Jiji la Dar kufumuliwa, Kupangwa upya

Jiji la Dar kufumuliwa, Kupangwa upya

Tofauti ya London na Dar ni kubwa...kila kiwanja kimepimwa tangu enzi na enzi na kinajulikana na kila huyo ana anuani...sisi Dar yetu hata ukiwa angani haina tofauti na wale wadudu wanaotoa moto usiku wakiwa porini hawana mpango maalum maana kila huyo anaruka kivyakevyake akitafuta ridhiki au malazi...Dar haipendezi kabisa katika mipango miji ya kisasa...hasa kwa kuwa kuna hata baadhi wana magari lakini hawawezi kufika kwao. Nadhani hii ndiyo maana ya Dar mpya si kuvunja nyumba zote. Kama ni kuvunja zote itakuwa shughuli kupata mahali pa muda kwa watu milioni sita...uh na wakiwemo mapapa!!!!!
Umenena vema sana.
 
This is simply a nonsense......,unajenga vip jiji moja upya wakati ulishaitangazia dunia una matano.......kwanin pesa hizo zisiende kuendeleza Tanga au hata Mwanza........huu uhuni wa kila kiongozi kuamua maisha yetu ifike mahali tuukatae, hadi inafika mahala unaogopa kuendeleza eneo lako kwa sababu ya kuhofia watu wanaojifungia ndani wasiojua shida za watu wa kawaida.....to most Tanzanians with mid level income all they have is a small house, be it in Tandika or Buguruni but it worth it.....,

Masterplan yeye lengo la kuwaondoa maskini kati kati ya jiji kwa nguvu haikubaliki, hivi mbona Kariakoo waliondoka wenyewe, nani aliwatoa?
Jiji linajijenga lenyewe, masikini wa Vingunguti na Tandale ndio hali halisi ya wananchi mil 50,haifichiki...tuache kulazimisha kila kitu,
NHC ndio kabisa wekuwa makuwadi wa matajiri...hivi mtu mwenye uwezo wa kununua fleti za 200m anahitaji nyumba kweli? Kama wazimu , na bado kuna fisi wanawatetea ...what a shame.
Masikini kila sehemu huwa hapendeki mkuu.

Hata na ndugu zake, achilia mbali serikali
 
Kuna mikoa kibao imechoka sana hii pesa wana taka kugawa tu majengo yatagarimu Pesa nyingi nusu ina ingia mifukoni mwao au wana andaa ufisadi wa namna nyingine!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Naona watu mapovu yanawatoka! Inaonesha jinsi ambavyo watu wamejenga hovyohovyo. Hahaa. Inatia huruma though.
 
mn naona ni wazo zuri hapa ndio sura ya mji na nchi hatuwezi kupaacha hivi hivi panatakiwa pabadilike pawe pa kisasa jiji la maonyesho libaki bwagamoyo tanga na zanzibar
kula nchi duniani lazima iwe na mji ulio jengeka na waki sasa hiyo London unayo iyona lei ilijegwa miaka iliyopita migi sana na walijenga majengo yanayo dumu 200 years sasa nyumba za manzese na mwananyamala ni za 80 years tu.nyingine zimeshaanza kubomoka zenyewe waache hinyo ili iweje?
 
Hamtaki maghorofa ya kupigia picha??

Mmesahau mlivyojengewa daraja la manzese miaka hiyo kila mjanja wa town alikuwa anakwenda darajani manzese kujifotoa, ili mradi na yeye aonekane ni "mutoto ya mujini"??
Ah!!Mighorofa tunaitaka aisee lakini usafi na usafiri kwanza!

Hao waliokuwa wanaenda kujifotoa daraja la Manzese sio wajanja wa town bali walugaluga wa town!! Wanapiga picha halafu wanazituma kwao kwa P.O. Box!!
 
