nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,033
- 2,949
Inasikitisha kuona kwamba Mwanza jiji la pili kwa ukubwa nchini Tanzania halina taa za barabarani mitaa yote, katikati ya Jiji ni giza tupu, barabara zote kuu tatu za kutoka na kuingia Jijini (Nyerere, Kenyatta na ile iendayo uwanja wa ndege) zote ni giza tupu.
Inafikia mtu unajiuliza hivi uongozi wa Jiji hili na ule wa Manspaa ya Ilemela unakwama wapi? Mbona miji midogo kama Geita na Kahama kwa sasa zina taa za barabarani?
Kwa kweli ni aibu kwa Jiji kama hili kukosa taa hizi hata maeneo nyeti kama stendi kuu ya mabasi Nyegezi n.k. Nadhani wakati umefika sasa wa viongozi wa mkoa, jiji na Manspaa ya Ilemela kuondoa kero hii.