Jina Dkt–Muhimbili aliyetaka kuhonga timu ya Makanikia

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,365
2,000
GTs,

Hivi huyu Dkt aliyetaka kuwahonga ile timu ya ukaguzi anaitwa nani?
Je, hawezi kuwa moja ya watoto wa wanasheria waliopita?
Mimi nafanya dodoso hapa,

Kuna jina moja la Mwanyika, huyu Johnson Paulo Mathias Mwanyika alishawahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, pia kuna jina hilo hilo Mwanyika anacheo fulani huko migodini.

Ila kuna mkaka mmoja anaitwa pia Dkt Moris Mwanyika nadhani atakuwa anafanya kazi Muhimbili.

Je, ndiye anaweza kuwa alitaka kuokoa jahazi la baba yake mzee Johnson Paulo Mathias Mwanyika.

Jibu hilo litakuwa ndiyo kama kuna mtu ana info hapa aongezee nyama kama ifuatavyo.

Je, Dkt Mwanyika, Mwanasheria mkuu wa zamani mzee Johnson Paulo Mathias Mwanyika ni baba na mtoto?

Naomba kuwasilisha wadau
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
14,340
2,000
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
..Mwanyika anayetajwa-tajwa anafanya kazi Barick.

..Johnson Mwanyika walimtoa kafara tu wakati wa Richmond but he had nothing to do na ufisadi ule.

..uzalendo wa Johnson Mwanyika unajulikana tangu yeye na William Sekule walivyokuwa mawakili upande wa mashtaka/serikali wakati wa kesi ya uhaini ya miaka ya 80/90.
 
VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,017
2,000
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders

Hivi tumekuwa na roho ngumu za kinafiki kwa nini? nimemsikia kada mmoja wa ccm akihojiwa Redio Tanzania au TBC akidai wale wote waliotajwa na tume ya pili waondoke haraka kwani wataendelea kupaka chama matope.

Hivi kwa nini hatupendi kusema ukweli na matokeo yake tunaendeleza unafiki? hao wote wanaotajwa hapo walikuwa ni viongozi na makada wa ccm amabo walikuwa wanasimamia kile kilichokuwa kinatekelezwa na serikali ya ccm na kupitishwa kwa miswaada ya dharula iliyoletwa na serikali ya ccm.

Sheria zote za uchimbaji madini na hata ile iliyopitishwa kwa hati ya dharula zilipitishwa kwa sauti za ndio na wabunge wa ccm tena wakiwakejeli na kuwapiga vijembe wabunge wa upinzani. Leo ingewezekana Rais kuwaomba radhi wananchi kwa niaba ya chama chake ambacho kimewaibia watanzania miaka yote maana hakuna chama kingine ambacho kimewahi kutawala nchi hii.

Hilo swala la kupitia upya sheria mbalimbali za madini ndicho Lissu na Mnyika wameyarudia mara zote wakadhihakiwa na wabunge wa ccm, hivi hizo sheria zinazoenda kufanyiwa marekebisho wabunge wa ccm watasema nini wakati walizipitisha kwa mbwembwe na kuwadharau wapinzani waliona hazipo vizuri?
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,387

Wakimgusa JK au Mkapa nitakupa offer wine baridi ujizimulie wakati una subiri episode 3 ya Makinikia
 
NnyaMbwate

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,652
2,000
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders
Hebu tujaribu kuwa wazalendo kwa nchi yetu. Sasa kama miongoni mwa hao CCM amejitokeza kuokoa utajiri wa nchi yetu, bado mnataka tuwaachie walafi watumalize kabisa? Rais ana nia njema na nchi hii, na hii inaonesha kuwa haya mambo yalikuwa yanamkera na hakuwa na namna nyingine kwa sababu alikuwa ni sehemu ya serikali.

Mh. Rais amepata nafasi ya kulishughulikia hili jambo basi sisi tumuunge mkono!
 
papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,497
2,000
Sizonje ni muongo wa kutupa anajua kucheza na akili za wdanganyika! Hata issue ya kafumu ni uongo mtupu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom