Jiji la Dar es Salaam kutopitika kabisa baada ya miaka 5

Dar haina magari mengi , ila barabara ndizo hatuna kabisaaa. ipo miji na majiji ya majirani zetu si wambli sana, na uchumi wao si hata mkubwa hata rasilimali zao si nyingi kama za kwetu ila mipangilio na utekelezaji wa maamzi vinaheshimiwa. nimetembelea miji na majiji machache mfano jiji la Addis Ababa Ethiopia miundombinu ya barabara isingekua bora basi kusinge pitika maana ukisema wingi wa magari basi Dar nikama hakuna hata gari na tukumbuke miaka kumi ilio pita walikua ndo mwanashikilia mkia kwa umaskini. Kwetu hayo ni matokeo ya kila alie na nafasi ya uongozi kuweza kuhoji na kuweka pingamizi au kuchelewesha utekelezaji wa mambo mbalimabali ya maendeleo. Siseme selikali isilipe fidia ila kwa manufaa au agenda binafsi tuzizuie bomoa bomoa kama mradi unao kuja niwa maendeleo ya wote.
Ina maana gani kutopanua barabara kwasababu watu watavunjiwa nyumba zao kwa manufaa ya wote. Majiji hayo yote yawenzetu hayakufanikiwa bila kuchukua maamuzi magumu ikiwemo kuvunja na kujenga nyumba za waathirika wa upanuzi au ujenzi huo. RUSHWA NI ADUI WA MAENDELEO
 

Chaotic Dar


dar es salaam 2.jpg
 
i wish ningekua kiongozi nionyeshe mfano kwan mpk muda huu mtu wa kuanziasha hayupo
 
Mkombozi;1728545]Nimebahatika kufika jijini Dar,ila cha ajabu hata kama unaenda sehemu ya karibu utachukua Muda mrefu sana.Kama hakutakua na jitihada za makusudi baada ya miaka 5 Dar hakutapitika kabisa.Kumetokea mtindo vijana wengi wananunua magari kwa kasi wakati miundombinu iko pale pale.Serika ianzishe usafiri wa uma kwa kujenga reli jijini Dar.Mradi wa mabasi ya kasi kitaalamu hautafanikiwa.Ijenge reli na kuimarisha usafiri wa umma.

Hebu tuelezee hiyo kitaalamu hautofanikiwa vipi?
 
Tatizo kubwa la miji ya Tanzania linaletwa na wizara ya Ardhi. Wizara hiyo haifanyi kazi yake kabisa. Kwa nini wasipime viwanja vya kutosha? Kuna wakati wanalalmika kuhusu gharama za upimaji kitu ambacho sikubaliani nacho nacho kabisa. Wananci DSM wnanunua viwanja kwa bei kali sana kuliko nchi nyingi za Africa. Serikalai ikipima viwanja na ikasema kila kiwanja kinauzwa milioni tano itapata wanunuzi wengi sana na pesa nyingi za kuendeleza huo mradi. Wakipima viwanja elfu 10 watapata bilioni 50. Tatizo liko wapi? Wanataka kuwe na viwanja vichache iwe washibishe matumbo yao kwa kuvirusha.

Wataalmu wetu waliopo wizara ya ardhi na mipango miji wameishia kuwa ni walanguzi tu. Nchi kama Botswana ilisomesha wataalmu wa ardhi na mipango miji hapo chuo cha ardhi. Botswana vilevile waliajiri wataalamu wengi wa ardhi na mipango miji kutoka Tanzania. Miji ya Botswana imepangika na inapendeza. Kwa sasa Botswana haina ghetto hata moja katika jiji la Gaborone yaani 100% ya jiji ni planned ukilinganisha na 20% ya Dar es salaam.

Tatizo siyo kuwa na reli. Johannesburg hawategemei usafiri wa reli. reli inaleta watu kutoka nje ya jiji. Gautrain ndiyo inaanza tu na inasafiri kati ya Pretoria na Johannesburg (70km). Barabara na mpangilio wa Johannesburg ni mzuri sana. Siyo kila penye uwazi pana nyumba, ugonjwa tulionao watanzania.

Maombi yangu kwa vijana ni kuwa ni lazima mdai kuwa na miji iliyopangika. Msikubali kuendelea kujenga nyumba mahali pasipo na barabara huku mkilazimika kuegesha magari mnayonunua CCM. Ni aibu kuwa na nyumba halafu huwezi kumwelekeza mtu jinsi ya kufika huko. Ni aibu kununua gari na kulipaki mbali na unakoishi halafu asubuhi unaamka na kuanza kuruka matope na uchafu mwingine ukielekea kwenye gari lako.
 
Back
Top Bottom