Jina halisi la marehemu Eddy Shegy ni nani?

Jina halisi la marehemu Eddy Shegy ni nani?

Alianza kuweka sukari kwenye mboga kulikuwa na wageni waliondoka bila kuaga,akaanza kuvunja vioo vya dirisha apate kuchungulia wapitao njiani! Shikaamoo ikaisha ikabaki vipi babu mambo zako eheee vipi babu mambo zako eheeee

'...alianza kuweka sukari kwenye mboga, nikaonja haviliki tukalala na njaa...kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai, nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga...kafuatia kuchelewa akienda sokoni, nikimuuliza anitukana hadharani aibu...kuna gari imekuja hadi mlangoni, kujitetea akasema mjomba wake kaja...hivi juzi kavunja kioo cha dirisha, apate kuchungulia wapitao njiani...hatimaye kunibeza na kunidharau, shikamoo ikaisha ikabaki vipi babu mambo zako weewe...nilishindwa kumuuliza, sikutaka kumuudhi, sababu nilikuwa nampenda, nampenda saana...!...asante sana Eddy Sheggy 'Fast Mover' na Emma Mkello
 
'...ama kweli hakikosi kasoro jamani ee, kwa muda mrefu tulioishi nayee, nilimpenda sana lakini mwenzangu mambo yake, yakawa ulaghai ee ya ulaghai mama ee... Nimekanyaga moto, kwa kujitosa kwa mchumba anayetingisha mji, nikajua nimepata oo jama kumbe nimepatikana....! Siku ya kuondoka kwake akabeba kila kitu, ndani ya nyumba nikabaki sina kitu... Tabia ya mchumba wangu ingelingana na urembo wake, angefaidika jinsi nilivyompenda sana...hata wazazi wangu kweli walimpenda sana lakini walisema mwenyewe kajiharibia.... Njoo tucheze kakaa njoo tucheze dadaa mtindo wa kileoo, Watunjatanjata..! Eddy Sheggy/ Adam Bakari 'sauti ya zege'/ Madaraka Morris/solo kali ikipigwa na Hamza Kalala 'Komandoo' Washirika Tanzania Stars Band
 
Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa....
Na kisirani cha kufokewa na bosi....
Nahitaji wa kunibembeleza....
Si kwa maneno ila kwa kunitomasatomasa....
Kwa mikono laini yenye bangili....
Rip Shekabughe

Hapo hajaimba Eddy Sheggy.
 
Mkuu usinipagawisheeeeeeeeee,nitaacha ofsi niende home nikazisikilize

Nyie vijana Wa leo sikilizeni mautumbo yenu, hizi tuachieni wenyewe! Nyimbo za vijana bwana hadi kichefuchefu!! Ubeti mmoja tu mapenzi limetajwa mara 30!!
 
Hata wewe kama umekosea uhakika ni Edmund Shekbughe siyo Edson Shekabughe.

Hilo jina la ubini linatoka sehemu gani ya Tanzania yetu. Sijawahi kulisikia hili jina likitumiwa na mtu mwingine yoyote.

Tiba
 
Eddy Sheggy,milima ya kwetu,r.i.p

Eddy Sheggy: Kapu la mjanja, Ogopa Tapeli, Mwisho wa mwezi( zote hizi vijana Jazz. Eddy Sheggy: Julie, Shakaza, Penzi la Ulaghai, Uke wenza- kulala sebuleni( zote hizi akiwa na Washirika Tanzania Stars- ni bendi mrengo wa pili wa Vijana Jazz).
Kwa kweli Eddie Sheggy alikuwa na sauti ambayo daah, we acha tu. Vibao hivyo nilivyovitaja vya bendi mbili hizo hata sasa hivi kikipigwa kimoja kila mmoja atasema vipaji vilikuwepo miaka ya tisini kurudi nyuma na hatabanduka kusikiliza hadi muziki husika uishe
 
'...ama kweli hakikosi kasoro jamani ee, kwa muda mrefu tulioishi nayee, nilimpenda sana lakini mwenzangu mambo yake, yakawa ulaghai ee ya ulaghai mama ee... Nimekanyaga moto, kwa kujitosa kwa mchumba anayetingisha mji, nikajua nimepata oo jama kumbe nimepatikana....! Siku ya kuondoka kwake akabeba kila kitu, ndani ya nyumba nikabaki sina kitu... Tabia ya mchumba wangu ingelingana na urembo wake, angefaidika jinsi nilivyompenda sana...hata wazazi wangu kweli walimpenda sana lakini walisema mwenyewe kajiharibia.... Njoo tucheze kakaa njoo tucheze dadaa mtindo wa kileoo, Watunjatanjata..! Eddy Sheggy/ Adam Bakari 'sauti ya zege'/ Madaraka Morris/solo kali ikipigwa na Hamza Kalala 'Komandoo' Washirika Tanzania Stars Band

Aisee hii Album naweza kuipata wapi! Kiukweli nikijua ilipo naenda kuinunua hata kwa elfu50. Penzi la Ulaghai yaani we acha tu. Kuna wimbo mwingine unaitwa WIVU nadhani aliimba Eddy Sheggy akiwa na Hemed Maneti kule Vijana Jazz au Washirika. Wakati fulani miaka ile ya tisini ilikuwa ni vigumu kujua hivi hii ni Vijana Jazz, Washirika Tanzania Stars( watu njatanjata) au Bimalee, kwa sababu combination za watu.kadhaa zilikuwa zikihama kati ya bendi hizo yaani Eddy Sheggy, Jerry Nashon( dudumizi) Muhina Panduka( toto tundu), Adam Bakari( sauti ya zege) na Abdallah Mgonazeroh. Kwa mfano wimbo ule wa Naenda Ilula kw wakwe zako sauti ya Toto Tundu imo lakini kama si kuambiwa na watangazaji wa RTD wakati kipindi cha jambo, mchana mwema na pole kwa kazi bila kusahau misakato kwamba ni Washirika au Bimalee au Vijana ndo wamepiga wimbo huu na hapo yupo msanii huyu na yule huwezi kuambua kiurahisi. Yaan bendi zilitisha kwa kila idara na kiukweli walikuwa kikazi kwa kuburudisha na tungo mahiri zenye mashiko na kila ujumbe mujaraabu kwa hadhira. Lakini daaaah leo musiki ni sauti kama mtu anaugua mafua yaani ni kero tupu
 
Hivi alikufa kwa ugonjwa au ajali ya gari.Eddy alikuwa mtunzi mzuri sana nakumbuka wimbo wake uitwao shakaza ulisababisha wagosi wote mjini wataniwe kwa kutumia jina la wimbo huo.
 
Hilo jina la ubini linatoka sehemu gani ya Tanzania yetu. Sijawahi kulisikia hili jina likitumiwa na mtu mwingine yoyote.

Tiba

Watu wa Tanga....ila sijui kama Eddy alikua mtu wa huko.
 
kama ndio hivyo,mbona hata Charles Hillary wa BBC nasikia ana jina lake halisi na sio hili ambalo tunamfahamu nalo.mwenye kulifahamu aliweke hapa tafadhali.kumbe huu utaratibu wa A.K.A haujaanza leo!?.nilidhani ni watu wa kizazi chetu tu.
 
Aisee hii Album naweza kuipata wapi! Kiukweli nikijua ilipo naenda kuinunua hata kwa elfu50. Penzi la Ulaghai yaani we acha tu. Kuna wimbo mwingine unaitwa WIVU nadhani aliimba Eddy Sheggy akiwa na Hemed Maneti kule Vijana Jazz au Washirika. Wakati fulani miaka ile ya tisini ilikuwa ni vigumu kujua hivi hii ni Vijana Jazz, Washirika Tanzania Stars( watu njatanjata) au Bimalee, kwa sababu combination za watu.kadhaa zilikuwa zikihama kati ya bendi hizo yaani Eddy Sheggy, Jerry Nashon( dudumizi) Muhina Panduka( toto tundu), Adam Bakari( sauti ya zege) na Abdallah Mgonazeroh. Kwa mfano wimbo ule wa Naenda Ilula kw wakwe zako sauti ya Toto Tundu imo lakini kama si kuambiwa na watangazaji wa RTD wakati kipindi cha jambo, mchana mwema na pole kwa kazi bila kusahau misakato kwamba ni Washirika au Bimalee au Vijana ndo wamepiga wimbo huu na hapo yupo msanii huyu na yule huwezi kuambua kiurahisi. Yaan bendi zilitisha kwa kila idara na kiukweli walikuwa kikazi kwa kuburudisha na tungo mahiri zenye mashiko na kila ujumbe mujaraabu kwa hadhira. Lakini daaaah leo musiki ni sauti kama mtu anaugua mafua yaani ni kero tupu

Eddy Sheggy: Kapu la mjanja, Ogopa Tapeli, Mwisho wa mwezi( zote hizi vijana Jazz. Eddy Sheggy: Julie, Shakaza, Penzi la Ulaghai, Uke wenza- kulala sebuleni( zote hizi akiwa na Washirika Tanzania Stars- ni bendi mrengo wa pili wa Vijana Jazz).
Kwa kweli Eddie Sheggy alikuwa na sauti ambayo daah, we acha tu. Vibao hivyo nilivyovitaja vya bendi mbili hizo hata sasa hivi kikipigwa kimoja kila mmoja atasema vipaji vilikuwepo miaka ya tisini kurudi nyuma na hatabanduka kusikiliza hadi muziki husika uishe

[video=youtube_share;DRXpd69qWxA]http://youtu.be/DRXpd69qWxA[/video]
 
Jamaa alikuwa na sauti tamu huyu, sikiliza hizi nyimbo ndiyo utajuwa kuwa Tanzania tulikuwa na wanamuziki kweli si hawa wezi wa beats za watu na wauza unga.
Shakaza Pele (Bima Lee)
Milima Ya Kwetu (Super Rainbow)
Kumaliza Mwaka Taabu (Bima Lee)
Tangawizi (Super Rainbow)
Kapu La Mjanja original (Vijana Jazz)
Happy Massawe original (Vijana Jazz)
Wivu (Vijana Jazz)
Ngapulila, Pt. I (Vijana Jazz)
Mwisho Wa Mwezi (Vijana Jazz)

Kaka Eddy, unastahili pongezi na Mungu mwenyezi akuweke mahala pema peponi, Amina!

Inaonekana hii ilikuwa ni BANTU GROUP na hawa jamaa walikuwa ndugu watatu kw amujibu wa Kitine.

"Hebu tumkumbuke Eddy Sheggy hapa akiwa na Bantu, akiimba na ndugu zaki Francis na Christian."
 
[Vituko Vya Bibi Huyu - Eddy Sheggy]

Nikitazama milima ya kwetu eeee,

machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo

Tulitoka wawili ninarudi peke yangu,

Baba na Mama wataniuliza Bibi yako yuko wapi

Natamani gari lisifike upesi,

kwa ile aibu nitakayo pata mbele ya wazazi

Kwa vile miezi michache imepita nilitoka na bibi yule

Alianza kuweka chumvi kwenye chai,

nilikua na wageni wakatoka bila kuaga

Akaweka sukari kwenye mboga,

nikaonja haviliki tukalala na njaa
Juzi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani
Walisema dalili ya mvua ni mawingu
Niliyempenda kanitoroka maa
(Kanitoroka nateseka) Walisema.........
[Sheggy]
Vituko eee vituko vya bibi huyu.......................
Sitaweza kumsahau oo mama aa
Sitaweza kumsahau oo bibi eeee
Alikua kama Helkopta,
ndege isiyochagua mahali pa kutua ee
Kila mtaa hapa jijini tazameni oh
Hana bwana mmoja wala wawili nifanye nini oh mama aa
(Walisema.............................)
​

​
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom