Jiji la Dar kufumuliwa, Kupangwa upya

Jiji la Dar kufumuliwa, Kupangwa upya

JIJI.jpg

Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kisha kupangwa upya, baada ya Ramani ya Mipango Mji (Master Plan) mpya kukamilika.

Akizungumza na Wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi jijini Dar es Salaam leo, Waziri Lukuvi amesema ameagiza mpango huo utakamilika kabla ya Julai ili mpango wa upangaji upya jiji hilo uanze.

Pia Waziri Lukuvi amesema kuwa nyumba zianazojengwa kwa sasa na kampuni na mashirika ya Umma, likiwemo Shirika la Nyumba la Taifa sio za bei nafuu kulingan na hali halisi ya kipato cha Watanzania wengi, na badala yake ameagiza NHC liwakusanye wabunifu wa nyumba za bei nafuu watoe muundo ili Watanzani ndio waamue aina ya nyumba za bei nafuu.

Source: Mwananchi
hatutakubali tena kusumbua wananchi kitapeli , ule mradi wa manzese kwa mfuga mbwa mmeishia wapi ?
 
Suala ni
Naona kama viongozi wetu wameishiwa uwezo wa kufikiri. Kuna haja gani ya kupoteza hela nyingi kuvunja na kujenga upya, kwanini wasitoke nje ya jiji la Dar, wanaweza kwenda Pwani, Tanga, mtwara ama Lindi wakajenga jiji lingine la kisasa na kuliacha jiji la Dar baadae litageuka kuwa jiji la kihistoria na kubaki na sura yake ya asili. Nimefika London, hakuna majengo marefu kama yalivyo Dubai lakini wana majengo mengi ya kale na ni masafi sana kwani yanatunzwa vizuri. Huko vijijini watu hawana maji wao wanalazimisha kutengeneza hapohapo Dar wanaposhinda hao wanaosema wacheza pooltable.
Suala ni majengo kwani?
 
Masikini kila sehemu huwa hapendeki mkuu.

Hata na ndugu zake, achilia mbali serikali

Haina maana kutengeneza jiji kwa kuwaharibia watu maisha yao mkuu, real estates zinabumaga hata US, huwez amino kuwa bei ya nyumba Dar ni ghali kuliko hata US, na hii ilisababishwa na mijizi kuiba pesa na kuzigawa bila hata kutumia akili,
Ikawavutia mabwenyeye wa mafuta wakaanza kushusha maghorofa ya nguvu , sasa hivi fleti nyingi za kkoo bei imeshuka na nyingine zipo tupu........
Real estate developer kama NHC anauza nyumba ghali kuliko private developers....uhuni at its best.........sijawah kuhitaji na wala sina shida ya nyumba za hao walafi, tatizo ni namna wanavyosumbua wananchi kwa mambo yasiyo na tafiti za kutosha.
 
Kwa nini msijenge mji mpya nje ya Dar maeneo kama Bagamoyo au kuendeleza miji mingine na kuepuka hii gharama na usumbufu kwa serikali na wakazi wa Dar?
Mnakwenda nje kila siku lakini hamjifunzi kwa majiji kama Delhi?
Mimi napata shaka kama kweli viongozi wetu mmekosa weledi au ni makusudi tu mnacho mnachokitafuta Dar manake hii awamu ya 5 inatawala Dar tu!
Kila siku Dar hiki,Dar kile Dar Dar..Dar...mji una population growth ya kutisha among the top five in Africa badala ya kufikiri kuutanua bado mnang'ang'ana na Manzese wee..mnachokitafuta mtakipata.
Dar itageuka zigo la misumari kwenu very soon!
 
  • Thanks
Reactions: 911
Naona kama viongozi wetu wameishiwa uwezo wa kufikiri. Kuna haja gani ya kupoteza hela nyingi kuvunja na kujenga upya, kwanini wasitoke nje ya jiji la Dar, wanaweza kwenda Pwani, Tanga, mtwara ama Lindi wakajenga jiji lingine la kisasa na kuliacha jiji la Dar baadae litageuka kuwa jiji la kihistoria na kubaki na sura yake ya asili. Nimefika London, hakuna majengo marefu kama yalivyo Dubai lakini wana majengo mengi ya kale na ni masafi sana kwani yanatunzwa vizuri. Huko vijijini watu hawana maji wao wanalazimisha kutengeneza hapohapo Dar wanaposhinda hao wanaosema wacheza pooltable.
Sawa kabisa, ungefika mji wa oxford ndo utashangaa majengo ya miaka 1500BC bado yapo na mji uko saafi.
 
Ok, nilidhani Kigamboni ndo ilikuwa sehemu lengwa ya sura mpya ya jiji la Dar. Sasa hv Rais mpya, mawaziri wapya wana mawazo tofauti na master plan mpya! Wa-Tz bwana, unless neno 'kufumuliwa' nimelielewa tofauti.
 
Naona kama viongozi wetu wameishiwa uwezo wa kufikiri. Kuna haja gani ya kupoteza hela nyingi kuvunja na kujenga upya, kwanini wasitoke nje ya jiji la Dar, wanaweza kwenda Pwani, Tanga, mtwara ama Lindi wakajenga jiji lingine la kisasa na kuliacha jiji la Dar baadae litageuka kuwa jiji la kihistoria na kubaki na sura yake ya asili. Nimefika London, hakuna majengo marefu kama yalivyo Dubai lakini wana majengo mengi ya kale na ni masafi sana kwani yanatunzwa vizuri. Huko vijijini watu hawana maji wao wanalazimisha kutengeneza hapohapo Dar wanaposhinda hao wanaosema wacheza pooltable.
yeap ni kweli kabisa tatizo kubwa viongoz wetu wengi wana ufinyu wa akili kubadili dar es salaam ni ndoto ya linacha na kutia loss serikali kikubwa ni kuweza kuhama dar es salaam na kutafuta chanzo kingine cha kuweza kusababisha dar watu wapungue
 
Naona kama viongozi wetu wameishiwa uwezo wa kufikiri. Kuna haja gani ya kupoteza hela nyingi kuvunja na kujenga upya, kwanini wasitoke nje ya jiji la Dar, wanaweza kwenda Pwani, Tanga, mtwara ama Lindi wakajenga jiji lingine la kisasa na kuliacha jiji la Dar baadae litageuka kuwa jiji la kihistoria na kubaki na sura yake ya asili. Nimefika London, hakuna majengo marefu kama yalivyo Dubai lakini wana majengo mengi ya kale na ni masafi sana kwani yanatunzwa vizuri. Huko vijijini watu hawana maji wao wanalazimisha kutengeneza hapohapo Dar wanaposhinda hao wanaosema wacheza pooltable.
Asante sana kwa uchambuzi yakinifu. Mimi naona MAGu aanzishe tovuti ambayo itakuwa inaweka inputs za changamoto zinazowakabili ili wazawa waweze kutoa ushauri. Well said bro, there is no need to demolish Dar Es salaam, but it make sense for them to relocate in places like Kibaha and so forth.
 
Mipango na ubunifu wa Lukuvi sijui anaitoa vitabu gani, nadhani bado kichwani mwake ana maendeleo ya enzi za Mesopotamia ya kale.
 
Achana na DAR mh. Waziri Jenga Satellite cities hata 5 hivi kwa nini Rasilimali na Nguvu nyingi kupanga Dar matokeo yake ni kuumiza wananchi. Kwanza Tanzania hatuna mji uliopangwa kwa nini usianzishe satellite cities hata 5 Tuna maeneo mengi Sana karibu na DAR.
Mkuu hawa bata hawana akili hizi bado wako mikaa ya nyuma sana aise.
 
Kwani lazima watu muendelee kusagana Dar es salaam?
Nchi yetu ina eneo kubwa sana kijiografia kwa nini tuendelee kujibana as if tupo Rwanda? Ni muda wa kufunguka na kuutumia uwanja wote.
 
Serikali ndiyo inayowafukuza watu kwenda mijini halafu inajifanya kulalamika.
 
Naona kama viongozi wetu wameishiwa uwezo wa kufikiri. Kuna haja gani ya kupoteza hela nyingi kuvunja na kujenga upya, kwanini wasitoke nje ya jiji la Dar, wanaweza kwenda Pwani, Tanga, mtwara ama Lindi wakajenga jiji lingine la kisasa na kuliacha jiji la Dar baadae litageuka kuwa jiji la kihistoria na kubaki na sura yake ya asili. Nimefika London, hakuna majengo marefu kama yalivyo Dubai lakini wana majengo mengi ya kale na ni masafi sana kwani yanatunzwa vizuri. Huko vijijini watu hawana maji wao wanalazimisha kutengeneza hapohapo Dar wanaposhinda hao wanaosema wacheza pooltable.
Nyumba za Tandale zinafaa kutunza?
 
Your right! Unajua hii program sio mpya ni ya kitambo na Mdau wa kwanza ambae aliingia kwenye hii project ni NSSF.

NSSF waliteua maeneo for pilot project na moja ya hayo maeneo ni Manzese ambayo walikusudia kuivunja na kujenga upya!!
Good idea NSSF watekeleze hiyo plan yao,Dar unabidi ipimwe yote no more slams...Serikali itekeleze wapange plan hata ya miaka 15 kutokomeza slams jijini dsm.
 
Wenzetu India walikua na mji umekosewa unaitwa Dehli wakaona isiwe shida wakatafuta eneo jipya wakaplan vizuri na sasa ndo mji wao mkuu unaitwa New Dehli. Kwa bongo kupanga mji upya unaweza ukalete migogoro mingi sana, mana utahitaji mashirika makubwa kama NSSF,PPF,NHC n.k japo changamoto kubwa ni kwa wamiliki wa nyumba.
Nimewahi kusikia plan wanayotaka kuitumia, mfano kama ni Buguruni wanachukua wamiliki 10 wa nyumba kisha wanatafuta mwekezaji anabomoa hizo nyumba kisha anajenga maghorofa kwa kufata ramani ya jiji, anaweza jenga ghorofa 5 zenye flats 10 let say kisha anawagawia wale wamiliki mojamoja zinazobaki zake.
 
  • Thanks
Reactions: 911
Haina maana kutengeneza jiji kwa kuwaharibia watu maisha yao mkuu, real estates zinabumaga hata US, huwez amino kuwa bei ya nyumba Dar ni ghali kuliko hata US, na hii ilisababishwa na mijizi kuiba pesa na kuzigawa bila hata kutumia akili,
Ikawavutia mabwenyeye wa mafuta wakaanza kushusha maghorofa ya nguvu , sasa hivi fleti nyingi za kkoo bei imeshuka na nyingine zipo tupu........
Real estate developer kama NHC anauza nyumba ghali kuliko private developers....uhuni at its best.........sijawah kuhitaji na wala sina shida ya nyumba za hao walafi, tatizo ni namna wanavyosumbua wananchi kwa mambo yasiyo na tafiti za kutosha.
Mkuu umenene hao jamaa waNHC ni balaa ukienda kwenye ofisi zao Temeke kuangalia bei za nyumba au flat ni hatari.
Nimeamua kununua shamba kubwa nje ya mji naishi vizuri tu.Wakae Na mji wao.
 
Good idea NSSF watekeleze hiyo plan yao,Dar unabidi ipimwe yote no more slams...Serikali itekeleze wapange plan hata ya miaka 15 kutokomeza slams jijini dsm.
Yah... ni good project ingawaje ni very expensive. Hata hivyo, nadhani kwa NSSF ya Dau na JK wangefanya lakini hii NSSF ya sasa na JPM, I doubt if they will! Kwanza hata Mawaziri wataogopa ku-approve larger investment ideas!
 
Back
Top Bottom