Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 5,976
- 11,982
Tanzania miji yote ina ujenzi holela tu ila kwenye jiji la Mbeya tumechemka 😂😂😂
Actually sitaki kuonesha picha za ujenzi holela hapa Mbeya lakini ukiingia Google, search tu "Mbeya" halafu nenda kwenye images, utakachokiona ndio Mbeya iko hivyohivyo
Hili suala linaniuma mno, kwa sababu hapa Mbeya kuna mandhari nzuri sana, pia kwa maeneo niliyotembea sijawahi kuona sehemu yenye hali ya hewa nzuri kama Mbeya (hapa naongelea Mbeya mjini)
Huku kuna ardhi yenye rutuba, hali ya hewa ya baridi kidogo, msimu wa mvua zinanyesha za kutosha, pia kuna milima mizuri sana. Yani huku Mungu alipapendelea
Lakini sisi Wabongo tulivyoanza tu kujenga Mbeya, tukaharibu kabisa.
Kwa sehemu ambayo ni nzuri hivi, hatukupaswa kujenga kiholela, tena nyumba za matofali mabichi
Hebu angalia Uzunguni na Uhindini, huku walijenga wazungu. Pamepangiliwa vizuri hadi raha, ukipita huku pamependeza mno mpaka ukishuka Jakaranda Street nako mambo ni safi, lakini ni eneo dogo tu
Lakini sasa karibia 80% ya Mbeya ni ujenzi holela, Angalia Mabatini, Nzovwe, Iyunga kote huko na viunga vyake Ikuti, Inyala na Kalobe ni uswazi tupu, ukitoka Mwanjelwa kwenda nanenane hapa kati Ilomba ni uswazi tupu, watu wanajenga milimani hadi milima inapoteza mvuto. Trust me, milima ya Mbeya ni mizuri sana, lakini tusipoangalia itazidi kuchafuka siku zinavyozidi kwenda
Pia haya malori ya mizigo, ni heri yangetafutiwa njia ya kupita tu, yasikatize hapa mjini maana ndio chanzo cha msongamano na ajali kuwa nyingi hapa Mbeya.
Mi naona Mbeya ingejengwa vizuri, plus ile milima, mvua, kabaridi na ukijani ingekuwa ni Switzerland ndogo kabisa. Lakini ona tumejenga uswazi tu. Ardhi ya Mbeya inatudai Watanzania, hatujaitendea haki kwa kweli. Sehemu nzuri kama ile tumeiharibu haribu tu
Kwa nature kitu kibaya Mbeya ni vumbi tu msimu wa Kiangazi, vingine vyote viko poa, sisi ndio tunapaharibu.
Ila sio Mbeya yote ni mbaya, kuna maeneo Isiese, Forest, Jakaranda, Uzunguni, kipande kidogo cha Mafiati pale maeneo ya CUoM, maeneo ya BOT, JB na kwa huku Iwambi kuna mtaa unaitwa Maziwa, ni mpya watu wanajenga sasahivi, (huku Maziwa watu wanajenga nyumba za maana kama za Ulaya vile, mpaka miaka 5 ijayo patapendeza sana)