Jimbo la Segerea: Liwike lisiwike kutakucha tu!!

Jimbo la Segerea: Liwike lisiwike kutakucha tu!!

Status
Not open for further replies.
Matola,
Katika hali ya kawaida mwanzisha thread ndiye anatakiwa awe eneo la tukio kwa ajili ya kutoa habari. Sasa hili wazo lako naona halipo kiuhalisia maana utakuwa unaendeleza tabia zilezile za baadhi ya member ambao wanakurupuka kuanzisha thread alafu wanategemea wengine wajaze habari. Mi nashauri mtu atakae kuwa Mahakamani ndiye aanzishe thread ya Live.

Invisible kazi yake iwe kumodarate thread kwa kuidentify member yupi yupo mahakamani then aifanye thread yake ndiyo ibebe kichwa cha thread zote zitakazokuwa zinajitokeza. Tuendeleze utamaduni wetu wa kila member kuwa huru kuanzisha thread na tuwaache moderators wafanye kazi yao.

swadakta tumbiri. ambaye atakuwa yupo kortini na thread yake imekidhi viwango,ndo aanzishe thread km vile alivyokuwa anafanya isango kule kortini singida.
 
Wakuu nawasalimu wote kwa jina la aliye mkuu,
Sikuwa na ulazima wa kuanzisha thread hii lakini nimelazimika kuianzisha thread hii mapema ili kuondoa mikanganyiko isiyokuwa na ulazima

Ikumbukwe kesho ndio tarehe 2 may, kwa sisi wapiga kura wa Segerea tunategemea kutendewa haki yetu na Mahakama kuu kuhusu kesi ya Fred Mpendazoe vs Makongoro Mahanga.

Sasa basi si nia yangu kupendekeza udikteta au ukiritimba wa Habari, bali kutokana na mfumo mbovu unaooneshwa na baadhi ya Member wenzetu hapa katika kupashana habari napendekeza hivi:
Invisible kesho ndiyo abebe jukumu la kuanzisha thread kwa Mtindo wa LIVE ili members wengine ndio watakuwa wanatupia habari kwenye thread, kwa Sababu kesi hii iko Mahakama kuu Dar es salaam nina uhakika watu wengi watakuwa na access ya kuleta habari Immediate.
Hayo ni maoni yangu tu wadau, au mnasemaje?

Pamoja na yote hukumu hajajulikana itasomwa ukumbi gani hivyo wadau wetu mnatakiwa kuwahi kabla
10.00 asubuhi pale mahakama kuu ili kujua kama tutakuwa pa au kule Mahakama ya
Biashara ukumbi uleule tuliotumia wakati wa kesi.:bange::bange::bange:
 
Mkuu Matola hoja yako ina mashiko sana,japo maelezo ya Feedback pia yanajitosheleza,mimi ninamwomba Invisible aseme hapa je hiyo kesho atakuwepo mahakamani???ili kama hatakuwepo basi members wengine watakao kuwepo mahakamani waweze kutuhabarisha.
 
Mkuu Matola umenena vyema kwa kuona hii shida ambayo tunaipata hapa siku hizi. Members wamekuwa wakianzisha threads nyiingi ambazo zinafanana ama kuongelea jambo moja hadi mtu unashindwa ufungue thread gani ili upate habari sahihi.Kwanza kabisa nadhani members wawe waungwana ili kabla ya kuanzisha thread wadurusu kuangalia kama hakuna thread inayofanana na anayotaka kuianzisha. Pili, kama kwa bahati mbaya kuna member ameanzisha thread ambayo tayari ipo basi moderators watusaidie kuziunganisha mapema. Nakuunga mkono kwamba kesho Mod mmoja aanzishe thread ambayo hata watu wengine ambao wako mahakamani watapost humo. Pia katika matukio makubwa ambayo yanajulikana kuwa yatatokea siku fulani, mfano hukumu basi Mod aanzishe thread mapema ili iwe ndipo mahala pa kupata taarifa na kila post iende huko. Nadhani tutapunguza thread zinazofanana ma pia itatusaidia kupata habari from one centre.
 
Last edited by a moderator:
well said mkuu, maana bila hivyo kesho humu itakua vurugu kila mmoja atajifanya ni reporter.. Invisible tunakuomba mkuu kama hautajali ufanye kama mkuu Matola alivyotoa pendekezo

Excellent,waiting you 2morrow for the updates.
 
Hoja yako ni nzuri sana @kimbunga na ninakubaliana na wewe kabisa ...cha msingi ambacho ni kama mapendekezo LEO @invisible atuaarifu kabisa headiing ya thread ili iwe rahisi kuitafuta kwani thread zinakua nyingi mno halafu nyingi yazo hazina cha maana wwala hazi-apdetiwi inakua kero sana hasa kwa slow internet connections kufungua page hukuti cha maana una-cancel unafungua nyingine hukuti kingine cha maana una-cancel tena yaani kero tupu...

Kingine ambacho nnakiona hapa ni suala la usumbufu wa NEW MEMBERS wa JF.. wengi wao huwa thread nyingi ni za hovyo hovyo sana.. zimejaa hisia na stori za vijiweni na fikiri kuna haja ya kale kautaratibu ketu ka zaman ka ku-post profile yake huyu jamaa anapoanzisha uzi ili iwe rahisi kujua ni NEW COMMER ... wengi wao hawana critical thinking na wengi wanakua na upepo wa KI-FACEBOOK zaidi.
thanx
 
Naona kesho tusubiri utitiri wa mithread umu
 
well said mkuu, maana bila hivyo kesho humu itakua vurugu kila mmoja atajifanya ni reporter.. Invisible tunakuomba mkuu kama hautajali ufanye kama mkuu Matola alivyotoa pendekezo

na wewe Manyanza jana ulianzisha kauzi kaajabu ajabu kuhusu kesi ya biharamulo halafu ukatokomea
 
Last edited by a moderator:
Manyanza

Mimi naona TUMBIRI yuko sahihi, mtu atakayekuwa mahakama ndiye aanzishe LIVE coverage, unakumbuka wewe Manyanza jana ulianzisha thread ya hukumu ya Biharamulo na hukuwa mahakamani matokeo yake ukashindwa ku-update? hukuonekana hadi matokeo yakatoka usiku saa 2.30. Mbaya zaidi thread yako ilikuwa ni quotation ya post ya QUALITY, sasa kulikuwa na sababu gani ya wewe kukimbilia kuanzisha ile thread, hayo ndiyo anayoyasema TUMBIRI.

Mwisho, JF ni ya wote tusimtegemee sana Invisible ndiye aanzishe thread huwezi kujua mipango yake ya kesho anaweza asiwepo mahakamani au asiwepo Dar kabisa au akachelewa, kwa hiyo akichelewa na mimi nimewahi nimsubiri hadi yeye aanzishe ili mimi ni comment, logical? Kama Invisible atawahi mahakamani na kuanzisha well and good ila zaidi yeye aendelee ku monitor thread zitakazoanzishwa baadae wala hakuna haja ya kumkumbusha ni kazi yake.

Mkuu Feedback,
Nakupa tano Jembe langu! Sina cha kupunguza wala kuongeza..
 
Last edited by a moderator:
Niko karibu sana na watu wa CCM na nimefanikiwa kuingiza viongozi 3 kwenye uchaguzi wao wa juzi, na hawa wapo CCM kwa kazi maalum.

Juzi alikuja katibu wao wa mkoa wa CCM na ameshatoa maagizo kwa matawi ya CCM kujiandaa na uchaguzi mpya Jimbo la Segerea, hili jambo wala halina siri yoyote kwa sisi tuliyopo hapa Jimboni.

Na ningependa kuwatoa hofu wale wote wenye wasi wasi wa kuchakachuliwa matokeo hakuna kitu cha namna hiyo, Jaji hawezi kujivunjia heshima kwa viwango hivi vya kesi ya Makongoro.
Mkuu Matola wewe unatisha sana kamanda.
 
Last edited by a moderator:
Niko karibu sana na watu wa CCM na nimefanikiwa kuingiza viongozi 3 kwenye uchaguzi wao wa juzi, na hawa wapo CCM kwa kazi maalum.

Juzi alikuja katibu wao wa mkoa wa CCM na ameshatoa maagizo kwa matawi ya CCM kujiandaa na uchaguzi mpya Jimbo la Segerea, hili jambo wala halina siri yoyote kwa sisi tuliyopo hapa Jimboni.

Na ningependa kuwatoa hofu wale wote wenye wasi wasi wa kuchakachuliwa matokeo hakuna kitu cha namna hiyo, Jaji hawezi kujivunjia heshima kwa viwango hivi vya kesi ya Makongoro.

mkuu sio uungwana m2 mmoja kuwa na kadi za vyama viwili tofauti huo ni unafiki,kama umeamua kuamia chadema kimoja basi rudisha kadi ya ccm...achana na siasa za kuchumia tumbo zitakuponza.

Ni ushauri tu,pia mnaweza kumshauri na Slaa arudishe kadi ya CCM kama ameenda uko kimoja na amejisahau alichotumwa
 
Vinega wa Cdm mnamatatizo sana..yani mwenzenu anajisifia yuko karibu na CCM kama Zito na nyie mnachekelea.
CCM ndiyo mtanijuwa mimi ni nani sasa, nimeweka mapandikii yangu ndani ya CCM, nyinyi wanya nje mtajiju!!
 
Mods nawaomba sasa hii thread iwe closed au ipelekwe kwenye trash. leo ni tarehe 2 tayari!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom