Jimbo la Musoma Vijijini Wananchi Waendelea Kutatua Matatizo ya Elimu Vijijini Mwao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI - WANANCHI WAENDELEA KUTATUA MATATIZO YA ELIMU VIJIJINI MWAO

Wananchi ndani ya Vijiji 68 vya Musoma Vijijini wamekua na mwamuko mkubwa sana kushirikiana na Serikali, na Wadau ya Maendeleo, kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili vijijini mwao.

Baadhi ya matatizo hayo kwa upande wa Elimu ya Sekondari ni:
umbali mrefu unaotembewa na baadhi ya wanafunzi kwenda masomoni

Mirundikano ya wanafunzi madarasani

Kijiji cha Wanyere chaamua kujenga Sekondari yake
*Kijiji cha Wanyere ni moja ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Suguti yenye Sekondari moja tu ya Kata, Suguti Sekondari.

*Wanafunzi wa Kijiji cha Wanyere wanalazimika kutembe umbali wa takribani kilomita 18 kwenda masomoni kwenye Sekondari yao ya Kata (kwenda na kurudi, km 36!)

*Ujenzi umeanza, Mbunge wa Jimbo aanza kuchangia
Wananchi kutoka Vitongoji sita (6) vya Kijiji cha Wanyere wameanza ujenzi wa Sekondari yao.

Kazi walizoanza kufanya ni hizi zifuatazo
  • Kusafisha eneo la ujenzi
  • Kusomba mchanga trip 6
  • Kusomba mawe trip 7

Mbunge wa Jimbo aanza kuchangia
Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia ujenzi huo kwa kutoa SARUJI MIFUKO 100 (mia moja)

Michango ya ujenzi ipelekwe:
*Mwenyekiti wa Kijiji cha Wanyere
+255 787 295 178

*Akaunti ya Serikali ya Kijiji:
Benki: NMB
Na: 30302301050
Tawi: Musoma
Jina: Serikali ya Kijiji cha Wanyere

MAOMBI KUTOKA KIJIJI CHA WANYERE
*Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa - hayo ni maombi ya Wanakijiji kwetu sisi sote.

Sekondari mpya zinazojengwa kwa sasa Jimboni mwetu, na tumepanga zifunguliwe mwakani (Januari 2024) ni za vijiji vya:
*Muhoji
*Wanyere
*Kisiwa cha Rukuba

Jimbo lina Kata 21, Sekondari za Kata 25, na za Binafsi 2.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
wwww.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumapili, 30.4.2023
 
Back
Top Bottom