Jina halisi la marehemu Eddy Shegy ni nani?

Jina halisi la marehemu Eddy Shegy ni nani?

ulivyombiwa ndivyo hivyo hivyo!kuna mwingine alikua anaitwa said salmin mziray yeye akajiita syllersaid mziray

Mmh nimefanya kazi na marehemu Mziray sijawahi kusikia kuwa hayo ndio majina yake! Kwani alibadili dini mbona alikuwa mkristu wakati majina hayo ni ya kiislamu? Mbona hata nduze wana majina ya kikristo? Kaka yake mmoja anaitwa Richard Mziray kama sikosei..
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia Jina lake ni EDWARD SHEKIONDO lakini akalifanyia usanii akajiita EDDY SHEGGY. Namzungumzia kaka wa Christian Sheggy, mwanamuziki wa zamani wa Orchestra Super Rainbow, na Washirika Tanzania Stars (Watunjatanjata). Ameshatangulia mbele za haki. Anayejua UHALISI WA JINA lake atujuze ili kuweka kumbukumbu sahihi.

WAtanzania
TUondoe
NJaa
TAnzania
NJaa
TAnzania
 
Jamaa alikuwa akiitwa Edmund Shekabughe anatoka lushoto vuga(bazo)bila shaka.
 
Jina la Mziray mwambie akutajie Jese John wa TBC, jamaa ananifurahisha sana akilitaja jina Syllasaid sijui nini nini............ Mziray. Hongera Kaka Jese John
 
Jamaa alikuwa na sauti tamu huyu, sikiliza hizi nyimbo ndiyo utajuwa kuwa Tanzania tulikuwa na wanamuziki kweli si hawa wezi wa beats za watu na wauza unga.
Shakaza Pele (Bima Lee)
Milima Ya Kwetu (Super Rainbow)
Kumaliza Mwaka Taabu (Bima Lee)
Tangawizi (Super Rainbow)
Kapu La Mjanja original (Vijana Jazz)
Happy Massawe original (Vijana Jazz)
Wivu (Vijana Jazz)
Ngapulila, Pt. I (Vijana Jazz)
Mwisho Wa Mwezi (Vijana Jazz)

Kaka Eddy, unastahili pongezi na Mungu mwenyezi akuweke mahala pema peponi, Amina!

Hadi mauti yanamkuta alikuwa akitumikia bendi ya Bantu Group ya kiongozi Komandoo Hamza kalala, na wimbo wao maarufu wa 'Ngondoigwa' katajwa sana. Wimbo huu waliutengenezea MJ Records kwa Master Jay.
 
Najuwa ila hizo ni nyimbo ambazo nafikiri watu wengi watamkumbuka nazo kwani alitia fora sana.
 
walisemaaaaa dalili ya mvua ni mawinguuuuu,
nilimyempenda kanitoroka mamaaaaaaaaaaX 2

Nakumbuuka kuna mama yangu mdogo ndo alikuwa anaimba wakati huo enzi la club raha leo shooooooooooooooooooooo!

mkuu naomba link ya huu wimbo tafadhali
 
Alianza kuweka sukari kwenye mboga kulikuwa na wageni waliondoka bila kuaga,akaanza kuvunja vioo vya dirisha apate kuchungulia wapitao njiani! Shikaamoo ikaisha ikabaki vipi babu mambo zako eheee vipi babu mambo zako eheeee
 
  • Thanks
Reactions: ram
Nikitazama milima ya kwetu eeh eeh
Machozi yanitoka aah,narudi nyumbani, tulikuja wawili eeh narudi peke yangu
Baba na mama wataniuliza mke wako yuko wapiii
Ndugu jamaaa wataniuliza.......

Jamani nyimbo za zamani zilikuwa nyimbo kweli, RIP Eddy!

RIP Eddy Sheggy. Wimbo wa milima ya kwetu ulipangwa na kupangika vizuri sana!
 
Jamaa alikuwa na sauti tamu huyu, sikiliza hizi nyimbo ndiyo utajuwa kuwa Tanzania tulikuwa na wanamuziki kweli si hawa wezi wa beats za watu na wauza unga.
Shakaza Pele (Bima Lee)
Milima Ya Kwetu (Super Rainbow)
Kumaliza Mwaka Taabu (Bima Lee)
Tangawizi (Super Rainbow)
Kapu La Mjanja original (Vijana Jazz)
Happy Massawe original (Vijana Jazz)
Wivu (Vijana Jazz)
Ngapulila, Pt. I (Vijana Jazz)
Mwisho Wa Mwezi (Vijana Jazz)

Kaka Eddy, unastahili pongezi na Mungu mwenyezi akuweke mahala pema peponi, Amina!


Mkuu usinipagawisheeeeeeeeee,nitaacha ofsi niende home nikazisikilize
 
Eeee wene weangu shakaza. Nina makosa ani weangu shakaza.
gouni ingwe weangu shakaza. weangu wedi naawanyiika shakaza puke. puke puke
Kusheghuighwa kohe ni kufa ughumba naneeee
 
Mandela ni mwana wa Afrika ehh afunguliwe Mandela, Nelson Mandela x2
Hiyo ilikuwa ni chorus katika wimbo wa Mandela nakumbuka ilikua 1990 wakati hayati Mandela alipotembelea TZ mara aya kwanza tangu alipoachiliwa huru na makaburu
 
walisemaaaaa dalili ya mvua ni mawinguuuuu,
nilimyempenda kanitoroka mamaaaaaaaaaaX 2

Nakumbuuka kuna mama yangu mdogo ndo alikuwa anaimba wakati huo enzi la club raha leo shooooooooooooooooooooo!

Vitukoo,vituko vya bibi yulee
Sitaweza kusahau mimi ooh
Mamaa eeh,
Sitaweza kusahau mimi ooh
Edy eeh
Alikuwa kama helikopta
Ndege isiyochagua mahali pa kutuaa eeh
Kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oh
Ana bwana mmoja ama wawili
La la la la,nifanye nini oh mama..haya Twilumba nimekugongea bridge hiyo nipokee na hiyo chorus tena ha ha haa,mambo matamu haya,huu uliitwa muziki,siku hizi kuna usanii.
 
Last edited by a moderator:
Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,
japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,
(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,
Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,
Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,
kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,
kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,
kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,
hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,
hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2
Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2
chorus:
walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,
(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,
(chorus)
Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,
 
Eeee wene weangu shakaza. Nina makosa ani weangu shakaza.
gouni ingwe weangu shakaza. weangu wedi naawanyiika shakaza puke. puke puke
Kusheghuighwa kohe ni kufa ughumba naneeee


Nakusikia kwa sauti ya Eddy Sheggy....cheza basi kidogo.
 
walisemaaaaa dalili ya mvua ni mawinguuuuu,
nilimyempenda kanitoroka mamaaaaaaaaaaX 2

Nakumbuuka kuna mama yangu mdogo ndo alikuwa anaimba wakati huo enzi la club raha leo shooooooooooooooooooooo!

Anaitwa edsoni shenyagwa
 
Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa....
Na kisirani cha kufokewa na bosi....
Nahitaji wa kunibembeleza....
Si kwa maneno ila kwa kunitomasatomasa....
Kwa mikono laini yenye bangili....
Rip Shekabughe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom