JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.51.
ILIPOISHIA;
Katika kutembeza macho aliwaona wajukuu wa mzee Njiwa wakicheza nje ya uzio, aliona kama atamuua mmoja basi mzee Njiwa Manga ataacha kazi ya kuwatibu ili ashughulikie msiba na kuwafanya Ashura na mwanaume wake kuondoka ili warudi siku nyingine. SASA ENDELEA...
Aliamini kama watatoka bila kupatiwa kinga yoyote angetumia nafasi ile kuwamaliza wote ili aweze kuishi na Muddy bila tatizo japo alijuwa kwa upande wa baba yake kulikuwa na vita nyingine.
Kila alivyotaka kuteremka roho ilimkataza kwa kuwaonea huruma viumbe wasio na hatia.
Kutokana na uwezo wake aliweza kuyasikia yote yaliyokuwa yakizungumzwa ndani na kupanga kama atakubaliana nao kabla ya kuwapa kinga naye, hatakuwa na budi kuua mtoto mmoja.
Ashura na mwanaume wake waliingia katika chumba cha mzee Njiwa Manga na kukaa kwenye mkeka.
Karibuni, mzee Njiwa Manga aliwakaribisha.
Asante, walijibu kwa pamoja.
Mh! Niwasaidie nini?
Mzee tunahitaji msaada wako, tuna vita nzito na mwanamke mmoja jini.
Mmejuaje ni jini wakati majini hayaonekani?
Anatutokea katika umbile la kibinadamu na wakati mwingine katika maumbile tofauti, pia tunatokewa na mambo ya kutisha.
Tena jana kamuua mganga mmoja Mbagala kifo cha kutisha, Ashura aliongezea.
Mmh! Majina yenu? Aliwauliza huku akichukua kibao cheusi na chaki.
Naitwa Shuuna.
Shuuna... mganga alilirudia jina lile kwa sauti ya chini huku akiliandika kwenye kibao.
Mbona unaonekana una majina mengi? Mganga Njiwa Manga alimuuliza Ashura.
Lakini hili ndilo langu la kuzaliwa.
Sasa nikusaidie kwa jina gani kwani yote uliyatumia na watu tofauti wanakujua kwa majina hayo?
Kwa sasa natumia jina hili.
Kama ukifanikiwa kurudi kwa Muddy utatumia jina gani?
Swali lile lilimfanya Ashura akae kimya na kukosa la kujibu kwa kuona kama siri yake inatoka nje.
Lakini mzee suala la Muddy tulishaachana nalo, kama kutusaidia msaidie kwa jina la Shuuna, Tonny aliingilia kati mazungumzo.
Najua mmekuja pamoja lakini kila mmoja ana mawazo yake ambayo sitaki kuyaingilia kwa vile siyo kazi yangu, mzee Njiwa Manga alijibu kwa fumbo lililomuacha gizani Tonny bila kujua dhamira ya Ashura kwa Muddy ilikuwa nini.
Naomba niachane na mwenzako kwanza, hebu nawe nieleze jina lako?
Naitwa Antony.
Antoniii, alilirudia jina lile kwa sauti ya chini huku akiliandika kwenye ubao.
Baada ya kuandika alitulia kwa muda akiandika vitu kwenye ubao na kukohoa kidogo kisha akauliza:
Nimeona yote, sasa shida yenu nini hasa?
Mzee kama tulivyokueleza kuwa tuna tishio la mwanamke mmoja ambaye ni jini, anatishia maisha yetu.
Kwa hiyo mnataka nini?
Tunataka utukinge ili tuweze kupambana naye.
Mnamjua jina lake?
Balkis, Ashura alijibu.
Mganga aliliandika jina lile, kama kawaida alilirudia kwa sauti ya chini.
Balkis...Balkis.
Baada ya kutulia kwa muda alisema:
Lakini mbona mimi sioni madhara ya huyu mnayemuogopa?
Mzee huyu ni mtu mbaya sana, amenitokea mara nyingi kwenye gari katika sura tofauti na kutishia maisha yetu, Ashura alisema huku macho yamemtoka pima kwa kusistiza.
Mbona hapa panaonesha jini huyo ni mpole sana kuliko majini wengine?
Si kweli, ana roho mbaya sana, amemuua mzee Chujio kifo kibaya sana, Ashura alisema.
Unajua sababu ya kuuawa mzee Chujio? mganga aliuliza.
Kutokana na maelezo ya huyo mwanamke jini anasema aliingilia kazi yake na kuwa mbishi ndio akaamua kumfanya vile.
Sasa hamuoni na mimi nikiingilia kazi si yangu anaweza kunifanya kama mzee Chujio?
Hawezi.
Kwa nini asiweze?
Tunasikia wewe ndio kiboko ya majini.
Ni kweli kazi yangu ni kutibu na si kushindana na majini.
Lakini mzee kazi yako si kutusikiliza wateja shida yetu na kukupa kiasi ukitakacho, Tonny alimueleza mganga..
Sikiliza kijana, mimi si mchawi ni mganga wa kuwasaidia wenye matatizo, ndiyo maana nipo mpaka leo.Waganga wengi wamepoteza sifa zao kutokana na kuingilia kazi ya wachawi.
Tumekuwa tukifanya makosa ya kuingia kwenye kazi ya kutesa, kuua au kuingia kwenye vita na viumbe kama majini ambayo wakati mwingine huwa hayana matatizo na watu.
Sasa mzee utatusaidiaje?
Mpaka sasa sijajua shida yenu nini?
Tunataka kinga ili tusiweze kudhuriwa na jini.
Jini gani wa kuwadhuru ninyi?
Balkis, Ashura alijibu.
Balkis atawadhuru vipi bila ninyi kumchokoza?
Yule hana cha kumchokoza bali huamua kuua bila sababu, Ashura alitengeneza uongo.
Sitawapa dawa yoyote zaidi ya kauli ya Balkis mwenyewe.
Mbona hatukuelewi, kauli gani?
Mtaisikia muda si mrefu kutoka kwake Balkis.
Mzee Njiwa alitoka nje na kurudi na kitezo chenye moto, akakiweka mbele yake, akatoa mavumba kwenye chupa kisha akasema:
Hii dawa kazi yake kuyavuta majini mazuri, kama Balkis ni jini mbaya hatakuja nikimwita.
Baada ya kusema vile alianza kuweka mavumba kwenye moto huku akisema:
Balkis binti mfalme wa bahari, naamini wewe ni jini mwema nakuomba uje mbele yangu, lakini kama si jini mwema ukiingia himaya yangu ndiyo mauti yako...Balkis njoo mbele ya wanadamu hawa wana mashtaka juu yako.
Je, Balkis ni jini mzuri au mbaya?
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.52.
Nimewaonesha ishara nyingi za vitisho ili wajue mimi si kiumbe wa kawaida ili wachane na mimi, lakini wamekuwa wabishi, kabla ya kuja huku niliwapa onyo zito lakini wamekuwa kama kenge, hawasikii mpaka watoke damu masikioni.
Tena wana bahati kubwa leo ningepata dhambi nyingine, wakati natoka nyumbani niliwaona wamekaribia kwako lakini kasi yangu ilichelewa kidogo na kuwakuta wameshaingia kwenye ngome yako.
La sivyo kama ningefanikiwa kuwatia mikononi ningewaulia mlangoni kwako na kama ungewasikiliza na kuwapatia tiba kabla tiba yao haijatimia ningemuua mjukuu wako mmoja ili uhalalishe kazi hii na wangetoka ningewamalizia mbali,
Balkis alisema kwa sauti isiyotaka mzaha, huku kauli yake ikizidi kuwatisha moyoni walioomba msaada wa mzee Njiwa Manga.
Nimekuelewa sana Balkis binti wa mfalme Barami, sasa ulikuwa unataka nini?
Kama nilivyowaeleza waachane na mimi, waendelee na maisha yao.
Wakifanya hivyo utakuwa na vita nao?
Niwe nao ili iwe nini ikiwa kila mmoja na maisha yake, ila tofauti ya hapo nitakachokifanya Mungu anajua.
Nina imani mmesikia yote aliyosema Balkis, niliwaeleza ni mpole mwenye huruma na upendo kwa viumbe wenzake.
Napenda kuwaeleza kuwa maelezo yake ndiyo tiba yenu na mkitoka hapa mkienda kinyume na haya aliyosema, nisione mtu hapa, mtamalizana wenyewe, mmenisikia?
Alijibu kwa kunyanyua vichwa kwani hata midomo ilikuwa mizito, baada ya majibu yao ya kibubu mzee Njiwa Manga alimgeukia Balkis.
Nina imani wamekuelewa ila wakienda kinyume mimi simo.
Wewe unasema hivyo lakini mioyo yao imejaa tamaa ya mali na uhai wa watu, narudia tena sitawaua ila nitawaadhiri mbele za watu, hilo litakuwa pigo kubwa na mkizidi nitawageuza mbwa.
Nimekuelewa sana Balkis unaweza kwenda, mzee Njiwa Manga alisema.
Baada ya kuruhusiwa kutoka alinyanyuka na kutoka chumbani katika umbile la kibinadamu, wote walimsindikiza kwa macho hadi nje.
Waliokuwa wamekaa nje kusubiri huduma macho yao yalishuhudia mwanamke mzuri akipita mbele yao huku wakijiuliza amepita saa ngapi kutokana na watu wengine kuwepo kwa muda mrefu. Balkis baada ya kutoka katika uzio wenye nguvu wa mzee Njiwa Manga alitoweka.
Baada ya kuondoka Balkis, mzee Njiwa Manga aliwageukia wateja wake na kusema:
Nina imani tatizo lenu limekwisha?
Mzee litakwisha vipi wakati umemsikia mwenyewe amesema nini, Tonny alihoji.
Kasema nini?
Si amesema tukifuatilia mambo yake atatugeuza mbwa, Ashura alijibu.
Sasa mnataka kufuatilia mambo yake?
Hapana.
Sasa tatizo nini?
Tulikuwa tunaomba kinga. Tonny alisema.
Ya nini?
Ili tujikinge na matatizo ya wanadamu na majini.
Ili?
Mzee kama hujui kazi yako, kwani wanadamu wanakuja kwako kutafuta nini?
Tiba ya matatizo yao.
Sasa mbona hutaki kutusaidia?
Kwani shida yenu iliyowaleta hapa ni nini?
Kuzuia nguvu za jini Balkis.
Sasa niwape kinga ya nini?
Anaweza kutugeuka na kutufanyia kitu kibaya.
Hawezi na sina tiba yoyote labda muwe na tatizo lingine.
Hatuna, ni hili hili la huyu mwanamke ndilo linalotutisha, unamuona kwa macho tu lakini ni kiumbe kibaya sana.
Yule hana ubaya kama nilivyowaeleza, lakini mioyoni mwenu mna dhamira mbaya naye, kwa hilo mimi halinihusu kama mnataka ushindani dawa hiyo sina.
Kwa hiyo huna msaada wowote kwetu? Tonny aliuliza.
Msaada niliowapa ni mkubwa kuliko kukuchanjeni au niwape dawa ya kufukiza.
Mzee msaada gani uliotupa zaidi ya kutuacha njia panda? Tonny alizidi kuhoji.
Msaada niliowapa hamuujui lakini ni mkubwa sana, najua mmezunguka kwa waganga wengi kwa kazi zenu za dhuluma. Hamkuwahi kukutana na tatizo kisha mkatibiwa bila kunywa, kujifusha au kuchanjwa dawa? Mliyekuwa mnamuona adui ameeleza hataki kitu gani, sasa mnataka nifanye nini?
Basi inatosha inawezekana na wewe umemuogopa, Tonny alisema kuonesha alitaka zaidi ya yale aliyoelezwa.
Kweli nimemuogopa nipo kwa ajili ya kutibu si kujiingiza kwenye matatizo ya kujitakia, kutokana na maelezo yake nilikuwa nampoteza mjukuu wangu kwa ajili yetu. Nawaeleza mkikosea kwenda kwa mganga mwingine kitakachowakuta hamtakisahau mpaka mnakufa.
Tumeelewa. Tonny alijibu kwa shingo upande.
Basi mnaweza kwenda ili niendelee na wenzenu.
Sasa mzee tukupe kiasi gani?
Nina imani hamkuona nilichokifanya, nendeni msitoe kitu chochote.
Hapana mzee hata ya kuangalizia, sijui elfu moja?
Hapana nimewasamehe kila kitu.
Walitoka huku wakiamini mzee Njiwa Manga uwezo wa kutibu umepungua ndiyo sababu ya kushindwa kuwasaidia kupambana na Balkis.
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.53.
Sauda, walisema mashoga zake waliokuwa wakilia huku mikono ikiwa kichwani, wengine hata nguo ziliwaanguka bila kujua.
Sauda kafanya nini?
Ame...
Amefanya nini mbona mnanichanganya, mke wangu kafanya nini jamani? mganga alijikuta kwenye mtihani mzito wa kujua mkewe amefanya nini kwani muda mfupi uliopita alimtuma dukani.
Mara aliingia mwanamke mwingine aliyekuwa akilia huku akisema:
Haiwezekani Sauda atutoke kirahisi namna hii.
Huu lazima uchawi haiwezekani njiwa amgonge afe, mwingine alisema huku akijitupa chini kwa uchungu.
Jamani mke wangu kafanya nini? pamoja na kuwasikia wakisema lakini hakuwaelewa.
Mara watu waliingia na mwili wa mkewe ambaye alikuwa amekwishapoteza uhai.
\Ha! Amefanya nini? Kakakuona alitaharuki.
Alimvamia mkewe ambaye alikuwa amefunikwa kanga, akamfunua na kumwinamia! Hakuamini alichokiona mbele yake.
Sauda mke wangu umepatwa na nini? Kwa nini nilikutuma kwenda kuchukua dawa? Kwa nini nilikuwa na wazo baya? Maskini mke wangu nimekuponza, ulikuwa ukizungumza na wanawake wenzako, ona sasa umebadilika jina na kuitwa marehemu! Nini faida ya kazi yangu? Mganga alilia kama mtoto mdogo huku akimgeuza mkewe ambaye alikuwa ameanza kupoa.
Ashura na mwanaume wake nao walikuwa wametoka na kushuhudia tukio lile. Balkis naye hakuwa mbali, moyo ulimuuma kwa kitendo chake cha kuyachukua maisha ya kiumbe kisicho na hatia.
Machozi ya damu yalimtoka.
Kila mganga alipokuwa anamlilia mkewe kwa maneno ya uchungu na yeye ndivyo alivyokuwa akiumia na kulia zaidi.
Ashura alipoangalia pembeni alishtuka baada ya kumuona Balkis akiwa katika kundi la watu huku naye machozi yakimtoka. Baada ya kumuona alipatwa na mshtuko mkubwa, akaanguka na kupoteza fahamu. Hali ile iliwatisha watu wote waliokuwa pale.
Mganga alimwacha mkewe na kukimbilia ndani kuchukua dawa ya unga kwa ajili ya kuzuia nguvu zozote mbaya.
Aliimwaga hewani lakini Balkis aliwahi kuondoka eneo lile na kwenda kukaa njiani kuwasubiri Ashura na mwanaume wake. Mganga baada ya kufanya vile bado hakuamini, aliuchukua mwili wa mkewe na kuuingiza ndani kujaribu tiba zote anazozijua akiamini atafanikiwa kumrudisha mkewe.
Alikuwa amesahau kuwa hakuna mtu wala kiumbe chochote dunia chenye uwezo wa kurudisha roho ya mtu au kiumbe zaidi ya Muumba peke yake.
Licha ya kuhangaika zaidi ya saa nzima kurudisha roho ya mkewe iliyopotea, bado hakufanikiwa.
Hatimaye alikubaliana na ukweli kwamba mkewe amefariki.
Ilibidi atoe taarifa za kifo cha mkewe kwa ndugu na jamaa, mipango ya mazishi ikaanza. Kutokana na kuchanganyikiwa na kifo cha mkewe alisahau hata kama kuna wateja aliokuwa akiwashughulikia.
Ashura baada ya kupata nafuu alijikuta akichanganyikiwa kwa kuamini kabisa kifo cha mke wa mganga kimefanywa na Balkis. Wasiwasi ulizidi kumpanda na kujiuliza kama ni yeye basi hata maisha yao yalikuwa hatarini.
Tonny nimemuona Balkis?
Wapi?
Alikuwa kwenye kundi la watu.
Mwongo!
Kweli! Tena alikuwa analia machozi ya damu.
Mungu wangu! Unataka kuniambia aliyefanya haya ni yeye?
Inawezekana kabisa, si unakumbuka kauli aliyotoa kwa mzee Njiwa Manga kuwa kama angetusaidia angemuua mjukuu wake.
Sasa unafikiria anaweza kutufanyia kitu kibaya?
Hata mimi nimechanganyikiwa.
Sasa mganga atatusaidia nini? Tonny aliuliza huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi.
Wee! Tena nyamaza, inavyonekana sisi ndiyo chanzo cha kifo cha mkewe.
Kwa hiyo unaniambia nini?
Tuondoke, ikiwezekana tusirudi tena na Balkis tuachane naye, Ashura alisema huku akitetemeka.
Wakati huo watu walizidi kusogea eneo la tukio, kila mtu alikuwa akisema lake juu ya kifo cha ghafla cha mke wa Kakakuona.
Wapo walioelezea jinsi walivyomuona njiwa yule akimpiga kichwani mke wa mganga na kutoweka kisha kuanguka chini na kupoteza uhai.
Kweli kabisa Balkis ndiye aliyemuua mke wa Kakakuona, Tonny alipata uhakika.
Sasa unaona tumechokoza nyuki wakati hatuna mbio.
Sijui tufanye nini ili Balkis atuelewe?
Nimekueleza tuachane naye.
Atatuelewa?
Mmh! Kazi ipo, kama amejua tunataka kumuua unafikiri atatufanya nini? Ashura alisema kwa sauti ya kukata tamaa.
Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, kwa nini tusiendelee kuwa hapa ili mganga atupe hata kinga ili asitudhuru?
Tonny hebu kuwa na akili, umesikia aliyefanya vile ni Balkis mganga atatufanya nini, hiyo milioni mbili yako itarudisha roho ya mkewe?
Mmh! Na kweli, kwa hiyo unasemaje?
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.55.
LIPOISHIA Jumamosi
Nilikuwa na mambo yangu binafsi wala hayahusiani kabisa na majini, Ashura alipindisha kwa kuamini mwanaume wake akijua kuwa alifuata dawa ya kurudiana na Muddy angekasirika.
SASA ENDELEA...
Ashura alikuwa na siri nzito moyoni mwake kama angefanikiwa kurudiana na Muddy, mwanaume aliyeamini kuwa bila ya mipango yao ya utapeli alikuwa ndiye sahihi kwake. Mpango wake ulikuwa kumuua mwanaume wake kwa kumuwekea sumu kwenye chakula ili aishi na Muddy katika maisha ya ndoa.
Kama nilivyokueleza kabla ya kujua kuwa yule mwanamke ni jini, nilikwenda kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kumuingia na kuweza kuchukua mali yake.
Lakini ilionesha si kiumbe wa kawaida na kama ulivyosikia, mzee Chujio alizidiwa nguvu na yule mwanamke. Lakini kwa mzee Njiwa Manga kutokana na historia ya watu hajawahi kushindwa suala la majini.
Tonny mbona hatuelewani nani ana majini mpaka twende kwa mzee Njiwa Manga?
Kumbuka tunataka mali ya Muddy na mkewe ambaye ni jini, huoni tunahitaji msaada wa mtu mwenye uwezo wa kupambana na majini.
Mmh! Kama ana uwezo huo kuna umuhimu wa kwenda kwake.
Hakuna njia nyingine kwa mambo niliyoyaona yamenitisha bila hivyo tunaweza kupotea.
Walikubaliana kwenda siku iliyofuta kwa mganga Njiwa Manga ili kutafuta uwezo wa kupambana na Balkis.
****
Siku ya pili Ashura na mwanaume wake walikwenda Bagamoyo kwa mganga Njiwa Manga, kwa vile Tonny alikuwa hajakwenda kipindi kirefu, ilibidi aulizie sehemu anayoishi. Alielekezwa na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa mganga huyo, walipofika walikuta magari aina tofauti zaidi ya kumi kuonesha kuwa siku ile kulikuwa na wateja wengi.
Ilibidi wakae kwenye benchi kusubiri kwa muda mbele yao kulikuwa na wagonjwa zaidi ya ishirini, walijumuika pamoja na kusubiri tiba. Wingi wa watu ulitaka kuwakatisha tamaa na kutaka kuondoka.
Tonny kwa nini tusiondoke turudi kesho mapema, huoni tutachelewa kutoka? Ashura alimwambia mwanaume wake.
Kwani tunawahi nini? Kwa vile tumeishafika hata usiku tutarudi, nataka nikueleze ukweli pamoja na kujionesha siogopi kitu, lakini siri niliyokuwa nayo moyoni ni Mungu tu anajua.
Kama yale maajabu yangerudia basi ningekufa kwa hofu.
Nilikuona ulikuwa mwenye hofu kubwa na niliyasikia mapigo yako ya moyo yakikimbia kama gari lililokatika breki na kunifanya nisimame kidete, alisema Tonny.
Mmh! Wee acha tu, kama angezidisha ningekufa, yaani maneno yako yalinitia nguvu ya ajabu. Kwa kweli nimeanza kuwa muoga wa kila kitu hata upepo sasa hivi ukivuma naogopa najua amekuja, alijibu Ashura.
Wee acha, baada ya kugundua yule mwanamke ni jini niliishiwa nguvu na kuamini simuwezi kwa lolote zaidi ya kutumia nguvu za ziada kuja hapa kwa mzee Njiwa Manga ndipo penye ufumbuzi bila hivyo tutaumia, alisisitiza Tonny.
Kwa hilo hata tukikaa siku mbili sioni tatizo, sasa hivi namuogopa yule mwanamke kama kifo, alimalizia Ashura.
Wakati wakibadilishana maneno hayo, Balkis hakuwa mbali na nyumba ya mzee Njiwa Manga, wakati alipokuwa akitoka kwa wazazi wake chini ya bahari aliwaona Ashura na mwanaume wake wakikaribia kuingia kwa mganga Njiwa Manga. Alijitahidi kuwawahi wasiingie, kasi yake iliishia nje ya uzio wa nyumba ya mganga huyo.
Alijipiga chini kwa hasira na kusababisha patokee mtikisiko mdogo uliowashtua watu, hakutaka kukubali kushindwa, alijigeuza njiwa na kwenda kwenye mti mrefu uliokuwa pembeni ya nyumba ya mganga Njiwa Manga.
Aliweza kuwaona wateja wa mganga huyo akiwemo Ashura na mwanaume wake, lakini nguvu za dawa za mzee Njiwa Manga zilimzuia asiweze kufanya lolote.
Akiwa na hasira alipanga kuwasubiri na kuwatia adabu baada ya kuonesha kiburi. Wasiwasi wake ulikuwa kwenye nguvu za yule mzee zingeweza kummaliza na kudhurumiwa mpenzi wake.
Kwa upande wa mali yake aliamini hakuwepo wa kuichukua kwa vile ilikuwa ndani ya uwezo wake.
Katika vitu alivyovipanga maishani mwake vilikuwa ni kubeba mimba ya Muddy kuwafanya wazazi wake hasa baba yake asiwe na nguvu ya kumlazimisha kuolewa na jini mwenzake.
Alijua kama Ashura akifanikiwa kupata kinga ya kumdhibiti, lazima atamnyanganya mume wake na kumlazimisha kuendelea kufanya kazi asiyoipenda ya kuchukua vizazi vya wanawake.
Akiwa juu ya tawi la mti akichanganyika na ndege wengine, moyo ulimuuma na kujiuliza amfanye nini mganga ili asiwape uwezo wa kudhulumu haki yake. Alijikuta akiwachukia baadhi ya binadamu ambao aliamini kabisa hawakutakiwa kuhurumiwa zaidi ya kuuawa japo siku zote roho yake haikupenda kufanya vile.
Akiwa anawatazama wateja waliokuwa wakienda kupata tiba kwa mzee Njiwa Manga, aliwaona Ashura na mwanaume wake wakinyanyuka na kwenda kuonana na mganga huyo. Alijikuta akipandwa na hasira lakini eneo lile lilikuwa lina nguvu za ajabu zisizowezesha nguvu za kichawi na kijini kuingia katika himaya yake.
Alipotazama huku na kule, aliwaona wajukuu wa mganga wa Njiwa Manga wakicheza, akaamua kumuua mmoja.
Kwanini Balkis alitaka kumuua mjukuu mmoja wa mganga Njiwa Manga?
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.57.
ILIPOISHIA:
Mzee Njiwa alitoka nje na kurudi na kitezo chenye moto na kukiweka mbele yake, alitoa mavumba kwenye chupa na kusema:
Hii dawa kazi yake kuyavuta majini mazuri, kama Balkis ni jini mbaya hatakuja nikimwita.
Baada ya kusema vile alianza kuweka mavumba kwenye moto huku akisema:
Balkis binti mfalme wa bahari, naamini wewe ni jini mwema nakuomba uje mbele yangu, lakini kama si jini mwema ukiingia himaya yangu ndiyo mauti yako...Balkis njoo mbele ya wanadamu hawa wana mashtaka juu yako.
SASA ENDELEA ...
Moshi ulikuwa mwingi kiasi cha kujaa chumbani, baada ya muda upepo mkali ulianza kuvuma na kusababisha baadhi ya vitu kutaka kupeperuka lakini mzee Njiwa Manga aliutuliza kwa kusema:
Najua una hasira lakini naomba uwe mpole kama ulivyo, wewe ni mpole tena mwenye upendo kwa wanadamu.
Upepo ulitulia taratibu wakati huo Balkis akiwa katika umbile la njiwa alijikuta akizidiwa na nguvu na kudondoka toka juu ya mnazi na kujikuta akijitahidi asianguke na kuingia kwenye dirisha la chumba cha uganga cha mzee Njiwa Manga.
Alitua pembeni ya mzee Njiwa Manga, Ashura na mwanaume wake walishtuka kumuona njiwa mzuri sana mwenye rangi nyeupe aliyepakwa wanja mwekundu uliozunguka katika macho yake.
Manyoya yake yalikuwa kama ya plasitiki iliyokuwa ikimelemeta.
Karibu Balkis kwa mzee Njiwa Manga.
Balkis katika umbile la njiwa hakujibu kitu alitulia akiwatizama Ashura na mwanaume wake. Mzee Njiwa Manga alisema:Najua hukupenda muda huu kuwa hapa, lakini nimekuita kwa nia njema kwa vile wewe ni jini mwema mwenye upendo kwa wanadamu. Nakuomba uwe kwenye umbile tunaloweza kuzungumza kibinaadamu.
Baada ya kusema vile kilipita kiza cha ajabu na baada ya muda ilirudi hali ya kawaida. Sehemu aliyokuwa njiwa alikuwepo Balkis katika umbile la kibinaadamu.
Ashura na mwanaume wake kidogo wakimbie kwa hofu.Msihofu, kama nilivyowaeleza kwa dawa niliyoichoma ni jini mwema tu anayeweza kuingia katika himaya yangu. Balkis asalam aleykumu.
Waaleiykum msalaam, alijibu kwa sauti tamu.
Karibu.
Asante.
Balkis aligeuza uso wake na macho yake yaligeuka rangi na kutoa machozi ya damu, kitu kilichozidi kuwatisha Ashura na mwanaume wake.
Hapana Balkis huna sifa hiyo wewe ni mpole nimekuita hapa kwa makusudi ya kuwaeleza hawa wanadamu ubaya wao mbele yako. Mganga Njiwa Manga alisema huku akimshika kichwani na kumpigapiga taratibu kumpunguza hasira. Balkis alitikisa kichwa kuonesha amekubali.
Balkis.Abee.
Nataka uniambie unataka nini wafanye hawa wanadamu wajue wewe si adui yao?Wanajua wenyewe, nilizungumza nao nini, Balkis alijibu kwa sauti tamu kama kinanda.
Naomba unieleze mbele yao.
Nikisema mimi nitaonekana muongo, napenda waseme kwa vinywa vyao.
Eti mlizungumza nini na Balkis? mzee Njiwa Manga aliwageukia na kuwauliza.
A...ali...nikataza nisimfuate mume wake ambaye ni mtalaka wangu, Ashura alijibu katika hofu kubwa.
Na kingine?
Tusimfuatilie maisha yake.
Mmefanya yote aliyowaeleza?
Wote walibakia kimya wakitazama chini, mganga alimgeukia Balkis na kumuuliza.
Wewe umeona nini?
Hawa walio mbele yako ni viumbe wabaya kuliko hata nyoka, wamepoteza maisha ya wanaume zaidi ya wanne na Muddy kama nisingemuwahi alikuwa wa tano. Wamekuwa na tabia za kuwatafuta wanaume na huyu mwanamke kujifanya anawapenda sana, kisha anajitambulisha kwa majina tofauti.
Kila mwanaume anamfahamu kwa jina tofauti kama waliokufa kwa ajili yao wakisimamishwa mbele yake watamtaja kwa majina tofauti, Muddy anamtambua kwa jina la Ashura lakini wengine walimtambua kwa majini ya Fatuma, Hilki, Masha.
Lakini jina lake halisi ni Shuuna, kwa utaalamu wako nina imani majina hayo yote umeyaona alipojitambulisha kwako na kujua sababu ya majina hayo?
Ndiyo, Mzee Njiwa Manga alijibu kwa sauti ya chini.
Hawa si viumbe wa kuonewa huruma hata mara moja, hebu angalia kila kukicha wamekuwa wakipanga mipango ya kudhulumu mali za watu na kuwatoa roho zao bila hatia kwa kigezo cha uzuri wa Shuuna. Hivi mimi na yeye nani mzuri?
Balkis alinyanyuka na kujigeuza pande zote kuonesha ufundi wa Maulana kumuumba katika umbile la uzani.
Ni wewe Balkis mwana wa mfalme wa chini ya bahari.
Mbona siui watu kama ninyi? Mtauliza kwa nini nilimuua mganga Chujio, kiburi chake kilimponza. Nilijua mtakwenda kule na kutaka kinga ya kupambana na mimi kama alivyowasaidia kudhulumu na kutoa roho za watu wasio na hatia. Lakini kwa busara zangu nilimuonya na kuonesha kiburi kwake ndicho kilichomponza.
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.59.
ILIPOISHIA;
Walitoka huku wakiamini mzee Njiwa Manga uwezo wake wa kutibu umepungua ndiyo sababu ya kushindwa kuwasaidia kupambana na Balkis.
SASA ENDELEA...
BAADA ya kutoka kwa mganga wakiwa ndani ya gari lao walianza kujadiliana kuhusiana na maneno ya mzee Njiwa Manga.
Sasa tutafanya nini?
Kwa nini tusiachane naye?
Mmh! Lazima atatufanyia kitu kibaya, si umemuona ametokwa na machozi ya damu kwa hasira, anaweza kutufanya kitu kibaya.
Sasa tufanyeje?
Lazima tutafute njia nyingine, unajua mzee yule nimemtoa akili, shida yake ni fedha na si kutaka kujua tutafanya nini.
Tena namshangaa anajifanya hataki fedha wakati anafanya kazi ile ili kusukuma maisha yake, Ashura aliongezea.
Ooh! Nimekumbuka kuna sehemu moja kuna mtaalam mmoja nina imani anaweza kutusaidia. Tonny alisema.
Kama ni hivyo tusirudi nyumbani tupitie huko huko maana bado simuamini yule mwanamke amenitisha sana, lakini Tonny asiwe kama mzee Chujio tukaumbuka?
Namuamini ameshawahi kunifanyia mambo mengi ambayo sikuwahi kukushirikisha, y ule mzee huwa haulizi ukimueleza chochote hata kuua anafanya,tena anapenda kuua kama nini.
Tena huyo ndiye mzuri sana, lakini tutafika salama? Ashura alikuwa na wasiwasi.
Sifa ya yule mganga ukiwa na wazo la kwenda kwake kuanzia hapo unakuwa salama hakuna kitu cha kukuzuia.
Tena huyo anafaa, kwa nini hukusema mapema?
Nilimuamini babu yule baada ya kujua ana sifa ya kutatua matatizo ya majini.
Basi tuelekee, leo hatuna kazi nyingine zaidi ya kuujua mwisho wa Balkis.
Safari ilielekea kwa mganga mwingine, njia nzima ilikuwa ni mitihani mingi kutokana na gari kuteleza bila utelezi na kuona mambo ya kutisha lakini safari iliendelea. Matukio hayo yalimtisha sana Ashura kufikia hatua ya kumuomba mwanaume wake wasitishe safari yao.
Tonny kwa nini tusirudi huoni safari yetu imejaa matukio ya kutisha tunaweza kupata ajali mbaya na kufa?
Shuuna hivi ni vitisho vya Balkis baada ya kugundua tunakwenda kwa mganga mwenye uwezo wa kumuangamiza. Hawezi kutufanya lolote ni kuhangaika kwake kwa mfa maji tu.
Mmh! Yaani naogopa kuna kipindi niliona mti wa ajabu umetokea ghafla barabarani, nilijua tunakufa na kufumba macho, nilipofumbua nilishangaa kuona tumevuka salama.
Shuuna hizo ni hila za majini, ule si mti ni kiini macho tu ukiukwepa tu umeumia lazima gari litapinduka.
Jamani! Ningekuwa mimi ningeukwepa.
Lazima ungepinduka, barabara hii umepita mara ngapi?
Mara nyingi tu.
Huo mti uliwahi kuuona?
Sijawahi kuuona.
Basi mimi nimepasua katikati ya mti ule hakuna kitu kilichoizuia gari kupita.
Mmh! Kweli yule mwanamke ni jini.
Awe jini mara ngapi?
Tukipata dawa itatusaidia sana.
Hesabu tumemkomesha, yule bwana alisema katika dunia hii hawezi kurudisha roho ya mwanadamu tu, kwa vile ni kazi ya Mungu peke yake. Lakini chochote kinachowezekana kwa mwanadamu kwa uwezo wa Mungu anakifanya kwa ukamilifu.
Baada ya kufanikiwa kuvuka vizingiti vya Balkis walifika Vingunguti walikata kushoto njia ya kuingia Jeti Rumo, waliifuata njia ile mpaka maeneo ya Kijiwe Samli. Tonny alisimamisha gari mbele ya duka moja ambapo pembeni yake kulikuwepo na vijana wakicheza drafti.
Tumefika, Tonny alisema huku akizima injini ya gari.
Mbona yupo kwenye makazi ya watu? Ashura aliuliza.
Siku hizi huduma zimewafuata watu, hakuna waganga wa kizamani kuwa kijijini nyumba za majani. Waganga wa siku hizi wanakwenda na wakati hata mavazi yao si kaniki na ngozi na shanga kibao.
Baada ya kufunga gari na kuliacha katika hali ya usalama aliifuata njia ya uchochoro kati ya nyumba ya duka na ya kawaida na kutokea mtaa wa pili walikata kulia kuelekea kwa mganga.
Tonny huku umepajuaje?
Kuhangaika, unafikiri kama tungekuwa tunamtegemea mzee Chujio peke yake ingekuwaje?
Mmh! Na kweli, ona kama alivyotutoa nishai yule mzee sijui kunguru, baada ya kifo cha mzee Chujio tungekwenda wapi?
Atajijua mwenyewe kama anaitwa Njiwa au bundi, mzee yule kanichefua hana lolote kumbe sifa za uongo. Tonny alimkandia mzee Njiwa Manga.
Nini kitaendelea? Kweli mganga huyu ana uwezo wa kumdhibiti Balkis?
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.61.
Ilipoishia:
ILE ilimfanya akose raha na kutokwa na machozi, alipata wazo la kuwahi chini ya bahari kabla uchawi wa kumuua haujafanywa. Lakini alikumbuka ana deni na baba yake la kuachana na Muddy mwanaume aliyepanga kuachana naye baada ya kumpa ujauzito ambao wazazi wake hawatakuwa na nguvu na kumruhusu aishi naye.
Sasa endelea...
ALIJIKUTA akiuapia moyo wake kuwa atapigana mpaka tone la mwisho la damu yake lakini hatarudi chini ya bahari. Akiwa amesimama pembeni ya nyumba kwenye mti wa jirani katika umbile la njiwa, alijiuliza atafanya nini ili aweze kujiokoa na hatari ile.
Alishuhudia Ashura akitoa laki tano kwenye mkoba na kumpatia mganga ambaye alinyanyuka ili akachukue vifaa vya kutengengeneza dawa ya kummaliza. Balkis juu ya mtu alijikuta akipoteza uwezo wake wa kawaida baada ya kuamini wakati wowote anaweza kufanyiwa kitu kibaya.
Alijua waganga wengi huwavuta majini kwa dawa na kuwamaliza, akiwa ametota kwa jasho kwenye manyoya yake kwa hofu ya kifo. Alimuona mganga akitoka uani kwake na kumwita mkewe aliyekuwa akizungumza na wanawake wenzake.
Mke wangu, alimsikia akimwita mkewe kwa sauti ya juu kidogo.
Abee mume wangu, alimuona mkewe aliyekuwa amevalia nguo na vito vya dhahabu kila kona kuonesha kwamba wanaishi maisha ya kifahari.
Hebu nenda dukani kaniletee ile kiboko ya majini.
Kuna mtu ana jini nini? Alimuuliza huku akipokea fedha.
Kuna jini mmoja anawakosesha raha wateja wangu.
Sasa unataka kumfanya nini, unataka kumtia kwenye chupa nini?
Namuulia mbali, unajua jini ukilifungia kwenye chupa likitoka linaweza kukumaliza. Dawa yake sasa hivi ni kulimalizia mbali, itakuwa wakijua wanakuja Kakakuona watakuwa wanakimbia wenyewe.
Ngapi nichukue?
Kwa vile nammaliza kazi kabisa nichukulie tano na ndimu kumi na nne na sindano kumi na nne.
Mmh! Mbona nyingi sana leo umepania.
Nimemuona ana kiburi, pia ana mchezo wa kutaka ushindani, nikimfunga anaweza kutoka, si unajua siku hizi watu wakikuta kitu lazima wakifungue.
Kauli ile ilimshtua Balkis ambaye aliamini siku ile ndiyo ilikuwa ni mwisho wa maisha yake, wazo la haraka lilikuwa ni kurudi kwao na kuwa tayari kukubaliana na matakwa ya baba yake ya kuachana na Muddy ili awe salama.
Mmh! Haya kazi kwenu, mkewe mganga alisema huku akitokea mlango wa nyuma kwenda duka la dawa za asili.
Balkis alimuangalia mke wa mganga na kumuona ni mweupe asiye na kinga imara ya kuzuia nguvu za majini, kutokana na kukataa kuchanjwa na mumewe. Kwa vile mumewe alimpata baada ya kuja kutibiwa kutafuta dawa ya kuolewa na kigogo mmoja na mganga akamgeuzia kibao cha kutengeneza dawa ambayo ilimfanya yule mwanamke ampende mganga badala ya mtu aliyemkusudia.
Baada ya kufanikiwa kumpata, ilibidi akubaliane na mkewe ambaye hakutaka kuishi kiganga zaidi ya maisha ya kifahari ya kujirusha kwa kutembelea gari. Kutokana na uwezo wa mganga wateja wake wengi walikuwa watu wenye uwezo hivyo kumfanya asiwe na shida ya fedha ndogo ndogo.
Pamoja na mkewe kutoishi kama mke wa mganga na muda wote kuvaa nguo na vito vya thamani, bado alikuwa akijua baadhi ya dawa ambazo zilikuwa zikitumiwa na mumewe.
Hata pale mumewe alipokuwa safarini alielekezwa jinsi ya kuzitengeneza na kuwapa wateja lakini mumewe alipokuwa nyumbani yeye aliendelea na maisha yake ya kujiachia.
Balkis aliona ile ndiyo nafasi yake ya kufanya kitu kitakachomfanya mganga asifanye lolote juu yake. Alikurupuka kutoka juu ya mti kama njiwa na kumgonga kichwani mke wa mganga ambaye alikwenda juu na aliporudi chini hakuomba hata maji.
Waliokuwepo pembeni walimuona njiwa mweupe akimgonga kichwani na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Kelele na kilio cha mtu aliyeingia kwa mganga zilimshtua mganga aliyekuwa ameanza kuandaa vifaa vya kummaliza Balkis. Aliacha na kutoka na kukutana na mfanyakazi wake wa mapokezi.
Vipi? alimuuliza baada ya kumuona amechanganyikiwa.
Mama.
Amefanya nini?
Ame....
Yupo wapi? aliuliza huku presha imempanda.
Yupo nje ya nyumba.
Kafanya nini?
Si...sijui.
Mara alisikia sauti za vilio vya mashoga wa mkewe ambao walikuwa wakizungumza naye muda mfupi uliopita, vilio vile vilizidi kumtisha na kumchanganya.
Jamani kuna nini? Aliuliza tena macho yakiwa yamemtoka pima.
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.63.
ILIPOISHIA
Hatuna jinsi
Huu si wakati wa kulaumiana tutafute njia ya kujiokoa kwa Balkis.
Mmh! Huoni tukitafuta mganga mwingine ni sawa na kuongeza mafuta kwenye moto?
Sasa tutafanya nini? Tonny alionesha kuchanganyikiwa na kusahau kama wanatakiwa kuondoka eneo lile na badala ya kujilaza kwenye usukani.
SASA ENDELEA...
Tonny hebu ondoa gari kama huwezi nipishe miye niendeshe.
Ashura njoo uendeshe nina imani Balkis anajua mimi ndiye mbaya wake namba moja, hata sijui itakuwaje?
Tonny we twende nyumbani lolote litakalotokea tuwe tayari kukabiliana nalo.
Mmh! Haya sina jinsi yaani najuta kumfahamu Balkis.
Lakini si tumeambiwa ni kiumbe mwenye huruma?
Si umesema umeona akitokwa na machozi ya damu kuonesha hasira unafikiri mtu tuliyetaka kumuua atakuwa na huruma na sisi?
Bwana wee hebu tuondoke mengine tutayajua huko huko.
Tonny alijikaza na kuwasha gari kisha waliondoka eneo la Kiwalani, Balkis aliwaona kwa mbali wakija, akiwa amejawa na hasira kutokana na kiburi walichokionesha alikosa adhabu inayowafaa kutokana na roho zao mbaya ili wasirudie tena kumfuatafuata. Adhabu aliyoipanga ilikuwa kuhakikisha kwanza anamtia aibu Ashura na mumewe kwa kumgeuza kiumbe wa ajabu asiyependwa na wanadamu au wanyama.
Hakutaka kuwasumbua aliwaacha warudi mpaka nyumbani kwao ili aweze kufanya alichokikusudia. Ashura na mwanaume wake walishangaa kwenda mpaka nyumbani kwao bila kukutana na tatizo lolote, walipofika walishukuru Mungu.
Baada ya kuingia ndani hata kabla hawajakaa vizuri mlango uligongwa, Tonny alikwenda kuufungua na Ashura alikwenda chumbani. Alipofungua alipatwa na mshtuko uliomfanya aanguke chini na kupoteza fahamu.
Ashura aliyekuwa chumbani alishitushwa na kishindo cha mtu kuanguka chini, alimwita mwanaume wake huku akitetemeka ili ajue kimetokea nini.
Toooni, aliita kwa sauti ya juu bila kupata jibu, woga ulimwingia.
Alirudia tena kumwita Tonny bila jibu lolote, alitoka chumbani huku akiwa na wasiwasi, kabla ya kufika sebuleni alisikia harufu ya manukato aliyoyazoea kuyasikia wakati Balkis akiwa karibu yake. Harufu ile ilimjulisha tayari walikuwa wamevamiwa ndani ya nyumba yao.
Mlangoni alikuwepo Tonny aliyekuwa amelala chini, alianza kutetemeka. Akiwa bado katika hali hiyo, mlango uligongwa tena, alitamani kurudi chumbani kwake lakini alijikaza na kusogea hadi mlangoni na kuufungua. Alipofungua alikutana uso kwa uso na Balkis, kwa woga alioupata haja ndogo ilimtoka bila kutarajia.
Samahani Balkis, aliomba msamaha huku akipiga magoti kwa kujua kiama kimefika.
Ya nini?
Najua nimekukosea.
Kosa gani?
Unajua, naomba usituue.
Kuua ni kazi ya Mungu peke yake si ya kiumbe chochote.
Mbona ume.., Ashura alisita kusema Balkis kamuua mke wa mganga Kakakuona kwa kuhofia kumzulia jambo ambalo huenda hakulitenda na kumuongezea hasira.
Nimefanya nini?
Hujafanya kitu.
Najua ulitaka kusema nini.
Ha...ha...pana, Ashura alitetemeka kwa hofu.
Kwanza mmwagie maji mwenzako azinduke, nashangaa anakuwa mwoga wakati yeye ni bingwa wa kutoa roho za watu.
Naomba unisamehe Balkis najua kiasi gani tumekuudhi.
Hebu fanya kwanza niliyokuagiza, Balkis alisema kwa sauti kali kidogo.
Ashura alikwenda jikoni na kurudi na maji kwenye bakuli.
Mmwagie kidogo kichwani.
Ashura alifanya kama alivyoelekezwa, baada ya kumwagia maji mwanaume wake alirudiwa na fahamu. Tonny alipozinduka alishtuka kujikuta yupo mbele ya Balkis. Alinyanyuka na kupiga magoti mbele ya Balkis kuomba msamaha.
Samahani Balkis najua umekuja kutudhuru, lakini tunakuhakikishia hatutarudia tena kukufuata, Tonny alisema huku akitokwa na machozi.
Kabla ya kuzungumza lolote naomba Ashura aende akajisafishe, siwezi kuzungumza na mtu aliyejipaka najisi.
Ashura alikwenda bafuni kujisafisha kisha kubadili nguo na kurudi mbele ya Balkis bila kujua nini hatima yao baada ya kumchokonoa kwa muda mrefu. Baada ya kurudi alisogea kwa mwanaume wake na kuungana naye kupiga magoti.
Naomba mkae chini, magoti yenu yataniongeza hasira niwageuze kuwa manyani
Baada ya kukaa alimuuliza Ashura swali lake la awali.
Ashura, uliuliza mbona nimemuua mke wa mganga?
Ha...ha...pana sikumaanisha hivyo.
Naona unataka kunichefua nikugeuze kuwa nyoka sasa hivi muuaji mkubwa, hivi mimi nikifa ninyi mtafaidika nini?
Hakuna aliyejibu kitu, wote walibakia kimya nyuso zao wamezielekezea chini kwa aibu.
Etaenelea baadae kidogo...............