shida nashukuru kesho nitakutafuta ofisini.”

LUCY: “Na uje mapema tupange mipango kuna vitu nataka nikwambie face to face.”

Baada ya kumaliza maongezi na Lucy nilishusha pumzi nzito sana muda huu na niliwaza pale nimetoka kuchukua mkopo kwa Mama wa2 juzi tu nitaulipaje kama sina mchongo wa kueleweka?.

Na muda huu nilipata wazo nimpigie simu Iryn ili nijaribu kumuweka sawa kuhusu hili jambo na ikiwezekana tuonane. Lakini baada ya kupiga simu alikuwa kani block kote mpaka Whatsapp na aliblock namba zangu zote, na hapa nikasema leo nimeyanyaga na muda huu nilipata wazo la kwenda kuangalia simu ya wife kama Iryn alipiga maana nilikuwa na wasiwasi sana.

Baada ya kurudi ndani wife kama kawaida alikuwa anapiga story na Manuel na nilifanya kumuazima simu yake na akanipa. Nilicheki call history nikakuta hakuna shida nikaenda mpaka whatsapp nikakuta mara ya mwisho wamechati jumapili, hapa nikawa na amani.

Manuel aliaga muda huu na nikampeleka hotelini na wakati narudi nilipata wazo solution ya haya yote inabidi nifanye kila mbinu nimle Iryn na hapa ningekuwa nimemfunga kusema kwa mama J na hasira zake zingeisha.

********
Asubuhi niliamka mapema na kwa upande mwingine Prisca alinipigia simu hii asubuhi na kubwa alikuwa anataka tuonane kwaajili ya mazungumzo na mimi nilimwambia tutaonana Ijumaa.

Nilikwenda mchukua Manuel pale Ramada na tulirudi home kumpitia mama J ili tuanze safari ya kwenda JNIA na alikuwa anategemea kuondoka na ndege ya saa 7 mchana.

Baada ya kuwasili pale JNIA tuliambiwa muda wa kuondoka umehairishwa na umepelekwa mbele hivyo ndege inatarajia kuondoka saa 9 alasiri. Ilibidi tumsubiri pale huku tukiendelea kupiga story mbalimbali na muda ulivyotimia wakucheck-in Manuel aliota Pesa nyingi tu akampa wife na Junior.

Baada ya kuachana na wife tulikwenda Cocobeach kupoteza muda na baada ya kuwasili pale tulikwenda kukaa kwa siku zote na baada ya jamaa kutuona alikuja kutupokea. Tuliagiza vinywaji pale kwa upande wangu nili odda heineken na yeye ali odda Kilimanjaro beer.

Muda huu tulikuwa tunazungumza masuala ya maisha na pia nilimwambia sababu ya kuacha biashara ya Uber na jinsi mambo niliyopitia mpaka kifo cha Pama. Manuel kwa upande wake ananikubali sana na alisema baada ya miaka 10 anaamini nitakuwa millionaire mkubwa na kila siku huwa analisemaga hili.

Baada ya muda mfupi jamaa alileta vinywaji pale na alionekana kuna jambo anataka kuniambia,

“Brother afu kuna dada wa kiarabu kuna siku mlikaa wote hapa alisema anaitwa Sia, alikuwa anakusalimia.”

“Wow alikuja lini hapa?”

“Alikuja Jumapili, alisema kama hutojali unaweza kuniachia namba yako.”

“Haina shida navyoondoka nitakuachia mkuu.”

Sia kipindi kile tumekutana tuliongea mambo mengi sana hivyo sikuona tatizo kuacha namba yangu ya simu.

Tulikaa pale Cocobeach na Manuel mpaka saa 1 usiku ndo tukaondoka maeneo haya lakini nilisahau kuacha namba yangu ya simu kwa jamaa. Nilimpeleka Manuel pale Ramada Hotel na mimi niliamua kupitia Juliana kwenda kuendelea kunywa maana home hakukuwa na mtu hata dada nilimwambia aende ukweni mpaka mama J atakavyorudi.

Wakati naendelea kukimbiza chupa simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Sumaiya na mimi muda huu ilibidi nitoke niende parking kwenye gari ili nipokee simu yake tuongee. Kwa upande mwingine simu iliita mpaka ikakata hivyo baada ya kuingia ndani ya gari nikampigia simu na haikuchukua muda akapokea,

MIMI: “Hi mummy.”