Sisi wakazi wa Dar es salaam kwa sasa yoooooote hayo hatutaki ila anzeni na suala la usafi kwanza na kero ya usafiri.
Kwa Sasa shughuli zote Ni Kariakoo , hivyo watu wengi ndani na nje ya nchi wanakuja K'koo , wakipanga upya shughuli zitatawanywa na hivyo kupunguza ujazi wa watu k'koo na hivyo kuwezesha USAFI
 
Naona wanaiwinda sana Manzese, wanataka kuifanya iwe sehemu ya City Center
Your right! Unajua hii program sio mpya ni ya kitambo na Mdau wa kwanza ambae aliingia kwenye hii project ni NSSF.

NSSF waliteua maeneo for pilot project na moja ya hayo maeneo ni Manzese ambayo walikusudia kuivunja na kujenga upya!!
 
Kwa Sasa shughuli zote Ni Kariakoo , hivyo watu wengi ndani na nje ya nchi wanakuja K'koo , wakipanga upya shughuli zitatawanywa na hivyo kupunguza ujazi wa watu k'koo na hivyo kuwezesha USAFI
Penye nia, itachukua less than 6 months Jiji kuliweka safi lakini kulisuka upya jiji hata kama tutakuwa na nia itachukua at least 10 years!!! So, kwanini tusianze na kinachowezekana?! Kigamboni satellite city zaidi ya miaka 5 sasa tunaishia kuiona kwenye mapicha tu!!
 
Hawa watawala wache mzaha, ni kweli kwamba ni jambo jema kuipanga Dar. Lakini kuna haja gani ya kujenga jiji moja kila mwaka wakata hata mji mkuu Dodoma haujastawishwa ipasavyo?
 
Hatuwezi kujenga jiji ndani ya Tanzania mpaka kiama kitafika. Itizame bandari yetu ilivyo ambayo inaingiza trilions kwa mwezi. Mpaka leo gari na containers zinakaa juu ya udongo. Kama kweli tunaweza, tungeanza na eneo la kilomita moja tu za mraba hapa mjini ikawa kama mfano, 1square km, na sio zaidi, tuoneshe mfano wa your imaginary city, Mheshimiwa!
 
Hawa watawala wache mzaha, ni kweli kwamba ni jambo jema kuipanga Dar. Lakini kuna haja gani ya kujenga jiji moja kila mwaka wakata hata mji mkuu Dodoma haujastawishwa ipasavyo?
Kuna mambo mengine hayazuiliki... watu wakubali tu na kuzoea kwamba at least for the next 30 years, Dar es salaam itabaki kuwa ndie mnyonyaji mkubwa wa resources za nchi hii!! Chukua watu wa majiji yote Tanzania halafu waweke pamoja bado idadi yao huenda isifike hata nusu ya wakazi wa Dar!
 
JIJI.jpg


Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kisha kupangwa upya, baada ya Ramani ya Mipango Mji (Master Plan) mpya kukamilika.

Akizungumza na Wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi jijini Dar es Salaam leo, Waziri Lukuvi amesema ameagiza mpango huo utakamilika kabla ya Julai ili mpango wa upangaji upya jiji hilo uanze.

Pia Waziri Lukuvi amesema kuwa nyumba zianazojengwa kwa sasa na kampuni na mashirika ya Umma, likiwemo Shirika la Nyumba la Taifa sio za bei nafuu kulingan na hali halisi ya kipato cha Watanzania wengi, na badala yake ameagiza NHC liwakusanye wabunifu wa nyumba za bei nafuu watoe muundo ili Watanzani ndio waamue aina ya nyumba za bei nafuu.

Source: Mwananchi
Achana na DAR mh. Waziri Jenga Satellite cities hata 5 hivi kwa nini Rasilimali na Nguvu nyingi kupanga Dar matokeo yake ni kuumiza wananchi. Kwanza Tanzania hatuna mji uliopangwa kwa nini usianzishe satellite cities hata 5 Tuna maeneo mengi Sana karibu na DAR.
 
Back
Top Bottom