Awamu ya 6 na Jiji la Dar - barabara kwishney!

Awamu ya 6 na Jiji la Dar - barabara kwishney!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,628
Reaction score
30,957
1780303087214.jpeg

Kwa sasa hivi Jiji la Dar halina mwenyewe.

Awamu ya 6 iko Dodoma, Dar itajiju.

Katikati ya Jiji kuna mahandaki kama tuko Bulyanhulu machimboni.

Mama anatoa Fedha lakini sijui zinaliwa na nani?
 
Sema hivi, kwa Sasa Tanganyika haina uongozi
Nenda Hospital za Serikali
Daladala
Takataka kila kona
Kuna mdau alitoa hoja ya majani kujaa jiji zima
Machinga mpaka kwenye pedestrian walk ways
Elimu imezikwa huko vyuo wanaishia kua content creators na kucheza Porn
Ajali zimekua kawaida
Kujengwa hovyo bila vibali wala mpangilio

Hakuna mwenye SAY ya nini kifanyike, wapi tuanze kurekebisha
 
Nafikiri kinachoendelea ni jambo jema.

Kitendo cha kutaja Bulyanhulu ni ushahidi kuwa maeneo yote au kwa usahihi nchi nzima hali ni tete.

Sasa, kwa kuwa upele umempata mkunaji, mkipiga kelele ninyi pengine na sisi watatusikia. Hali ni mbaya, barabara zimechoka.

Magufuli alisema tutatumia "taksi kutoka Bukoba hadi Mtwara, ( kwa maana ya ubora wa baraara) sasa hali inageuka. Kama kuna mahandaki tunatumia usafiri gani?
 
Ingawa ni Tatizo ni nchi nzima, ukitembea maeneo mbalimbali ya Mwanza, utabaki kujiuliza, hivi kuna serikali inayofanya kazi?

LIicha ya idadi ya watu na vyombo vya ussafiri kuongezeka kila kukicha, mamlaka zinahangaika kuweka taa na hivyo kuongeza foleni, hata kwenyemaeneo ambayo awali hayakuwa na foleni.

Kwingineko, hali ni tete, kuna kituo cha Afya Bulale, chenye kuhudumia kata za Buhongwa hadi maeneo ya wilayaya Misungwi, ambulance zinapishana,lakini barabara ni mahandaki, kipande cha mita 500 kilichopaswa kukamilika July 2025, mpaka sasa miezi 10 hakijakamulika!
 
Hii hali tuliiona miaka ya Mwinyi, Mzanzibari mwingine.
Mkapa ndiyo alianza kuokoa jahazi kwa kuunda TANROADS na ROAD FUND.
Sasa hivi Hela ya ROAD FUND inatumika kwingine isivyotazamiwa.
 
Nafikiri kinachoendelea ni jambo jema.

Kitendo cha kytaja Bulyanhulu ni ushahidi kuwa maeneo yote au kwa usahihi nchi nzima hali ni tete.

Sasa, kwa kuwa upele umempata mkunaji, mkipigie keleeninyi pengine na sisi watatusikia. Hali ni mbaya, barabara zimechoka.

Magufuli alisema tutatumia "taksi kutoka Bukoba hadi Mtwara, ( kwa maana ya ubora wa baraara) sasa hali inageuka. Kama kuna mahandaki tunatumia usafiri gani?
Kama kuna mahandaki basi watakuwa wanatumia treni
 
Kwani si pesa inaenda kwenye michezo, sanaa na utamaduni.
Comedy, Soccer, mikopo ya wasanii, n.k.
Barabara, maji na afya mtajua wenyewe.
Kwani akina Rio Ferdinand na Didier Drogba wamelipwa bei gani?
 
Saivi ukiwa na hela nunua plot Dodoma. Utakuja kunishukuru……Dodoma ya kipindi kile sio hii ya sasa
 
Magufuli alisema tutatumia "taksi kutoka Bukoba hadi Mtwara, ( kwa maana ya ubora wa baraara) sasa hali inageuka. Kama kuna mahandaki tunatumia usafiri gani?
Barabara zikipita tu zile Lori za mizigo zinazotoka Bandarini kubeeba kontena likapita njia hio siku hio basi ndio imeisha hio panatokea mshimo hapo wa ajabu na barabara ndio inakua imeishia hapa
 
View attachment 3599096

Kwa sasa hivi Jiji la Dar halina mwenyewe.
Awamu ya 6 iko Dodoma, Dar itajiju.
Kati kati ya Jiji kuna mahandakai kama tuko Bulyanhulu machimboni.
Mama anatoa Fedha lakini sijui zinaliwa na nani?
"Mama anatoa pesa" ndiyo ujinga gani. Pia huyo huyo mama anakopa je atalipa? Huyo huyo mama yenu anateka na kuua je atarudisha uhai au at least kuzifahamisha familia kuwa ameteka na kuua na hakuna wa kumfanya lolote. Huyo mama yenu anadaiwa matrilioni vipi mbona hasifiwi au kulaumiwa kwamba ana deni lake kubwa ambalo atawatwika walipa kodi mzigo wa kulilipa.
 
Back
Top Bottom