SUMAIYA: “Insider nimesimamishwa kazi na Queen leo.”

MIMI: “Umesimamishwa? umefanya nini?”

SUMAIYA: “Hata sijui kwakweli maana Queen alikuja ofisini na mimi nilikuwa sijafika bado, ndo akaacha haya maagizo kwa Asmah.”

MIMI: “Aisee mimi sijui na hajanipa hizi habari, lakini subiri kukusimamisha sio kukuaachisha kazi atakuwa kachukia tu. Kama kukuachisha angekupa barua na huu ndo utaratibu na masuala ya HR yako chini ya Mama Janeth na sio kwake.”

SUMAIYA: “Insider jana demu wako kaja ofisini amenuna balaa kila mtu alikuwa anamwogopa sijui kakutana na mashine kubwa jana.”

MIMI: “Tutaonana kesho ili tuongee vizuri.”

SUMAIYA: “Insider sitakiwi kuonekana hapo ofisini au huelewi? Naomba uniombee msamaha kwa Queen maana sikuchelewa ofisini makusudi, nilienda kwa mama Banana, mwanangu anaumwa hata hapa bado nipo kwa mama, nilisahau kutoa taarifa mapema.”

MIMI: “Kumbe una mtoto na hujawai kuniambia hili.”

SUMAIYA: “Insider hujawai kuuliza maisha yangu sasa ulitaka niropoke na mtoto?”

MIMI: “Haina shida niachie hili nilifanyie kazi ila unaweza ongea na mama Janeth.”

SUMAIYA: “Iryn ndo top kwenye hii kampuni na amerithi nafasi ya mama yake, mama Janeth anaplay party yake tu.”

MIMI: “Incharge kapewa nani sasa?”

SUMAIYA: “Inamaana wewe hujui kinacho endelea? au unanichora tu hapa.”

MIMI: “Iryn hajanambia kabisa rafiki yangu ndomana unaona nashangaa hapa.”

SUMAIYA: “Asmah ameachiwa uongozi kwasasa na hizi ndo taarifa nilizopata.”

Nilijisikia vibaya sana muda huu na mimi nilijua Iryn kamuachisha kazi Sumaiya sababu yangu na sio kingine. Kwa upande wangu sikutaka kumwambia Sumaiya kama mimi na Iryn tumezinguana niliamua kunyamaza. Na mimi niliondoka palepale sikutaka kurudi kumalizia vinywaji vyangu.

Asubuhi ratiba zangu zilikuwa kama kawaida na mapema sana nilikuwa nimewasili pale Masaki na nilimkua Asmah pale ofisini amewasili tayari, kwa upande mwingine nilishangaa kuona ana andaa hesabu za mauzo. Ilibidi nimuulize kinachoendelea na alisema ameambiwa na Iryn aandae hesabu na aende bank kudeposit pesa.

ASMAH: “Insider, Bossy ndo katoa haya maagizo na mimi nimeogopa hata kumuuliza maana nafahamu hili ni jukumu lako, jana kamuachisha kazi Sumaiya najua una habari.”

MIMI: “Sumaiya alinipigia simu jana usiku hata mimi nimeshangaa maana ni ghafla sana.”

ASMAH: “Hapa kila mtu anaogopa sahivi, ni nini kinaendelea kati yenu? From nowhere haiwezekani anambie nitume ripoti za mauzo wakati ni kazi yako.”

MIMI: “Ni story ndefu kidogo lakini nakuona hata wewe hauko sawa kama una wasiwasi.”

ASMAH: “Insider mimi na wewe tunafanya ujinga lakini kwa hapa ofisini tuwe na mipaka mimi sitaki kuingia kwenye ugomvi na Bossy na nina muheshimu sana.”

MIMI: “Sawa lakini inaonekana Iryn kakuchimba sana mkwara, bye Asmah mimi naondoka kama kuna lolote utakuwa unanijulisha.”

ASMAH: “Poa Insider usijali weekend hii tuonane kama vipi.”

Kutokana na hili suala la ripoti za mauzo kuandaa Asmah lilinipa ukakasasi sana, nilitoka pale Masaki na nilichoma mafuta mpaka Mikocheni ili nikaonane na Lucy. Baada ya kuwasili pale Mikocheni niliingia ofisini moja kwa moja na nilimkuta Lucy anakunywa chai.

LUCY: “Insider bora nimekuona mshikaji wangu.”

MIMI: “Unashindwa kunambia kama sina kazi kwasasa seriously?”

LUCY: “Jana nilitegemea ungekuja lakini ukanambia unampeleka wife Airport, sasa Bossy jana alikuja akanambia niwe natuma ripoti za mauzo kwake.”

MIMI: “Na kuhusu mimi hajasema kitu?”

LUCY: “Nothing, kwanza niambie ni nini kilitokea huko? Maana Iryn anasema alisikia maongezi yenu yote na akajua yule Prisca ana mimba yako, ilikuwaje mpaka mnaongea haya mbele ya Bossy?”

MIMI: “Nilikutana na Best yake Prisca pale Capetown na yeye ndo aliyeniona na aliniita shem…, hapa Iryn ndo alishtuka na akaanza ku-monitor maongezi yetu, aliongea na mimi hata dakika 3 hazikufika akaondoka. Bossy wako alianza umbeya kufuatilia maongezi yasiyo muhusu, lakini dada alikuwa kalewa na haikuwa akili yake maana nilitumia mbinu zote kumtuliza lakini wapi.”

LUCY: “Insider unajua hapa duniani hakuna siri unakumbuka ulinikatalia hamna mahusiano?, na hiyo mimba vipi sasa?”

MIMI: “Mimba iliharibika rafiki yangu, nishauri kwa hili tunafanyaje?”

LUCY: “Pole sana rafiki yangu, ila haya yote umeyataka mwenyewe maana unapuuziaga mambo.”

MIMI: “Huu sio muda wa kuninanga bali nipe formula nachomokaje?, hata kwenye simu kaniblock kuonesha hataki tena kusikia sauti yangu.”

LUCY: “Jaribu kuongea naye kwa simu yangu afu tuone response yake.”

Nilimpigia simu Iryn kupitia simu ya Lucy na baada ya kupokea na kusikia sauti yangu alikata simu.

MIMI: “Lucy unaona I told you.”

LUCY: “Nenda kwake leo anaweza kuwa ametulia tofauti na jana. Insider kwasasa ndo muda muhafaka wa kuyamaliza haya mambo, usiendelee kupoteza muda maana hatujui balaa atakaloleta.”

MIMI: “Alete balaa gani wakati kamsimamisha Sumaiya kazi bila sababu ya msingi.”

Ilibidi nimsimulie Lucy mkanda mzima kuhusu sakata la Sumaiya mpaka anaachishwa kazi, kwa upande wake alionekana kuumia sana kwa haya maamuzi ya Iryn. Kwa upande wangu sikutaka kuendelea kupoteza muda hivyo nilimuaga na nilikwenda moja kwa moja mpaka kwa Iryn.

Baada ya kuwasili pale getini nilipiga honi lakini kwa upande mwingine nilimwona Mlinzi akija direct usawa wangu.

“Mzee shikamoo mbona hufungui gate?”

“Kaka tumepewa maagizo tusikuruhusu kuingia ndani, na sisi kama walinzi hatuwezi kukuruhusu kuingia maana tunaweza fukuzwa kazi.”

“Shit!, what the fvck?

Nilikaa pale getini kwa dakika 5 na nikaondoka kurudi home kupumzika. Wakati niko home kwa upande mwingine Prisca alinipigia simu na kubwa alikuwa anakumbushia appointment yetu maana nilimuahidi leo. Kwa upande wangu sikuwa hata na mood ya kuonana naye hivyo nikamwambia tutaonana kesho jumamosi.

Usiku nilikwenda Ramada kuonana na Manuel ili tutoke out lakini tulipitia kwanza pale Juliana kupata kitimoto. Baada ya kula tulindoka kwenda “25 Lounge” ya pale Makonde, kwa upande mwingine Manuel alikuwa ana miadi na ile pisi ya Kidimbwi hivyo walikubalina wakutane pale.

