Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 57

Baada ya kumpandia hewani Dav alisema yuko tayari kwenda ilimradi uwe mkataba wa uhakika na nikamwambia aandae CV na vyeti viwe karibu.

CONTINUE

Jumapili asubuhi nilipigiwa video call kutoka kwa Iryn kubwa alikuwa ananisalimia pamoja na kunipa taarifa za kufika salama Ethiopia. Muda huu alikuwa kutembelea kaburi la mama yake na alikuwa ananionesha kupitia video. Kwa upande mwingine walionekana watu tofauti pale kaburini na alinambia ni ndugu zake,

“Insider huyu ni dada yangu tumefanana eeh.”

“Mmefanana aisee ukoo wenu umebarikiwa kwakweli.”

Hao ndugu zake walikuwa ni wazuri balaa.

Yalikuwa ni maongezi kama ya dakika 15 hivi na Iryn aliniaga kwani alisema wanapanda maua na kuosha kaburi.

Kwa upande mwingine toka lile sakata la Prisca litokee alikuwa kaniblock namba zangu zote mpaka Whatsapp hata hali yake nilikuwa sijui ikoje. Ilibidi nimpigie simu Mary ili nijue maendeleo yake na baada ya kupiga simu ilisikika sauti ya Ivy kwa simu,

IVY: “Shem shikamoo.”

MIMI: “Wow Ivy hujambo?.”

IVY: “Sijambo kwanini unamkasirisha dada Prisca?

MIMI: “Kwanini na wewe unapokea simu ya da Mary?”

IVY: “Kanipa nicheze game! yeye anapika na da Prisca.”

MIMI: “Mpe simu da Prisca niongee naye sawa eeh.”

IVY: “Da Prisca hataki kuongea na wewe…”

Na muda huu Mary alichukua simu na tukaanza maongezi.

MARY: “Insider wewe na mama kijacho wako kwani mnashida gani? Mapenzi yenu huwa siyaelewi kabisa. Ni nini kinaendelea?”

MIMI: “Yeye anasemaje?”

MARY: “Hajasema lolote.”

MIMI: “Itakuwa mimba inampa mabadiliko so inabidi umzoee tu mdogo wako.”

Kwa upande mwingine nilikuwa simwambii Mary mambo yangu na Prisca maana kama mdogo wake alikuwa hamwambii mimi ninapatia wapi hiyo nguvu?.

Jioni niliondoka kwenda kwa Mama wa2 kwaajili ya kuzungumza suala la dili ambalo alikuwa kanipigia assist na baada ya kuwasili pale kwake alisema twende sehemu nzuri tukatulie.

Tuliamua kwenda Ramada Hotel kwa upande wa mama wa2 alikuwa kaongozana na bint yake Rachel. Ulikuwa ni mwendo wa dakika 10 mpaka tunawasili pale na baada ya kuingia ndani tulikwenda kukaa karibu na swimming pool kwenye miamvuli.

Kila mtu aliagiza anachotaka muda huu na baada ya hapo maongezi yaliendelea kuhusu suala la kazi.

Kwa ufupi, Mama wa2 alinambia ile baada ya mimi kumtumia CV alianza michakato mapema na mtu aliyemcheki ni Baba Rachel, hivyo kuwa na qualifications nzuri zilimvutia sana Baba Rachel na palepale alimvutia waya HR na akasema kuna nafasi Mtwara ipo wazi na inahitajika kujazwa haraka sana, ila kwa Dar es Salaam hakuna kwa kipindi hiki.

“Aisee Mama mkwe umeupiga mwingi sana hujalipia kweli kwa Baba Rachel?”

“Hahaha Insider wewe ni mshenzi sana, yule ni Baba mtoto wangu hanaga shida na ananisaidiaga mambo mengi sana, mtu kama huyu unaanzaje kumkazia.?”

Hata mimi nilishindwa kumjibu maana niliona mama wa2 yuko sahihi kabisa.

Mama wa2 alinambia ilibidi anipambanie mapema maana alihisi niko kwenye wakati mgumu kutokana na suala la biashara kuwa ngumu. Mama wa2 alinisisitiza niende Mtwara afu baada ya mwezi ningerudi Dar es Salaam na alinihakikishia kwa 100%.

“Mama mkwe kwanza niseme ahsante sana kwa yote ila wakati jana unanipigia simu sikutaka kukataa hili dili maana ninge kuvunja moyo. Pia muda ule nilikuwa nimetoka kuonana na yule Mzee Juma nilokwambia kaachiwa maagizo na Mzee kuhusu kazi.”

Muda huu ilibidi nimpe mkanda mzima kuhusu Mzee Juma na mama wa2 hakuwa na shida kwani alinielewa na alifurahi sana kusikia hizi habari.

“Mama mkwe nafasi hii imepatikana tukisema tuiache ipotee hewani hata Baba Rachel ataona hatuko serious. Naomba tumpe ndugu yangu kama itawezekana yeye ana Digrii ya Finance na yuko vizuri.”

“Sawa Insider haina shida mwambie akutumie CV na certificates tuone kama anasifa maana kwasasa hili jambo liko chini yangu.”

Ilibidi niwasiliane na Dav muda huu na chap akanitumia CV yake pamoja na vyeti na baada ya kumuonesha mama wa2 alizikubali na akasema kesho aende ofisini wakaonane.

Nilimpigia simu Dav na nikampa hizi taarifa lakini kwa upande wake alijua kama natania hivi maana alikuwa dizaini kama haamini nachomwambia muda huu.

Tulikaa pale na mama wa2 mpaka saa 3 usiku na alikuwa kashazipeleka Savanna 6 na alionekana kuwa hoi sana na mtu mwenye upwiru.

Niliwapeleka home na mwanae na kabla hawajashuka nilimkabidhi mama wa2 pesa na niliclear deni lote la mkopo lililokuwa limebaki. Mama wa2 alinipongeza sana na akanambia nikitaka mkopo mwingine mkubwa nimwambie muda wowote.

Tuliagana na mimi nilimkiss shavuni kama shukrani ya kunisaidia kumpa kazi jamaa yangu na mimi niliondoka kwenda home kulala.

Jumatatu asubuhi niliwasiliana na Dav na nilimpa maelekezo jinsi ya kufika ofisini ili kuonana na mama wa2 na nilimpa namba zake za simu ili wawasiliane.

Ile mchana Dav alinirudia na alinipa taarifa ya kupewa mkataba wa kazi na Bank hivyo jumatano ataanza training. Kwa upande wake alinishukuru sana maana alikuwa haamini mpaka alivyopewa mkataba wa kazi na kuusaini hapo ndo sasa alijua ishu kweli ni serious.

Dav alishangaa sana kuona kupata kazi kimasihara tena bila hata kufanya interview zaidi alihojiwa kidogo na mama wa2. Aliniuliza nimezipataje hizi connection na mimi nikamwambia tukionana tutaongea haya yote.

************
Jumatano nilikuwa na miadi na Mzee Juma kama tulivyokubaliana jumamosi na alisema safari itaanzia kwake Mikocheni.

Kwa upande mwingine kwa siku za kazi ratiba zangu zilikuwa vilevile, kwa ile asubuhi lazima nimpeleke mama wa2 ofisini kwake lakini hii kazi ilikuwa imesha nichosha tayari na nilikuwa natamani sana mama wa2 anunue gari. Na baada ya kuachana na mama wa2 nilikuwa nakwenda salon zote kukagua mauzo na kisha kupeleka pesa Bank.

Hii siku baada ya kumalizana na ofisi ya masaki niliamua kwenda kutulia pale Mikocheni kwa Lucy huku nikibuy time ya kwenda kwa Mzee Juma na nilikuwa na wazo kichwani ambalo nilipenda sana kumshirikisha Lucy.

Nilimshirikisha Lucy kuhusu mpango wa kumshauri Iryn awe anatoa mikopo kwa wafanyakazi wake ili kuwasaidia kiuchumi pale wanapokwama. Kwa upande wa Lucy aliunga mkono mpango huu na alisema ni mzuri sana hivyo nikaplan Iryn akirudi nitamshirikisha.

Saa 6 mchana niliwasiliana na Mzee Juma na akanielekeza nyumbani kwake, na mimi sikutaka kwenda na gari hivyo niliacha gari pale kwa Lucy nikaenda kwa Bodaboda.

Baada ya kuwasili pale kwake nilikaribishwa ndani seblen na nilikuwa niko peke yangu pale nikishangaa ukubwa na uzuri wa ile sebule. Na baada ya dakika 5 alitoka Camilla na tukasalimiana na alimwambia dada aniletee kinywaji na mimi niliomba niletewe maji tu.

Pale sebleni kulikuwa na picha kubwa ya familia na niliweza kuwaona watoto wa Mzee Juma na mke wake, ilikuwa ni familia ya watoto 3 tu.

Baada ya nusu saa Mzee Juma alitoka na nilisimama kumsalimia na yeye alimuita Camilla pale seblen.

MZEE JUMA: “Hivi nyie mmelelewaje? Unamuachaje mgeni seblen peke yake?”

CAMILLA: “Sorry daddy nilikuwa namwambia kaka aoshe gari tunayo ondoka nayo.”

MIMI: “Mzee naona familia yako yote kwenye picha lakini wengine siwaoni.”

MZEE JUMA: “Kaka yao kama nilivyokwambia siku ile anafanya kazi nje, Camilla ndo huyu na uyo mdogo wao anasoma India science, Mama yao yuko kazini.”

MIMI: “Hongera sana Mzee.”

MZEE JUMA: “Sasa ngoja amalizie kuosha gari tuondoke na mimi nikajiandae.”

Mzee Juma aliondoka na alituacha pale seblen mimi na Camilla. Muda huu tulikuwa kimya pale seblen hakuna aliyekuwa anamsemesha mwenzake mpaka Mzee Juma alivyotoka ndani.

Mzee Alisema tuondoke yuko tayari na baada ya kutoka nje gari tuliyokuwa tunakwenda nayo ni Jeep na Camilla alikuwa dereva.

Ulikuwa ni mwendo wa dakika 45 mpaka tunawasili Mbweni kwa Jane na tulikaribishwa ndani seblen.

Muda huu mazungumzo yalikuwa yakiendelea pale seblen na mimi nilikuwa napiga story na Vicky mdogo wake Jane na alikuwa yuko likizo kipindi hiki amefunga chuo.

Baada ya nusu saa tulipata lunch ya pamoja na baada ya lunch Mzee Juma alitoka na Jane nje garden, walikuwa na mazungumzo private hasa mipango ya kwenda Tabora kumaliza msiba pamoja na mirathi na wiki hii walitakiwa kuondoka Dar.

Nilitoka nje nikiwa nimeongozana na Vicky na nilikwenda moja kwa moja kuangalia gari yangu na ilionekana kuchubuliwa kwelikweli hasa kwenye bampa zote nyuma na mbele.

VICKY: “Dada amekuharibia gari yako si unaona kazi hiyo.”

MIMI: “Ni kawaida hata hivyo kajitahidi, lakini atakaa sawa tu bado ana ulena.”

VICKY: “Lakini alisema atakununulia gari nyingine hii ataendelea kujifunzia.”

Tuliongea mambo mengi sana na Vicky muda huu na tulikuwa tumezoeana hivyo story zilikuwa nyingi sana na tulikuwa tumekaa nje kibarazani muda huu.

Saa 10 jioni tuliondoka pale Mbweni na tulikwenda mpaka Ununio kwa Mrs. Pama, tuliwakuta watoto wake wote na ndugu wengine lakini Mrs alikuwa kazini.

Tuliwasalimia na tulitumia lisaa kukaa pale Ununio na tukaondoka maeneo yale na break ilikuwa Bahari Beach kwenye gate ambalo lina uzio mkubwa. Na baada ya kuingia ndani nilijua lazima lile ni eneo la mzee maana lilionekana kuwa kubwa sana afu halijajengwa.

Tulitumia pale kama nusu saa na Mzee alionekana kuwa busy na bint yake kama wakipanga mipango yao kuhusu eneo hili.

Wakati tunarudi niliomba waniache pale Palm village ili iwe rahisi kwenda ofisini kuchukua gari. Baada ya kuwasili pale tuliagana na akanambia jumamosi wataondoka na Jane kwenda Tabora hivyo akirudi tutaongea na lile jambo letu.

Kwa upande mwingine hii siku pia Prisca alinipigia simu wakati niko na Mzee Juma na aliniomba msamaha kwa lile jambo na alinipa taarifa za kuanza field na pia nikamwambia jumamosi tutaonana maana nina safari ya Dodoma.

*******
Ijumaa niliandika barua vizuri ya kuomba emergence ya siku 5 na niliituma kwa mama Janeth.

Kwa masuala ya Human resource yote yapo chini ya Mama Janeth na masuala ya Fedha yapo chini ya Iryn.

Baada ya kumtumia ile barua kwenye e-mail, mama Janeth alinipigia simu na akaniuliza nimepata shida gani na mimi ilibidi nimwambie ni masuala ya kifamilia tu.

Mama Janeth hakuwa na tatizo na alinipa ruhusa pamoja na kunitakia safari njema ya Dodoma. Na alinambia kama kuna jambo lolote nitahitaji nimwambie na mimi nilimtoa wasiwasi.

Kwa upande mwingine Iryn alisema angerudi Ijumaa ya week hii lakini baada ya kuwasiliana nae alinambia anakwenda kwanza Ufaransa hivyo atarudi jumatano, na mimi sikutaka kumwambia kama nimeomba emergence sababu hili suala halikuwa chini yake.

Niliongea na Lucy pamoja na Sumaiya ili wawe wananisaidia kuziingiza Pesa bank kipindi ambacho sitokuwepo, kwa upande wao hawakuwa na shida hivyo walinitoa wasiwasi.

Baada ya kumalizana na Lucy nilikwenda kuonana na Dalali kwaajili ya kwenda kuangalia nyumba na baada ya kuzikagua zote niliipenda nyumba ambayo ilikuwa mbezi Beach upande wa chini unaingilia sheli ya Puma.

Mazingira ya nyumba yalikuwa mazuri mpaka usalama hata kodi ilikuwa ya kawaida. Kwenye compound kulikuwa na jumla ya nyumba nne tu, baada ya kuridhika na nyumba ilibidi niwasiliane na wife kwanza na baada ya kuyaona mazingira kupitia simu alisema nilipie tu haina shida.

Kutokana na suala la kupatikana kwa nyumba tulishauriana na wife tuhamie kabla ya safari ili tukirudi Dodoma twende moja kwa moja makazi mapya.

Jumamosi tulipanga tuhamie pale na ile asubuhi tulikwenda wote kufanya usafi kwenye makazi mapya. Wakati wanaendelea na usafi kwa upande wangu na Junior tulikuwa tunabeba vitu vidogo vidogo tunapeleka. Mpaka kufikia saa 2 usiku kila kitu kilikuwa kimekamilika kwa upande wa kuhamia makazi mapya.

Baada ya kuona mambo yameenda sawa ilibidi nichomoke ili nikaonane na Prisca ili nimjulie hali kabla sijaondoka. Sikutaka kuwaaga na muda huu walikuwa wanapanga vitu vizuri pale sebleni.

Baada ya kuwasili pale getini Prisca alitoka na Mary na tukaondoka kwenda mpaka “Target” ndo tulichill pale. Tuliagiza chakula pale na story zilikuwa zinaendelea pale wakati tukipata dinna.

Wakati Mary amekwenda washroom Prisca alinambia ana upwiru sana na sababu nakwenda Dodoma kukaa kwa muda mrefu atazidiwa hivyo tutafute means ya kupunguza muwashawasha wake.

Ofcourse niliona kutengeneza njia ya mtoto ni muhimu na mpaka akanambia nilijua tu lazima Prisca yuko kwenye hali mbaya maana ilikuwa ni week tayari na siku zimepita sijamgusa.

PRISCA: “Honey tunafanyaje sasa maana njia ya mtoto itaziba pia, tumuage da Mary afu tutamrudia.”

MIMI: “Mhh that is bad idea, dada yako ajue tumetoka kulana? Tumekuja wote afu tumuache alone sidhani kama ni sawa.”

PRISCA: “Sasa unampango gani?”

MIMI: “Nafikiri tubadili kiwanja twende pale 25 then tumuache Mary kwa muda afu mimi nitamwambia soon tunarudi.”

Baada ya Mary kurudi nilimwambia tunakwenda EB 25 na yeye aliunga mkono hoja na hao tukaanza safari ya kwenda Makonde. Baada ya kuwasili pale nilimwambia Mary ashuke atafute sehemu nzuri ya kukaa sisi tunarudi soon nayeye hakuwa na maswali.

Niliondoka na Prisca kwa kasi na tulikwenda Hotel moja ya karibu na maeneo yale. Hatukutaka kupoteza muda maana zoezi lililokuwa limetuleta ni kutengeneza njia ya mtoto, hivyo kazi ilianza.

Prisca na aina ya wale wanawake ambao wana ile high sex drive tena kipindi hiki cha ujauzito ni kama alikuwa too much yaani muda wote anataka dyudyu.

Tulitumia kama dakika 45 kutengeneza njia na baada ya hapo mimi nilitoka nje nikimsubiri atoke ili tuondoke, na muda huu Mary alipiga simu kuuliza tuko wapi na mimi ilibidi nimdanganye tu, nikamwambia tuko njiani tunarudi.

Baada ya kuwasili pale 25 Mary hakuwa na maswali yoyote japo aliishia kulalamika tumemwacha peke yake yale maeneo teba kwa muda mrefu. Tulishinda pale mpaka saa 7 usiku tukaondoka na kwa upande wao ilibidi warequest usafiri wa kuwarudisha nyumbani.

Asubuhi mapema tuliamka kujiandaa maana tulikuwa tunaondoka na ndege ya saa 5 asubuhi kwenda Dodoma. Tuliondoka na Junior lakini kutokana na mazingira mageni ilibidi dada aende nyumbani kwa wife (ukweni) mpaka tutakavyo rudi.

Tuliondoka saa2 asubuhi kuelekea Airport na nilirequest uber ya kutupeleka, na baada ya kuwasili JNIA Terminal 2 nilionana na Tyna na yeye ndo aliyenisaidia kukata tiketi. Tulipiga sana story wakati tukisubiri kucheck-in na muda ulivyofika tuliagana pale.

Baada ya kuwasili Dodoma tulikutana na Aggy ndo ambaye alikuja kutupokea pale Airport na tulipitia kwanza pale “Chako ni chako” tukapata lunch then tulipitia madukani kununua masweta kwaajili ya mtoto na sisi, si mnajua mazingira ya Dodoma ni baridi.

Baada ya kupata lunch tulikwenda mpaka Hotelin maeneo ya CBE ambapo tungekaa kwa kipindi chote ambacho tungekuwa Dodoma.

Aggy na wife walikuwa wanajuana hata Junior alikuwa anamjua ila alimuona akiwa mdogo bado. Aggy akijaga Dar kikazi lazima aje home na mara nyingi huwa analala kwangu ni kama ndugu kwa upande wangu.

Baada ya kuweka mabag tuliamua kwenda mpaka site Oysterbay na mimi nilikuwa nina hamu sana ya kuiona nyumba hata wife naye alikuwa anashauku sana.

Kwa upande mwingine mzee Mollel alikuwa na taarifa ya ujio wangu wa Dodoma hivyo alisema nikienda site nitawakuta mafundi wakiendelea na ujenzi na akasema jioni itabidi tuonane.

Baada ya kuwasili pale site kweli tuliwakuta mafundi wakichacharika kwa upande mwingine nyumba ilikuwa imeisha ndani na kila kitu kilikuwa tayari ni vitu vichache sana vilikuwa bado.

Mama Junior kwa upande wake alifurahi sana na hapo sasa aliamini kweli nilikuwa serious na ujenzi. Na yeye alisema anataka kufanya jambo atatengeneza bustani nje ya fense na atapanda maua na miti. Na pale kulikuwa na fundi anajenga ukuta wa tank waka fanya makubalino ya ujenzi wa bustani.

Kwa upande wa madirisha nilinunua kwa kutumia Pesa aliyokuwa amenipa Mzee Pama hivyo nilitafuta msumari nikasogea kwenye dirisha la seblen nikachonga tarehe ya kifo cha Pama kama kumbukumbu (X../VI/MMXXII). Na nilifanya hivi kwa madirisha yote ya seblen kwa nyumba zote 2 mpaka leo hii tarehe ipo ni kama memory kwangu.

Tulishinda pale mpaka jioni ya saa 11 na muda huu mipango ilikuwa kwenda kuonana na Mzee Mollel ili aijue na familia yangu.

Kwa upande mwingine Aggy aliniachia gari na akasema niitumie mpaka nitakavyo maliza ratiba zangu kwa Dodoma. Baada ya kuachana na Aggy pale CBE sisi tulikwenda mpaka nyumbani kwa Mzee Mollel na baada ya kuwasili pale tulikaribishwa ndani.

Mzee Mollel kama nilivyowaambia awali kwangu ni kama ndugu maana wametoka mbali sana na Mzee wangu. Baada ya utambulisho mzee Mollel alinipongeza sana kwakuwa na familia na muda huu alikuwa amemshika Junior.

Mama Junior naye hakuwa mbali aliungana na Mama Mollel Jikoni kwenda kupika na sisi tukabaki seblen tukiendelea na maongezi yetu.

Mzee Mollel alinipongeza sana na alisema mpaka sasa nyumba imekwisha na ilikuwa bado kuweka makabati ya jikoni, pervings pamoja na kuweka blundering. Pia kutokana na kuwa na eneo kubwa linalobakia alinishauri kwa upande wa juu nijenge chumba na sebule.

Kwa upande wangu niliona ni ushauri mzuri na nilimwambia tujenge kwanza msingi afu tutaendelea nikishakamilisha nyumba. Pia tulipiga hesabu ya vitu vilivyobaki ili kukamilisha ujenzi na ibaki kuhamia tu.

Kwa upande mwingine Mzee Mollel alinambia kuna kiwanja kinauzwa Ihumwa na kipo karibu na barabara na eneo kilipo ni kimezungukwa na makazi ya watu na ukubwa wake ni nusu heka. Mzee alitoa simu na kunionesha kile kiwanja na kweli kilionekana kuwa kizuri sana,

“Kiwanja ni kizuri sana ni vile mimi nina mambo mengi pia nimeshanunua viwanja vingi mpaka sasa ila ningekuwa na pesa hiki ningechukua.”

Mzee alinishauri kama niko vizuri nichukue kile kiwanja maana ni kikubwa afu mhusika alikuwa anakiuza kwa bei ya kutupwa sababu alikuwa na shida sana ya pesa.

Nilimwambia Mzee Mollel kesho ambayo ni Jumatatu tutakwenda kukiona na kama kitakuwa vizuri nitafikiria

“Kijana kama upo vizuri chukua hiki kiwanja Ihumwa ni eneo zuri sana badae kitakuwa asset kwako. Mwenye kiwanja anashida sana na hela kwa sasa na ameshusha bei ya kiwanja na bei yake ni 16million.”

Baada ya kupata dinna pale ya pamoja tuliaga tunaondoka na Mzee Mollel akasema kesho asubuhi atanipitia CBE ili twende kukiona kiwanja na sisi tulirudi hotelin kulala.

******

Jumatatu asubuhi niliamka mapema na tulikuwa tumeanza mwezi mpya wa August, sasa baada ya kupata breakfast tuliondoka kwenda Ihumwa na tulikutana na Mzee Mollel pale CBE.

Baada ya kuwasili eneo la tukio ukweli eneo lilikuwa ni zuri sana hata wife alivutiwa nalo maana halikuwa mbali na Dsm Road, na ukubwa wa kiwanja ni 1600sq (40x40) ni eneo kubwa sana.

Sikutaka kupoteza ile chance hivyo nikawaza nitumie ile pesa ya Muajemi kwenye kununua kile kiwanja, afu pesa ya kumalizia ujenzi ningekopa. Mzee Mollel alifanya mawasiliano na wahusika na ndani ya nusu saa walikuwa eneo la tukio na walikuja na hati ya kiwanja.

Kwa upande wangu nilikuwa namuamini sana Mzee Mollel maana alinitoa wasiwasi kabisa kuhusu kile kiwanja. Tuliita mashahidi pamoja na serikali za mtaa tukaandikishiana na baada ya hapo Mollel aliupeleka mtaba kwa mwanasheria ukagongwa mhuri.

Tulikubaliana million 15 na nilifanya malipo ya million 10 kwanza na balance tulikubaliana ndani ya mwezi ningekuwa nimeclear deni lote. Baada ya kulipia nilipewa hati ya nyumba ambapo tulikubaliana itakaa kwa Mzee Mollel na Jamaa alisema tutabadilisha jina pale ambapo nitamaliza deni.

Baada ya hapo nilirudi na mama Junior pale site na yeye alikuwa bado anaratiba zake za kupanda miti na maua na tulishinda pale mpaka jioni ndo tukarudi hotelini.

Kwa upande mwingine toka niwasili Dodoma sikuwahi kuwasiliana na Maggy na alikuwa hajui ujio wangu, hivyo niliona bora nimpe taarifa ili hata kesho tuonane na pia aijue familia yangu.

Baada ya kumpigia simu Maggy nilimpa taarifa niko Dodoma na alifurahi sana kusikia taarifa hizi hivyo tukakubaliana kesho jioni tungeonana.

Asubuhi ratiba zilikuwa ni zilezile kwenda site na good news hii siku mzee Mollel alinipa hesabu inayohitajika ili kumaliza ujenzi.

Mchana nilipigiwa simu na Mama kijacho na baada ya kupokea simu yake tulianza mazungumzo

“Nambie mama kijacho unaendeleaje ?”

“Safi tu mke mkubwa anaendeleaje? Na hujanambia unafanya nini huko.”

“Nikirudi nitakuambia maendeleo yako ni vipi?”

“Tumbo linauma sana honey.”

“Mtoto anakua tumboni ni kawaida hata mama Junior alikuwa analalamika kama wewe, ukiona maumivu yanazidi nenda hospital.”

“Sawa honey, I love you.”

“I love you too byee.”

Hii siku tuliwahi kutoka pale site na tulikwenda moja kwa moja mpaka hotelini naa usiku tulimpitia Aggy ili twende kupata Dinna pamoja pale Golden Fork.

Kwa upande mwingine Maggy alikuwa amewasili tayari muda mtefu na alikuwa ananisubiri.

Baada ya kuwasili maeneo yale na kuingia ndani Maggy aliniona na alinikimbilia akani-hug kwa furaha ni kama alikuwa haamini anayeniona ndo mimi Insider.

“Wow nimekumiss sana Insider.”

Na muda huu wife macho yote yalikuwa kwa Maggy ni kama aliona Maggy anaingilia code za watu.

Tulikwenda kukaa na muda huu Maggy macho yote yalikuwa kwa Junior,

MAGGY: “Insider huyu ni mtoto wako maana mmefanana sana.”

MIMI: “Macho yako hayadanganyi unachoona na huyu ni mke wangu mama watoto, dada hapa ni ndugu yangu anaitwa Aggy yeye anafanyia kazi taasisi X.”

Muda huu pia nilimtambulisha Maggy kama dada yangu wa karibu sana.

MAGGY: “Insider hukuwai nambia kama una mke na mtoto ila hongera sana.”

MIMI: “Ahsante nilipanga siku nitakusaprise kama leo hivi na nimekufuata Dodoma.”

MAGGY: “Ndugu zangu nimefurahi sana kuwafahamu, nipe Junior nimshike,….Insider mna agenda gani huku Dodoma maana mpaka umekuja na familia sio jambo dogo.”

MIMI: “Usijali tukimaliza kula tutaongea kwa nafasi.”

Baada ya kupata dinna tulikaa sehemu nyingine na Maggy na tukaanza maongezi pale, ilibidi nimwambie Maggy ukweli kuwa kilichonileta ni suala la ujenzi.

MAGGY: “Insider hongera sana na umejengea wapi?”

MIMI: “Makulu huko na nyumba ni ya kupangisha ikiisha nitakuambia ili na wewe uwe mteja wangu. Mpaka September kila kitu kitakuwa sawa kwa wapangaji kuingia.”

MAGGY: “Insider ikiisha nambie ili nihamie niwe mteja wako, nimepata nyumba mbaya na bado mshahara hawajaingiza mpaka sasa.”

MIMI: “Aisee pole sana na pia unaonekana kufubaa, Dodoma imekukataa mama vipi upo sawa lakini? Seem like you’re not.”

MAGGY: “Acha tu Insider nimefulia hatari kwasasa maana nimetumia akiba zote kulipia kodi na kununua vitu.”

MIMI: “Seems like unataka mkopo kwangu.”

MAGGY: “Hahahahaa naogopa hata kukupiga mzinga maana umekuja kwaajili ya ujenzi najua umetoboka sana.”

MIMI: “Kwako wewe usiwe na wasiwasi nambie unahitaji kiasi gani? Maana wewe ni ndugu yangu.”

MAGGY: “Nikipata laki5 nitakuwa niko pazuri sana kwakweli kwenye kipindi hiki cha mpito.”

MIMI: “Sawa hio usijali nitakupa ukikaa sawa utanirejeshea.”

Maggy alifurahi sana hii siku na tuliagana pale maana alisema asubuhi atawahi kuamka sababu ya kikao hivyo aliwaaga akina Mama J na nilimsindikiza mpaka nje akaondoka.

Baada ya kuachana na Maggy muda huu Iryn alipiga video call na baada ya kupokea tulianza story pale. Iryn alinambia kesho ambayo Jumatano anarudi Tanzania hivyo nikampokee na mimi nilimwambia niko Dodoma.

IRYN: “Insider huko Dodoma una b*tch maana hunaga sababu ya msingi.”

Na mimi nilisogea mpaka kwa wife na akawa anatuona pale.

MIMI: “Huyu ndo b*tch wangu unayemwongelea sema lingine dada.”

IRYN: “Wow kumbe upo na wifi yangu, guys mna agenda gani huko Dodoma?”

WIFE: “Nimekuja kutambulishwa mpenzi si unajua ndoa soon.”

IRYN: “Safi sana na mimi nataka mwaka huu mfunge ndoa nitalipia gharama zote za harusi.”

MIMI: “Acha uchawi wako harusi mapema hivi?”

Tulipiga sana story na Iryn muda huu na alionekana kuwa na furaha sana usiku huu na alisema nikirudi nimjulishe tuonane.

Tuliendelea kukaa pale mpaka saa 4 usiku ndo tuliamua kuondoka kurudi kulala kwa upande mwingine nilimwambia mama Junior kesho asubuhi tutakwenda Kondoa kumsalimia mamdogo wangu pamoja na kumtambulisha.

Ile asubuhi baada ya kupata breakfast tulianza safari ya kwenda Kondoa na hii siku mamdogo hakwenda kazini kwaajili yetu.

Baada ya kuwasili Kondoa mamdogo alikuwa yuko barabarani tayari kutupokea na tuliondoka moja kwa moja mpaka nyumbani kwake.

Hii ilikuwa ndo mara ya kwanza mamdogo kuwaona live wife na Junior maana alikuwaga anaishia kuwaona kwenye picha tu. Na mimi niliishia kufanya utambulisho kwa wote pale na mamdogo alifurahi sana.

Baada ya maongezi kidogo niliwaacha seblen wakiendelea kufahamiana na mimi nilitoka nje kupiga simu maana wakati tuko njiani nilipigiwa simu na Mary kutokana na mazingira sikupokea simu zake.

Nilifanya mawasiliano na Mary na alinambia wako hospital kwani Prisca analalamika sana tumbo lina uma. Ilibidi niulize maendeleo yake na Mary alinambia yuko salama kabisa hakuna shida yoyote niwe na amani.

Tulishinda na mamdogo pale kwake mpaka jioni ndo tuliaga na kuanza safari ya kurudi Dodoma. Lakini tukiwa njiani kurudi Dodoma Roho yangu ilikuwa inauma sana kwani kuna ndoto niliiota nikiwa na Prisca lakini sikujua ilikuwa inamaanisha nini na muda huu nilikuwa naifikiria sana.

Wakati tuko njiani tulipanga na wife kwa kesho tutakwenda kufanya usafi wa nyumba ndani na nje pamoja na kupanda miti mingine afu ijumaa tungerudi Dar.

Baada ya kuwasili Dodoma ilikuwa ni usiku tayari hivyo nilikwenda kuoga na niliishia kulala pale kitandani maana nilikuwa nauchovu sana hii siku.

Usiku mida ya saa 6 simu yangu ilianza kuita na nilishtuka muda huu na ile kucheki alikuwa ni Mary na mimi nilitoka room kwenda koridoni kupokea simu yake.

Baada ya kupokea simu muda huu Mary alinipa taarifa mbaya sana na nilijikuta nikianza kuishiwa nguvu pale, maana zilikuwa ni habari mbaya sana kwa upande wangu.

TUTAENDELEA

Kusema ukwel mim sio mpenz wa kureply story ila katika hii story mtu ninae mkubali kuliko wote ni prisca sasa kama kafariki ntahuzunika sana kwakweli
 
Hii story siipendi natoa sababu.
1.unataka tujue umepiga hatua sijui unawatu wakubwa sijui wa njee yaani kuna vitu vinaonyesha unajionyesha au upo kwenye matangazo,either ya kibiashara au yakinini. Yaani haupo real kuhadithia story ya huyu demu ,jingine kwenye hii story lazima ujue hili haihiitaji utuanzie undani wa maisha yako sana ingekuwa imeisha unatoa na prove yanini siuende kwenye point ya huyo msichana na baadhi ya vitu vyako vya muhimu pale mwanzo ni sawa katikati ulipoanza kujielezea undani wa biashara basi hujanivutia tena inaboa

Mi nakushauri usiifuatilie wala kuisoma
Achana nayo tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom