Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kisha kupangwa upya, baada ya Ramani ya Mipango Mji (Master Plan) mpya kukamilika.
Akizungumza na Wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi jijini Dar es Salaam leo, Waziri Lukuvi amesema ameagiza mpango huo utakamilika kabla ya Julai ili mpango wa upangaji upya jiji hilo uanze.
Pia Waziri Lukuvi amesema kuwa nyumba zianazojengwa kwa sasa na kampuni na mashirika ya Umma, likiwemo Shirika la Nyumba la Taifa sio za bei nafuu kulingan na hali halisi ya kipato cha Watanzania wengi, na badala yake ameagiza NHC liwakusanye wabunifu wa nyumba za bei nafuu watoe muundo ili Watanzani ndio waamue aina ya nyumba za bei nafuu.
Source: Mwananchi