Jina unalompa mwanao lina maana gani?

Jina unalompa mwanao lina maana gani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,586
Reaction score
161,451
Majina yana maana kubwa sana kwenye maisha yetu.
Tabia na muonekano wetu umejengwa kwa kiasi kikubwa na majina tuliyopewa.
Mtoto akiitwa siwema, kamwe hawezi kuwa mwema.
Ukimuita mwanao Majuto, daima atakuwa anajuta.
Haya sasa oneni maajabu haya yaliyotokea Sinza.

Ni kweli majina yana maana sana tunapowapa watoto wetu na hili hata mi nimeliona na kulishuhudia mi mwenyewe sio kuisimuliwa,hiku kuna watu wanaoitwa taabu,masumbuko,mateso na shida ambao nawajua jamani kama ni mateso,taabu,shida na mahangaiko wanavipata kweli.najua yote hayo huwapta wengine pia na hayaepukiki lakini kwa wenye hayo majina hali ni mbaya zaidi so chonde chonde wazazi names are the authors of our children destinies!
 
Na si hayo tu hata majina ya kurithisha mara nyingi huwa yana matatizo. ukimpa mtoto jina la kurithi basi mara nyingi huwa na tabia kama za yule mwenye jina.
 
Ni kweli majina yana maana sana tunapowapa watoto wetu na hili hata mi nimeliona na kulishuhudia mi mwenyewe sio kuisimuliwa,hiku kuna watu wanaoitwa taabu,masumbuko,mateso na shida ambao nawajua jamani kama ni mateso,taabu,shida na mahangaiko wanavipata kweli.najua yote hayo huwapta wengine pia na hayaepukiki lakini kwa wenye hayo majina hali ni mbaya zaidi so chonde chonde wazazi names are the authors of our children destinies!
Na ndo maana wanyakyusa wanawapa majina yenye akili watoto wao,utasikia
ASANGALWISYE,ANDULILE,ANGOLWISYE,ANDANBWIKE................
 
Hii inamata sana, kuna mwandishi mmoja maarufu alimwita mwanae "Tanzania".
Sijui alifikiria nini.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Majina yana maana kubwa sana kwenye maisha yetu.
Tabia na muonekano wetu umejengwa kwa kiasi kikubwa na majina tuliyopewa.
Mtoto akiitwa siwema, kamwe hawezi kuwa mwema.
Ukimuita mwanao Majuto, daima atakuwa anajuta.
Haya sasa oneni maajabu haya yaliyotokea Sinza.

535610_10151536096921660_1951249359_n.jpg

ni kweli aise midomo huumba! muhimu kuliko yote ni kumpenda mwanao kabla hajazaliwa kwa kumtafutia baba/mama mwinyi kila ambacho ungependa awe nacho kuanzia muonekano mpaka akili na akizaliwa umpende zaidi kwa kumpa jina zura ambalo litamuongezea baraka maishan.
 
Mtoto wangu nilimaanisha unconditional love, unlimited love. God's love. Gracelyne
 
siku hizi watoto utasikia kitaa wanaitwa Rihanna,Jakaya,Bujibuji n.k muulize sababu utasikia oooh nampenda huyo mtu,au unamwita mtoto jina la babu au bibi yake wakati ni mlevi wa kupindukia,anapenda nguvu za giza,matambiko ndo usisema halafu hufanyi jitihada za kuyavunja hayo manguvu yasimwingie mtoto matokeo yake mtoto akiharibikiwa wachawi wanatafutwa loh!!!!!!!!!!!!!
 
Nawashukuru wazazi wangu mungu awaondolee abadhabu ya dunia na akhera, katika watoto 10 hakuna hata mwenye jina la ajabu,mamangu mkubwa watoto wake laa mpaka nashanga sijui majina anayatoa wapi, Oktoble,sijui Taudundo,yani mpaka nashangaa .. ahh mungu aninusuru sitowapa wanangu majina mpaka yakawa vituko...
 
Mkuu em funguka basi utuambie maana yake yasije yakawa ndio yaleyale ya akina mateso.
Na ndo maana wanyakyusa wanawapa majina yenye akili watoto wao,utasikia
ASANGALWISYE,ANDULILE,ANGOLWISYE,ANDANBWIKE................
 
mhm hapo nakataa kabisa kwani kila kabila lina majina mabovu sana mfano hao wanyakyusa majina yao ya ajabu sasa wewe kumpa mtoto jina la ambindwile, afwelile, angolwisye, asangalwise, bukenja, bikunyasya, ambilikile, fikufyuka, ngupasya na mengineyo mengi huoni hayo ni majina mabovu ambayo yatamletea mwanao matatizo matupu sio hata ndugu zetu wangoni nao utasikia mapunda, man'gombe, masuluali, na wamakonde ndo kabisa chipuni, chipedi na wapare hao ndo sisemi maana naogopa mtu fulani hapa atanitoa roho bure

quote_icon.png
By NITIKE NDOSI
 
ladyfurahia, Wanyakyusa ni wacha Mungu sana, majina yao yanampa sifa na utukufu Mungu. Ambindwile, maana yake amenibadilisha, kutoka kwenye dhambi na kunifanya mwema.
Afwilile, maana yake Yesu alinifia msalabani.
Hayo majina yanayo anzia na herufi B mengi yao ni ya BHAPANJA, yana mapepo
mhm hapo nakataa kabisa kwani kila kabila lina majina mabovu sana mfano hao wanyakyusa majina yao ya ajabu sasa wewe kumpa mtoto jina la ambindwile, afwelile, angolwisye, asangalwise, bukenja, bikunyasya, ambilikile, fikufyuka, ngupasya na mengineyo mengi huoni hayo ni majina mabovu ambayo yatamletea mwanao matatizo matupu sio hata ndugu zetu wangoni nao utasikia mapunda, man'gombe, masuluali, na wamakonde ndo kabisa chipuni, chipedi na wapare hao ndo sisemi maana naogopa mtu fulani hapa atanitoa roho bure
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom