Jimbo la Iramba ni mojawapo ya Jimbo la Ubunge lililopo Mkoa wa Singida. Mwanzani Wilaya ya Mkalama ilikuwa pia ni Jimbo la Ubunge lililojulikana kama Iramba Mashariki.
Kwa maana hiyo Wilaya ya Iramba pamoja na ukubwa wake jimbo lake la Uchaguzi ni moja tu - ajabu sana!
Historia ya kisiasa kwa Jimbo na Wilaya hii inaonekana kuwa na wanasiasa wasiopata mafanikio sana sababu wengi wao wamekuwa wabinafsi.
Viongozi wa kisiasa na wale wasio wa kisiasa wamekuwa wakifika nafasi za juu basi kiburi kinawajaa - wanajiona wao ndiyo wao na wanakwama kabisa kuunganisha wanachi.
Ukiacha ubunge wa Nalingigwa na Nkurlu waliofuatia kama Nalaila Kiula walishindwa kabisa kuuunganisha wananchi.
Nalala Kiula alikuwa mara zote akinunua ubunge na kuwatelekeza watu wake na kujikweza kwa kufanya mambo ya Kitaifa alipokuwa Waziri na hivyo kufanya asionekana kuunganisha watu na kuiletea Iramba maendeleo.
Hakupenda kupata upinzani wowote na ndiyo maana alipoanza kupata misukosuko wanaIramba walimshiti na akapotea kweli.
Baada ya Kiula alifuata Shango ambaye alitawala kwa maneno ya kukashifu kashifu tu na hata Juma Kilimba alipoingia mambo yakawa yale yale tu - tena huyu ndiyo mbaya kabisa.
Mwigulu alipopata nafasi mwanzoni akiwa kijana mwenye ari kubwa akaonesha dalili za kuweza kuunganisha Iramba na kuiletea maendeleo.
Mara naye akatekwa na siasa za Kitaifa na kutamani Urais kwa udenda haraka kadri alivyoweza ilihali akiwa na muda mfupi tu katika Ubunge.
Hadi ikasemekana eti ana undugu na Ridhiwan Kikwete - ajabu kweli. Kwa sasa anatapatapa na amekuwa na kakikundi kadogo ka kisirisiri maeneo ya karibu na kwao Makunda, Ndago na Maluga akifikiri kuwa kanaweza kuiunganisha Iramba na kumpatia ushindi.
Mbaya zaidi amekuwa akisisitizwa na kupewa nafasi katika vikundi vivavyoangalia maendeleo ya Iramba lakini anavikwepa kwepa tu.
Ukweli Iramba inakosa sana mtu wa kuiunganisha pamoja na kuwa ina watu wengi wenye uwezo wa kuiunganisha na kusababisha maendeleo.
Mipango yote ya Iramba yenye mafanikio imekuwa ni ile ya Kitaifa na hamna hata kitu Mwigulu, Nalaila, Kilimba wala Shango wanaweza kujivunia waliunganisha wana Iramba wakapiga hatua za kimaendeleo zinazotokana na juhudi za wabunge wao.
Ndiyo maana Mwigulu baada ya kutolewa Uwaziri huko Bungeni kama mpole utafikiri bweha kanyeshewa mvua.
Bila kujirekebisha ukweli ubunge ushaota mbawa!