Jimbo la Mbarali litachukuliwa na upinzani kisa GN 28

fullcup

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
806
2,182
Kesho tarehe 5/07/2023 ndio siku ambayo mwili wa aliyekua mbunge wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Francis Mtega utazikwa huko kwao Ludwa. Kuzikwa kwake kutafungua nafasi ya kufanyika Kwa uchaguzi mdogo Ili kuziba nafasi yake.

Kufuatia msimamo wa serikali wa kuondoa wananchi maeneo mbalimbali ya kiuchumi hasa mashamba ya mpunga ya Madibira phase 2, mwanavala, mnazi na mahongole umeongeza chuki ya wananchi dhidi ya Chama Cha mapinduzi. Ikimbukwe waziri mkuu alikua mbarali na kuifuta GN 28 kwahiyo wananchi wanaondolewa Kwa Sheria iliyofutwa jambo ambalo limepelekea uwepo wa msururu wa kesi mahakamani na vikao vingi vya usuruhishi.

Kwa miaka mingi tangu 2008 CCM ilikua ikitumia GN 28 kujipatia kura za kutosha Kwa madai ya kuitetea mbarali dhidi ya Sheria Hiyo. Kwahiyo Kila ukikaribia uschaguzi suala Hilo lilikua likiibuliwa na CCM wanaliweka sawa wanapita. Mfano 2008, 2015,2019, na 2022. Lilipoibuliwa 2022 inasemekana ilipangwav2024 warudishiwe wananchi Ili 2025 kura zizolewe za kutosha. Bahati mbaya imetokea ajali na uchaguzi lazima ufanyike wakati ambao suala hili limepamba moto na kitaifa Kuna suala la bandari.

Kwasasa mbarali chama Cha mapinduzi hata angegombea Spika Dr. Tulia na upinzani agombee kijana wa bodaboda uchaguzi utakua mgumu Kwa Spika. Cha kufanya labda srikal ilipe fidia Kwa haraka Kwa wahanga wa maeneo hayo ( jambo lisilowezekana maana hata tahimini maeneo mengi bado), itangaze kurudisha maeneo Kwa wananchi kuelekea uchaguzi mdogo.
 
HAPANA SIO KWELI, CHADEMA wakienda kwenye Uchaguzi watashinda kwasababu ya uharamia wa majizi ya CCM including hio GN 28. I mean GN 28 ni tone la maovu ya CCM kwenye bahari ya ujangili, wizi, na uporaji
 
Sidhani kama CDM itashiriki, mshiriki mkubwa wa hizi chaguzi ni ACT wazalendo japo tangu aanze kushiriki chaguzi za marudio hajawahi kufanya vizuri sehemu yeyote ile, naamini na huu ukitangazwa atashiriki tu

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kwaakili ya mbowe anaweza kususa maana chaguzi zote za madiwani kasusa huu wa ubunge unatofauti gani? Kikubwaa maadam ACT inakubalika mbarali basi zito asimamishe mtu sahihi itatosha
Hata wagombea wa CDM wanaweza kuhamia huko, kwasasa hata Gamdust Haji anaweza kuchukua Kama akigombea upinzani peke yake maana yule mgombe kampeni zake anazijua mwenyewe.
 
Huu uchaguzi watashiriki na vikao vya ndani vimeshaanza kufanyika na ukizingatia 2020 Magufuli aliiokoa Sana mbarali ila kwasasa njia nyeupe.
Mkuu mimi naongea na hao watu wenyewe wananiambia hakuna mpango wowote mpaka sasa. Kwa mujibu wa habari za leo.

Na hawa ni watu wanaoniheshimu sana na wananitegemea kuwa sehemu ya fundraising, so hawana sababu ya kunidanganya, in fact wana kila sababu ya kuniambia as soon as possible.

Msimamo wa CHADEMA mpaka sasa ni kususia uchaguzi.
 
Kesho tarehe 5/07/2023 ndio siku ambayo mwili wa aliyekua mbunge wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Francis Mtega utazikwa huko kwao Ludwa. Kuzikwa kwake kutafungua nafasi ya kufanyika Kwa uchaguzi mdogo Ili kuziba nafasi yake.

Kufuatia msimamo wa serikali wa kuondoa wananchi maeneo mbalimbali ya kiuchumi hasa mashamba ya mpunga ya Madibira phase 2, mwanavala, mnazi na mahongole umeongeza chuki ya wananchi dhidi ya Chama Cha mapinduzi. Ikimbukwe waziri mkuu alikua mbarali na kuifuta GN 28 kwahiyo wananchi wanaondolewa Kwa Sheria iliyofutwa jambo ambalo limepelekea uwepo wa msururu wa kesi mahakamani na vikao vingi vya usuruhishi.

Kwa miaka mingi tangu 2008 CCM ilikua ikitumia GN 28 kujipatia kura za kutosha Kwa madai ya kuitetea mbarali dhidi ya Sheria Hiyo. Kwahiyo Kila ukikaribia uschaguzi suala Hilo lilikua likiibuliwa na CCM wanaliweka sawa wanapita. Mfano 2008, 2015,2019, na 2022. Lilipoibuliwa 2022 inasemekana ilipangwav2024 warudishiwe wananchi Ili 2025 kura zizolewe za kutosha. Bahati mbaya imetokea ajali na uchaguzi lazima ufanyike wakati ambao suala hili limepamba moto na kitaifa Kuna suala la bandari.

Kwasasa mbarali chama Cha mapinduzi hata angegombea Spika Dr. Tulia na upinzani agombee kijana wa bodaboda uchaguzi utakua mgumu Kwa Spika. Cha kufanya labda srikal ilipe fidia Kwa haraka Kwa wahanga wa maeneo hayo ( jambo lisilowezekana maana hata tahimini maeneo mengi bado), itangaze kurudisha maeneo Kwa wananchi kuelekea uchaguzi mdogo.
Acha uongo. CCM inakubalika mno hayo maeneo
 
Tanzania kwa sasa hakuna chaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Nitawashangaa sana cdm kama watajitokeza kushiriki chaguzi hizi za kihayawani.
 
Back
Top Bottom