Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
- Thread starter
- #41
JINI WA DARAJA LA SALENDA......EP.10.
ILIPOISHIA;
Nawe ulipakwa mafuta yale ambayo hutumia majini wa kike, kujipaka sehemu za siri ambayo huongeza raha ya mapenzi kiasi cha kumfanya mwanaume asikuchoke na yeye kusikia raha ya mapenzi. Hata wewe hukuchoka na kusikia raha muda wote wa kufanya mapenzi na ulipoamka hukusikia uchovu wa mwili. Kwa kutumia mafuta yale unaweza kufanya mapenzi kila siku bila kuchoka.
Mmh! Kumbe.
Wakati wewe unakula raha ndiyo siku hiyo shoga yako yalimtokea kama yaliyokutokea siku za nyuma za mumeo kupoteza nguvu za kiume. Shogayo alikuja kazini akiamini ungeungana naye kwenye tatizo lake, lakini ilikuwa kinyume kitu kilichomchanganya mwenzako na kuwa njia panda tatizo la nguvu za kiume za mpenzi wake lilitokana na nini.
Baada ya jini Balkis kuwachanganya wazo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu lilifutika. Hali ile mwenzako aliamini huenda itaisha kutokana wewe kumhakikishia huenda tatizo lake likaisha kama lako bila kwenda popote. Naye aliamini na kumpa nafasi jini Balkis kufanya mapenzi na mpenziwe usingizini kufikia hatua ya kutokuwa na hamu naye. SASA ENDELEA...
Baada ya kuweza kukuchanganyeni akili, penzi mlilofanya na mumeo lilirudisha mapenzi yaliyoanza kutoweka. Kitu kile kilimuudhi sana jini Balkis na kuamua kukukomoa. Najua alichokufanya nikikueleza utaogopa lakini kwa vile umetaka mwenyewe sina budi kukueleza, kauli ya mganga ilinitisha lakini kwa vile maji nilikwisha yavulia nguo nilikuwa sina budi kuyaoga. Basi mganga akaendelea.
Usiku mlipokuwa mkifanya mapenzi bila kuzima taa jini Balkis alishindwa kufanya kitu chochote, kosa kubwa mlilofanya japo msingeweza kujua madhara yake. Nina imani mapenzi uliyofanya wakati wa giza na mwanga kuna mabadiliko yalitokea ulipofanya mapenzi?
Ndiyo.
Mlipokuwa mkifanya mapenzi gizani ulihisi maumbile ya mumeo kuwa makubwa na kusababisha uumie sana badala ya raha ikawa maumivu.
Ni kweli kabisa.
Basi wakati mlipokuwa mkifanya mapenzi gizani, mumeo aliondolewa juu yako na jini Balkis aliingiza mguu wake uliokuwa na kwato kama mbuzi na kuanza kukusukumia ndani.
Kauli ile ilinifanya nisijikie vibaya mpaka tumbo likaanza kunikata chini ya kitovu, nikiwa navuja jasho la hofu. Mganga aliendelea kunieleza maneno niliyohisi yananikata maini.
Basi ulijikuta ukivumilia huku ukiumia, ilifikia hatua kutotamani tena kufanya mapenzi na mumeo kwa kuamini maumbile yake yameongezeka ukubwa. Lakini ulipowasha taa ulishangaa kuyaona ya kawaida uliyoyazoea, kweli si kweli?
Kweli, nilijibu huku nikizidi kumuogopa mganga kuwa na uwezo wa ajabu kuyajua mambo ambayo hakuyaona lakini utafikiri alikuwepo.
Ajabu hukumwambia mumeo, kwa nini?
Hata sijui, nilimjibu.
Baada ya kuamua kutofanya mapenzi na mumeo kuogopa kuumizwa badala ya kupewa raha, uliamua kutafuta visingizio ili usikutane naye kimwili, uongo kweli?
Kweli.
Jana kuna kitu cha ajabu kimekutokea ndiyo sababu ya kumpigia simu Bi mkubwa wako?
Ni kweli.
