Sasa hivi Jiji la Mwanza linaanza kupendeza. Barabara ya uwanja wa ndege taa za barabarani zimewekwa na zinawaka hadi raha. Kenyatta road nayo si haba zinawaka kutoka mjini hadi Mswahili. Kwa kweli tuupongeze uongozi wa Jiji na Tanroad kwa kazi njema. Tatizo limebaki tu pale city Centre ndio giza totoro. Naomba mipango ifanywe kuhakikisha taa zinafungwa na kuwaka ili kuimarisha usalama kwenye Jiji hili kubwa la pili nchini Tanzania.Taa za barabarani Kenyatta road zimeishia voil tu. Hata Mkuyuni hazijafika ! Sijui tatizo ni nini ?