Baada ya kuwasili pale tuliendelea kunywa taratibu huku tunapiga story na kubwa alinisisitiza sana nisiachane na mama J maana ametokea kumkubali sana. Pia aliuliza maendeleo ya biashara zangu za Dodoma maana kipindi amekuja May nilimwambia na mpango wa kufungua biashara Dodoma na alinisaidia kiasi cha pesa. Sikutakaga kumwambia ukweli kuwa najenga Dodoma hata watu wangu wote wa karibu nilikuwa siwambii hili.

Baada ya lisaa yule dada aliwasili pale na alisema anakaa Sinza, tuliendelea kupiga story pale na dada alionekana kumuelewa sana Manuel. Midnight tuliamua kuondoka na Manuel alisema haina haja ya kuwapeleka hivyo wata-request usafiri wa kuwapeleka.

*******
Jumamosi Manuel alikuwa na safari ya kwenda Uswiss na alitarajia kuondoka saa 9 mchana na alitakiwa kucheck-in saa 7 mchana. Mapema sana nilikwenda kumchukua na nilimkuta yuko na pisi yake ya jana na tuliongozana wote tukaidrop ile pisi pale Mlimani city na wakaagana na Manuel.

Baada ya kuwasili Airport tuliendelea kupiga story pale mpaka muda wa kucheck-in ulivyofika tuliagana kwa kukumbatiana na akaondoka. Manuel alifurahi sana kuiona familia yangu na alichoniahidi ni kumpa Junior connection za masomo Uswiss hapo baadae, pia alisema itabidi na mimi niende Uswiss nikatembee.

Ilikuwa ni saa 8 mchana tayari wakati tunaagana na Manuel hivyo baada ya kurudi parking nilimpigia simu Prisca ili tuonane, tuyajenge. Baada ya kuwasiliana naye alinambia yuko kwake hivyo nikamwambia itapendeza akisogea mpaka Mlimani City.

“Baby I thought unakuja home au hujanimiss?”

“Wewe njoo hapa Mlimani City na nikukute hapo mimi natokea Airport.”

Baada ya kuwasili pale Mlimani niliamua kwenda kukaa kwenye mgahawa ambao unapakana na “Kuku kuku.”. Niliagiza chakula maana nilikuwa na njaa sana, na baaada ya nusu saa Prisca aliwasili pale na alikuwa kapendeza sana tena alikuwa na muonekano mpya. Na yeye kwa upande wake aliagiza chakula,

MIMI: “Ulivyokuwa unasema nije kwako kumbe hata hujapika.”

PRISCA: “Ungesema unakuja ningekupikia mme wangu. Pia nimekuja kuomba msamaha kwa lile jambo la sikuile.”

MIMI: “Prisca unakumbuka before hatujaingia kwenye mahusiano nilikwambiaje?”

PRISCA: “Ulinambia una mke na mtoto.”

MIMI: “Ndo unakumbuka hivyo tu?, sawa nilikwambia wewe ni mchepuko kwangu na unatakiwa kuwa na heshima kwa mke wangu. Kitendo cha kumuita mke wangu malaya tena mama watoto wangu kwa hili siwezi kukusamehe na kunzia leo mimi na wewe bhasi naomba tusitishe mahusiano yetu kwa maelewano mazuri.”

PRISCA: “Insider what are you talking about? Mbona sikuelewi, so umenitumia unavyotaka isitoshe ukanipa na mimba, leo hii ndo unaniambia habari za kuachana?.”

MIMI: “Prisca umeshindwa kufuata masharti tuliyopeana umebreach contract mwenyewe maana kama kukupenda nilifanya na nilikujali sana na wewe unajua hili. Kwasasa acha nifocus na familia yangu yaliyotokea na wewe ni bahati mbaya na elewa siwezi kumpoteza mama J kwaajili yako, naomba kuwa muelewa.”

PRISCA: “Insider wewe ni Playboy, Bossy wako ndo mchepuko wako kwasasa taarifa zako ninazo.”

Na muda huu Prisca alitoa simu yake na akanionesha picha ambayo ilionesha mimi kuwa na Iryn kule Capetown na nilijua lazima Eva alitupiga na akamtumia Prisca.

MIMI: “Clever Eva, mwambie nitamuajiri kwenye kampuni yangu ya upaparazi, mimi naondoka kwaheri nafikiri hakuna nilicho acha kwako.”

PRISCA: “Insider you can’t do that, You’ll pay for this and I swear.”

Na mimi niliamua kuondoka na nilimuacha pale amekaa akiwa haamini kilichotokea, ofcourse niliachana na Prisca muda huu lakini nilikuwa bado nampenda sana, licha ya kuniomba sana msamaha na kuahidi kutorudia tena, kwa upande wangu sikuwa na jinsi maana niliona angekuja kuleta maafa makubwa zaidi huko mbeleni.

Baada ya kuingia kwenye gari niliwaza kwenda kuonana na Lucy pale ofisini ili tushauriane juu ya hili suala, kwa upande wangu hofu yangu kubwa ilikuwa ni wife tu wala sio Iryn.

Baada ya kuwasili pale ofisini nilikwenda moja kwa moja mpaka ofisini lakini nilipitia kwanza kitchen na nilikuta kuna wine kwenye fridge nikaibeba. Nilitulia pale ofisini na nilianza kuigugumia ile wine kwa fujo sana na muda huu Lucy aliingia ndani.

LUCY: “Insider unakunywa wine ya wenzako watamind sana.”

MIMI: “Nitaacha hela wakanunue nyingine.”

LUCY: “Jana ulikuwa hupokei simu zangu na leo asubuhi ulikuwa unatumika na hukutaka kunirudia, nambie jana ulienda kwake?”

MIMI: “Yes I went, lakini nimefika getini nikazuiwa na mlinzi rafiki yangu sina hata hamu kwasasa.”

LUCY: “Daah! pole sana mshikaji wangu, leo nimeongea naye mmalize tofauti zenu lakini yeye anasema hana shida na wewe ila hataki kukuona machoni pake.”

MIMI: “Hizo sio habari za kunambia Lucy kwamba umeshindwa kumlainisha?”

LUCY: “Kuna jambo sikukwambia, Iryn anasema wewe ndo mwanaume pekee ambaye ulifanikiwa kurudisha furaha yake na pia wewe ndo uliye ondoa furaha yake.”

MIMI: “What do you mean?”

LUCY: “Iryn anasema mambo yote uliyomfanyia kwasasa inatosha hataki kukuweka close tena.”

MIMI: “Sasa unanishaurije maana mimi hata sielewi, kama atamwambia wife inaweza leta shida.”

Na muda huu nilimalizia wine ilokuwa imebakia kwenye chupa yote mdomoni, na Lucy alibaki mdomo wazi.

LUCY: “Insider njia pekee ambayo naweza kukushauri ni kumla tu maana Iryn anaonekana bado anakupenda ila anajifanya like I don’t care.”

MIMI: “Kwa hii stage tuliyofikia kwasasa naona ni ngumu sijui nitatoboaje.”

LUCY: “Insider kwamba umekosa kabisa mbinu ya kuonana na Iryn?, sikia ukiweza kumla utakuwa umepiga ndege wa2 kwa jiwe moja, na Iryn anakupenda akikuona tu machoni pake utamla trust me, mimi naondoka nakazi huko si unajua jumamosi leo wateja ni wengi?”

Nilikaa pale kama dakika 20 na nilikuwa nawaza kichwani namna ya kuingia kwa Iryn na nilimua kuondoka nikasema leo liwalo na liwe kama nitafanikiwa kuingia ndani lazima nimle.

Baada ya kuwasili pale getini kwa leo nilimkuta Mlinzi mwingine pale getin ambaye ni mama na baada ya kuliona gari langu alikuja mpaka usawa wangu akanambia kuwa siruhusiwi kuingia ndani na amepewa hayo maelekezo. Lakini kwa upande wake alikuwa anashangaa maana mimi pale ni kama home tu,

“Mama nani katoa hizi taarifa?”

“Mzee ndo amenipa hizi taarifa hata mimi nimeshangaa kwakweli, kwani kuna tatizo gani?”

“Mama tumegombana na huyu mpenzi wangu sasa hataki kuniona wala tuyajenge ndomana unaona hataki niingie humu ndani, lakini mimi nimekuja ili tuyajenge, hivyo naomba niruhusu niingie nikaongee naye, unanijua vizuri siwezi kuleta shida yoyote.”

“Upo sahihi kumbuka na mimi hapa nimeajiriwa nikikaidi haya maagizo nitakuwa matatizoni, jaribu kumpigia simu ili aje.”

“Ameni-block mama, naomba umpe taarifa kuwa nipo hapa nje kama atakataa bhasi, naomba msaada kwa hili nitakupa hela ya sukari ya mtoto.”

“Labda nimpigie simu lakini kwenda ni ngumu.”

Mama alipiga simu pale lakini hakuwa na majibu yoyote na alipiga mara 5,

“Unaona simu hapokei kwa hapa sina msaada mwingine, kwaheri.” Na muda huu aliingia ndani akafunga geti.

Nilikaa pale nje kwa dakika 10 hivi nikifikiria cha kufanya lakini nilikosa majibu hivyo niliamua kuondoka, sasa ile narudisha gari reverse geti lilifunguliwa akatoka mama na akanipa sign ya kusimama na akaja usawa wangu.

“Kaka wewe unanisaidiaga sana nitakuruhusu uingie ila naomba usilete tatizo lolote na utaniachia funguo ya gari.”

“Ahsante mama nashukuru sana chukua na hela yako ya sukari mapema maana naweza toka huko nimechanganyikiwa, kama kuna tatizo nitakupigia simu.”

“Nashukuru sana tuko pamoja kuwa na amani, nafikiri mtayajenga huko ndani.”

Nilifungua kwenye drow kulikuwa na elfu 50 nikampa na mama alifurahi sana, Mama alinifungulia gate na mimi nikaingia ndani na nikapark gari upande mwingine na nikampa funguo ya gari.

Muda huu nilikuwa natembea kuelekea apartment ya Iryn lakini kwa upande mwingine nilikuwa naogopa sana, nilikumbuka Iryn ana gun , niliwaza vipi kama ataamua kunitia risasi?.

Baada ya kufika mlangoni sikutaka hata kugonga bali nilifungua mlango na kuingia ndani, uzuri ulikuwa haujafungwa. Baada ya kuingia seblen kwa upande wake alikuwa yuko jikoni hivyo nilienda moja kwa moja, na nilimkuta anaosha vyombo.

Na mimi nilimuita “Iryn…..”

IRYN: “Insider what are you doing here? na nani kakuruhusu kuingia ndani? Sitaki kukuona kwenye macho yangu naomba uondoke before I call the Police.”

MIMI: “Iryn, calm down please, nimekuja kwa mazuri nachotaka kwako ni just five minutes zinanitosha kabisa, then maamuzi yatabaki kwako.”

Na mimi nilimsogelea na alikuwa ameegemea karo la kuoshea vyombo. Baada ya kumsogelea na kuwa naye close, nilijaribu kumvuta nimpe kisi lakini niliishia kuchapwa na kibao cha nguvu sana muda huu, kwa upande mwingine Iryn hasira zake zilionekana kupanda.

Kile kibao kiliniingia sana maana alinipiga cha sikio hivyo nilikuwa nasikia “nziii nziii…..”., ukweli sikuamini kama Iryn angenipiga kibao cha nguvu kama kile. Kwa upande wangu sikutaka kuendelea kubaki maeneo haya maana ningeleta matatizo zaidi hivyo niliamua niondoke.

TO BE CONTINUED
Mmmmhhh
Nziiii umeyakanyaga tna mara ya pili pi w
 
Broh laki 2 kwaajili ya mtoto unaona ni kubwa? Maana kwa Junior nikiingia shopping inanitoka si chini ya laki 3, bila shaka huna mtoto.

Pampas kwa mtoto mchanga kwa mwezi si chini ya 60k

Mama watoto kula kwa mwezi bajeti andaa 100k

Ungekua na mtoto usinge comment shit kama hii,
I've got Two kids wanakula hela hatari kuna mda nikimwangalia mwanangu anavyofakamia nyama nawaza siku nikikosa hela ya nyama inakuwaje

Watoto ni gharama kweli kweli. Unamvalisha pampers anakunya hapohapo mda huo huo🤣

Mzee malizia story tufanye maisha mengine
 
I've got Two kids wanakula hela hatari kuna mda nikimwangalia mwanangu anavyofakamia nyama nawaza siku nikikosa hela ya nyama inakuwaje

Watoto ni gharama kweli kweli. Unamvalisha pampers anakunya hapohapo mda huo huo

Mzee malizia story tufanye maisha mengine

Hawa vijana hawana familia mimi Junior bajeti yake ya mwezi ni balaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom