Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,441
- 40,425
Wakuu habari za jioni?
Kuna mdada mmoja nilimpenda sana, nikafa nikaoza; nilikuwa tayari nilale njaa ili tu yeye aweze kufurahi.
Mahusiano yangu naye, yalikuwa na changamoto sana, huna hela lazima mkorofishane au mtafute sababu mbili tatu mzinguane.
Nikajifanya mjinga ili nitundike ki-zygote, nikiamini atabadilika huko mbeleni.
Katika harakati zangu za kupambana ili apate ki-zygote, kumbe nayeye kwa upande wake alikuwa akipambana na kutumia vitu vya kiimani (nabii) ili iweze kunasa bila mimi kujua.
Kutokana na ujuzi na shabaha, kitu kikanasa; mtoto akaanza kudeka, na katika kudeka kwake kukaleta athari kwenye uchumi; ikanibidi baadhi ya mahitaji yasiyo ya lazima nayafyekelea mbali.
Ile ilimpelekea kidogo kuwa na hasira, na kuniambia nifute namba yake; nami nilitii, ingawa nilisema kwa sababu ana kiumbe changu huko mbeleni nitakiitaji.
Sasa leo nimeamua kumchokoza kwa kumuuliza, vipi maendeleo ya kiumbe changu; kidogo akawa mkali na kusema sitakiwi kujua maendeleo yake.
Nikamwambia akizaliwa na akawa amechukua sura ya baba (yangu) namchukua; hapo ndipo akawa mkali zaidi, na kusema ukitaka maisha yako yawe mafupi uje ufanye hivyo.
Sasa hapa natafakari, naona kama vile mbegu yangu imepotea; na kwa kawaida, mbegu yoyote nzuri ni gharama, kwa nini yeye awe amejipatia bure?
Wakuu, leteni ushauri.