Basi, baada ya kuona hufanyi tena mapenzi na mumeo, jana ulipolala uliota ndoto kuna mtu anakuingiza mkono sehemu zako za siri na kuanza kukukoroga kama anavuta kitu toka sehemu zako cha siri na ulipoamka ulijikuta ukitoka damu ambazo uliamini ni za hedhi japo ulishangaa kutokwa na damu ya hedhi mara mbili kwa mwezi kitu ambacho hakikuwahi kukutokea maishani mwako.
Ni kweli.
Unajua madhara yake?
Hapana!.
Naomba uwe na moyo mgumu kwa vile alichokifanya kwa tiba ya kubabaisha hutapona milele.
Mungu wangu, kauli ilitushtua mimi na mama na kujiuliza ni ugonjwa gani tena huo Yaillah.
Baba ni ugonjwa gani tena huo? Ilibidi mama aulize baada ya mimi kuwa katika wakati mgumu nilishika mikono kifuani, nilimuomba Mungu aniepushe na balaa linalotaka kunikumba.
Jina Balkis alijiulaumu kwa kuamini alifanya kosa ambalo aliliona limempotezea mapenzi ya mumeo kwake, mganga alimjibu mama.
Mapenzi yapi hayo? Mama aliendelea kuuliza.
Kosa kubwa alilofanya ni kumpaka mafuta ya kuongeza ladha ya mapenzi mwanao, kumbuka maumbile ya jini na mwanadamu yanatofautiana, kwa vile yako ya kibinadamu baada ya kukupaka ilizidi raha mara dufu na thamani yake kwa mumeo ilishuka. Alichokifanya kilikuwa kukutoa kizazi kitu ambacho ndicho kitakacho vunja ndoa yenu. Katika ndoto ulichokiota ndicho kilichotendeka usiku wa jana. Jini Balkis alikutoa kizazi na sasa hivi huwezi kuzaa tena maishani mwako.
Mungu wangu, kauli ya mganga ilinikata maini.
Sasa baba utatusaidia vipi? Mama bado alikuwa na ujasiri kutaka kujua nini hatima ya ukatiri wa jini Balkis kwangu.
Mmh! Ndiyo maana nikasema ipo kazi tena kazi kubwa sana si ya kitoto na tukifanya mchezo tutapotea wote.
Jamani, tupotee kivipi?
Vita yake ni kubwa sana, kumdhibiti naweza lakini kama nitakufanyia kinga ya kukufunga huwezi kupona tena. Na kosa lolote linaweza kuhatarisha maisha yetu. Hawezi kukubali kuona anazuiwa kutimiza dhamira yake, kwa kutumia nguvu zake anaweza kututeketeza wote.
Unataka kutuambia kuna uwezekano wa kupona?
Upo, lakini ndiyo mzame sana.
Baba wewe huwezi? Mama aliuliza tena kwa vile mimi nilikuwa nimechanganyikiwa kwa niliyoyasikia.
Uongo mbaya, mimi siwezi kukirudisha kizazi chake, si yeye ni wanawake wengi wametolewa na yote kaenda kuiweka chini ya bahari kwenye mwamba wa maji yaliyotulia pia hayafikiwi na kitu chochote kitakachoweza kugusa kizazi kile. Kama utaenda hospitalini wanawake wengi wanasumbuliwa na maradhi ya tumbo na wengi maradhi yao kwa tiba ya kisasa hayaonekani lakini siri ni kwamba wengi wao wameondolewa kizazi na kingine sasa hivi matatizo ya nguvu za kiume yamekuwa mengi ambayo yameweka migogolo lakini mabwana hao wakifanya mapenzi ndotoni na mwanamke mzuri hujikuta hawana hamu na wake zao.
Ni kwa sababu gani? Mama aliuliza.
Hakuna sababu nyingine ni ya huyo huyo jini Balkis ambaye amekuja duniani kwa sababu ya kuharibu ndoa za watu pia kupata tiba ya tatizo lake la uzazi. Tatizo hili litakwisha akiisha maliza kazi yake ya kupata vizazi mia, ambao walipata bahati ya kutokutana naye. Lakini wengine wote ambao hawatapata tiba mapema ndiyo watakuwa tasa milele.
Siri nzito za jini Balkis zinazidi kufunguka, nini hatma ya yote je kuna tiba sahihi ya tatizo hilo? Kuyajua yote hayo? Endelea hapa chini
JINI LA DARAJA LA SALENDA.......EP.11
ILIPOISHIA:
Eneo hilo halifikiwi na kitu chochote kinachoweza kugusa kizazi kile. Kama utaenda mahospitalini wanawake wengi wanasumbuliwa na maradhi ya tumbo. Wengi maradhi yao hayaonekani kwa vipimo vya kisasa lakini siri ni kwamba wengi wao wameondolewa vizazi.
Kingine sasa hivi matatizo ya nguvu za kiume yamekuwa mengi ambayo yamesababisha migogoro mikubwa. Wanaume hao wakifanya mapenzi ndotoni na mwanamke mzuri hujikuta hawana hamu na wake zao.
Ni kwa sababu gani? Mama aliuliza.
Hakuna sababu nyingine zaidi ya huyo huyo jini Balkis ambaye amekuja duniani kwa sababu ya kuharibu ndoa za watu pia kutafuta tiba ya tatizo lake la uzazi. Tatizo hili litakwisha akishamaliza kazi yake ya kupata vizazi mia. Watakaokuwa na bahati ya kutokutana naye watasalimika. Lakini wengine wote ambao hawatapata tiba mapema ndiyo watakuwa matasa milele. SASA ENDELEA...
Unafikiri ni mganga gani anaweza kutusaidia? Nilimuuliza nikiwa nimekata tamaa.
Mmh! Nendeni Bagamoyo kwa mzee mmoja maarufu sana maeneo ya Mlingotini, anaitwa Ustaadh Sudi Makata.
Una uhakika?
Japo sina uhakika kwa asilimia mia, lakini yule bwana namwamini sana.
Tutamjuaje?
Mkifika pale Bagamoyo maeneo ya Mlingotini muulizeni mzee Njiwa Manga.
Ni tofauti na ustaadhi Makata?
Hapana ndiye huyo huyo Makata, jina la Njiwa Manga kapewa na watoto aliokuwa akiwatuma wamkamatie njiwa manga kwa ajili ya kazi zake za majini. Kila mtoto aliyetumwa akimuona alimwita babu wa njiwa manga. Basi ikawa njiwa manga, njiwa manga mpaka leo.
Mmh! Tutajitahidi twende haraka.
Wala msiwe na haraka, jipangeni kwani tatizo limekwishatokea, mganga alitutuliza.
Sawa tutafanya hivyo.
Ila leo nitakupa dawa ya kuoga na kufukiza ndani mwako, lakini hapa naona itakuwa vigumu kwa vile mumeo haamini ushirikina. Kwa hiyo dawa ya kufukiza iache ila utaoga hii ambayo itakusaidia kumfukuza jini Balkis asikusogelee. Pia kuna kitu nilisahau kuwaeleza, leo wakati mnarudi nyumbani kutoka ofisini, mlipofika daraja la Salenda mlimuona mwanamke mmoja mrembo sana akiwa amesimama pembeni ya barabara chini ya mti?
Ndiyo.
Baada ya hapo gari lilizima ghafla?
Ndiyo.
Yule mwanamke mlimuona akibadilika mavazi?
Ndiyo.
Basi yule ndiye jini Balkis, ni mwanamke mzuri sana ambaye hakuna mwanaume yoyote anayemtaka akamkataa. Lakini ana roho mbaya, kwa sababu ana matatizo ya uzazi, dawa aliyoelezwa ni kutafuta vizazi vya wanawake mia moja ili atengenezewe dawa ya kupata mtoto.
Mungu wangu, kama ni hivyo unafikiri nitaweza kupona kweli? Niliuliza kwa sauti ya kukata tamaa.
Ukiwahi utapona! Mpaka sasa inaonesha ana vizazi ishirini na mbili, bado vingi na havipati kwa urahisi namna hiyo.
Mbona mzuri sana, jini gani anavaa nguo kama binadamu, si huwa nasikia wana mabawa?
Wenye mbawa si majini bali malaika, wao ni kama binadamu kabisa, wanaishi maisha kama watu ila wamepewa uwezo wa kujibadili kuwa katika umbile lolote watakalo, pia wana nguvu za ajabu walizobarikiwa na Mungu za kuonekana wanapopenda wao.
Kumbe!
Alifanya vile ili mmuone, baada ya hapo aliondoka na ninyi gari lenu liliweza kuondoka, kitu ambacho kiliwahi kumtokea shoga yako siku aliyohudhuria sherehe ya kuagwa jini Balkis kuja duniani rasmi. Mlipofika nyumbani kwako kuna kitu kimoja kilitokea ambacho shoga yako ilifikia hatua ya kukufikiria vibaya na kuamini huenda na wewe ni jini.
Mungu wangu, kitu gani hicho?
Alipoingia ndani taswira ya sura ya jini Balkis ilitanda kwenye uso wa mama yako, kitu kilichomshtua sana. Baadaye alijiondoa na bi mkubwa kuwa katika hali yake ya kawaida. Shoga yako aliondoka akiwa hakuamini kabisa. Kama unabisha ukirudi nyumbani muulize kaona nini.
Basi baada ya maelezo yale tulirudi, huwezi kuamini kidogo gari linishinde kuendesha kutokana na mshtuko nilioupata. Lakini mama alinipa moyo kwa kuniambia ili nipate ukweli wa kile nilichoambiwa na mganga lazima niende kwa waganga zaidi ya mmoja. Lakini nilimweleza mama mbona yote aliyoyasema yana ukweli kwa asilimia mia?
Lakini mama alinieleza inawezekana ni kweli kwa asilimia kumi, mengine tusiyoyajua huwa ni uongo wa waganga ili kujipatia pesa. Nilimueleza mbona hakutaka pesa zaidi ya kutueleza twende kwa mganga mwenye uwezo zaidi yake.
Mama alinikata maini kwa kunieleza kuwa waganga wana tabia ya kutafutiana wagonjwa na kugawana pesa kwa kuufanya ugonjwa uonekane mkubwa usioweza kutibiwa. Tukienda kwa mganga mwenzake tutaambiwa pesa nyingi ambazo hatutaweza kukataa.
Kwa hiyo mama hata kutolewa kizazi ni uongo? Nilimuuliza.
Uongo, nilishindwa kumkatalia angeona namuingilia kwenye kazi yake.
Kwa hiyo mama nisiwe na wasiwasi?
Ondoa wasiwasi, kitu kama hicho hakipo.
Basi shoga niliporudi kidogo moyo ulitulia japo maelezo yote kila nilipoyafikiria mwili ulisisimka. Niliporudi hata bila kupumzika nikakupigia simu. Basi shoga habari ndiyo hiyo tumekamatwa na jini sijui Balkis, Sharifa alimueleza Suzy aliyekuwa ametulia kama sanamu asiamini alichokisikia toka kwa shoga yake.
Sharifa acha kuligeuza jina lake si umesema anaitwa Balkis.
Kweli, Balkis.
Mmh! Mbona kama...
Kama nini?
Sijaelewa basi inaonekana hata mimi ana mengi juu yangu, kuna umuhimu kesho kunipeleka na mimi, Suzy alimweleza shoga yake huku wasiwasi ukiongezeka moyoni mwake kwa kuamini mpenzi wake anaweza kumuacha kwa penzi la ndotoni na jini Balkis linalotumia dawa ya kuongeza ladha ya mapenzi na yeye kuonekana si mali kitu.
Sawa tutakwenda.
Waliagana kwa Suzana kurudi nyumbani kwake kutafakari aliyoelezwa na Sharifa, moyoni alikuwa na mambo mawili; kukubali na kukataa. Akili yake ilikuwa kwenye kukataa na kuamini hakuna vitu kama vile. Etaendelea baadae......................