Jiji la Dar es Salaam kutopitika kabisa baada ya miaka 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiji la Dar es Salaam kutopitika kabisa baada ya miaka 5

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Mar 12, 2011.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nimebahatika kufika jijini Dar,ila cha ajabu hata kama unaenda sehemu ya karibu utachukua Muda mrefu sana.Kama hakutakua na jitihada za makusudi baada ya miaka 5 Dar hakutapitika kabisa.Kumetokea mtindo vijana wengi wananunua magari kwa kasi wakati miundombinu iko pale pale.Serika ianzishe usafiri wa uma kwa kujenga reli jijini Dar.Mradi wa mabasi ya kasi kitaalamu hautafanikiwa.Ijenge reli na kuimarisha usafiri wa umma.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,438
  Trophy Points: 280
  serikali haiwezi kufanya hii kitu wapo wapo tu na watakuwepo sana tu kutokana na huu ujio wa babu
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mpaka tubadilishe uongozi tunaokuwa nao vinginevyo improvement will always be impossible!
   
 4. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kila cku maeflu ya magari yanaingia bongo bila usafiri wa reli hata uongeze barabara bdo msongamano hautapungua. Solution ni usafiri wa reli kama india, china, etc
   
 5. K

  KVM JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa ni kuwa hatuna jiji. Duniani kama majiji yenye watu na magari mengi na hawana reli wala mabasi yayanyoenda kwa kasi lakini mambo nishwari kabisa. Dar es salam si mji bali ni ghetto au kijiji kikubwa. Kwa kweli hakuna wizara iliyoiangusha Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla kam wizara ya ardhi. Sioni hata umuhimu wa uwepo wake, na kama inatakiwa kuwepo basi iwe ni idara tu katika wizara nyingine.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Well said which we will need demolition and revisiting urban planning, we need brains at the top. Serikali imelala wanafurahia hali hii
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 6,027
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kwa 100%. Kama umehahi kutembelea majiji ya wenzetu halafu ukalinganisha na Dar es Salaam (sembuse Tanga, Mbeya, sijui na wapi), unaweza kulia machozi. Hili sio jiji, tunafanya mzaha kwenye kila kitu miundombinu ya hovyo - usafiri na majengo vikiongoza. Nadhani kuna haja ya kufanya maamuzi magumu kama Nigeria walivyowahi kufanya; waliachana na Lagos wakajenga jiji lingine la kisasa - Abuja ambalo lilipangiliwa kwanza kwenye karatasi (ramani) na utaratibu ukaheshimiwa. Vinginevyo tutaendelea kuvimba vichwa na Dar wakati wenzetu wanatushangaa - inatia hata aibu.
   
 8. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hili suala limezungumziwa sana mradi wa mabasi ya kasi hautatusaidia kitu, tutangeneza miundombinu hiyo ya mabasi na baada ya miaka 20, tutaibomoa na kusema tunahitaji huduma ya treni, hatuna mipangilio ya kudumu. ukweli unabaki palepale kwamba tunahitaji usafiri wa treni kwa jiji la Dar sasa, wasomi wapo wanasoma kila siku, tena wana majina makubwa makubwa kabisa Profesa, Daktari , Injinia n.k.... tatizo ni kwamba waliopo kwenye nafasi hizo pengine wamejawa na ubadhirifu ama ni wavivu wa kufikiri. Mimi ninashauri kwamba, kama wewe ni raia wa Tanzania una jukumu na haki kikatiba kutoa maoni yako, watembelee wahusika maofisini kwao, ama waandikie barua na kutoa maoni yako.
   
 9. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  sawa hatutonunua magari tutatembea kwa miguu ili mjini kusijae
   
 10. n

  nyantella JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  This is the Bongo Paradox!! halafu watu hao hao wanalalamika maisha magumu sana!!! wabongo bwana!! halafu si magari ya kitoto yanayoingia, ni ya nguvu, makubwa makubwa. yaani wakati wenzetu wana nunua gari kwa ku consider tatizo la parking space (angali vijigari wanavyoendesha wazungu katika miji ya ulaya!!), sisi wabongo the bigger the car the better!!! matokeo yake ndio hayo.
   
 11. n

  nyantella JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye red nakubaliana nawe kabisaa ila tatizo ni pioneers of the changes and the political will, kama unakumbuka jinsi ilivyokuwa vigumu kupanua Morogoro road, Kawawa, Mandela Kilwa etc, wanasiasa wanatumia opportunities hizo kuvuruga the good plans. The other problem ni cancer ya waTZ kuongea sana lakini vitendo ni zero!!! ndio maana jana wakati Mh. Nyalandu anongelea mambo ya umeme wa upepo watu wakaona kichefu chefu so that is our TZ.

   
 12. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekupenda Nyantella hapo " The other problem ni CANCER ya waTZ kuongea" ndio tunachojua tu. Ila inawezekena mipango ipo hatutaki kujaribu au ndio utasikia ile HAKUNA FUNGU LABDA TUSUBIRI WAHISANI.
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Folni na msongamano havitaisha Dar.
  Waziri husika anajaribu kutanua barabara kwa kubomoa nyumba zilizojengwa kiholela lakini waziri mkuu anampiga stop bila kutoa solution mbadala.
   
 14. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 280
  Kujenga mji mzuri, mitaa mizuri, nyumba nzuri, n.k mipango inaanzia vichwani mwa wakazi wenyewe wakiongozwa na viongozi wao.
  Jiji lisilopangwa vizuri ni uthibitisho tosha kwamba akili za wenye jiji hasa hasa viongozi hazijapangika, hawawezi kutofautisha kizuri na kibaya na madhara yake ni makubwa sana kwa jamii inayoishi humo.
  Maneno mengi kuhusu miji mipya ya kisasa ya pembezoni lakini utekelezaji hakuna, uthibitisho mwengine wa kuwa wanachokisema hawakijui na hawawezi ila wanakariri maneno tu!
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,406
  Trophy Points: 280
  amiin amin nawaambia wala dar hakuna magari mengi.. ni upuuzi tu watu wachache waowekwa maofisini, watu wa mipango miji, tanroads na ujenzi sijui hata wanafanya nini no plans at all! mpaka bara bara zinazojengwa sasa hivi wanafikiria kujenga two lanes!!! this is absurdy

  bara bara wanayotaka kujenga sasa hivi mwenge mpaka tgt nayo nasikia ni mbili kushoto na mbili kulia.. hiyo mandela road inayotengenezwa sasa hivi nayo hivyo hivyo, sam nujoma walianza na mkwala wakakwangua bara bara pana lakini mwisho wa siku ndo wamepanda minazi katikati.. hizo bara bara ndogo za mitaani ambazo zingeboreshwa zingeweza kupunguza foleni ndio zina mahandaki ya kuu gari za watu

  aaaaaaaaarg thsi country sucks big tyme bana!:embarassed2:
   
 16. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hii Mada ni Nzuri sana,

  Tatizo la msingi hapa ni wizara ya aridhi, na sio kila kitu tulaumu serikali kuu.
  Tatizo la aridhi linaanzia kwenye serikali za mitaa na kufikia wizarani, upimaji wa viwanja imekuwa ni tatizo kubwa sana hapa tanzania, na kama tungeliangalia hili tungeondoa matatizo mengi sana, kwa kweli hakuna sehemu yenye ubabaishaji mkubwa kama wizara ya aridhi na wababaishaji wala sio wanasiasa bali ni watendaji wa wizara, watu wanafikiria pesa tu na sio kufanya kazi. Ukienda serikali za mitaa kwa maswala ya aridhi ubabaishaji, ukija wilayani kitengo cha aridhi ubabaishaji ukienda wizarani ndio kabisaaa….. watu wanakuangalia tu, waziri husika yupo!, naibu yupo!, Katibu na wakurugenzi wapo tu wanatafuna pesa za Kodi zetu na hasa lipa kama unavyopata.

  Kwenye miradi ya upimaji Viwanja ndio balaa kabisaa, kama kunaeneo linapimwa viwanja ni maafa, habari sahihi hazitolewi, wanachi hawaelezwi nini cha kufanya na wala hawaambiwi haki zao, tunaoharibu nchi hii wa kwanza ni sisi wanachi hasa watendaji wa ngazi za chinina pili ni viongozi wa juu kushindwa kuwawajibisha watendaji wabovu.

  kwa mfano; hivi kunaubaya gani kuwaeleza wakazi wa kigamboni ukweli na kuchukua hatua haraka kuliko kuwababaisha mara kuna mradi, mara hakuna, uongo mtupu, ifikie mahala watu wajifunze kusema ukweli ili kurahisisha mipango ya nchi, ni busara kuwaeleza wanachi kuwa eneo hili litajengwa barabara na wote waishio hapo wanatakiwa kufanya A,B,C na kama unamaswali Uliza office Z na wakifika huko Office Z wamwone office Y na Officer Y ajue cha kuongea na Wanachi na ukweli tu, hata kama kitawauma wanchi lakini ikiwa ni kwa mujibu wa sheria nafikiri wataelewa cha msingi ni kuangalia haki na maslahi ya pande zote mbili, na sio maslahi ya watendaji ambao wanalipwa mishahara kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

  Pia hakuna mawasiliano kati ya wizara moja na nyingine, kwa mfano kukiwa na mradi wa upimaji viwanja wizara ya aridhi inatakiwa iwasiliane na wizara nyingine husika ili wawe na mpango kazi wa pamoja na ndipo utaona , upimaji utaenda sambamba na upimaji wa barabara, tanesco nao watafika, maji nao pia, Afya,Elimu nk. Na tutaepusha mpangilio mbovu wa makazi na bomoa bomoa zisizo za lazima na zinazo umiza wanchi hasa wa kipato cha chini, wewe unafikiri nani atasubiri kwa miaka 10 mpango wa kupima viwanja na ilihali anakaa nyumba ya kupanga! Hapa inaatkiwa wanachi wapimiwe viwanja kwa haraka na kuwapa plan ya jinsi ya kujenga Simple!

  Tatizo kubwa la Watz ni ubinafsi wa kutaka kujilimbikizia mali, kwa mfano utaambiwa mkubwa flani ana hekari 500, pwani, 300 MZA, 80 Lindi, 200 Kigoma zote hizo za nini? mapori Tu! na ukija mradi kigamboni wakubwa wanataka viwanja Vyote, Tamaaa ya nini, mwisho wa siku utahitaji 6x4 sq metres and 6 ft down, Tubadilike kwa maendeleo ya nchi hii.
   
 17. M

  Mndamba Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Uko sahihi kabisa. Tunahitaji Reli. Tatizo liko kwenye maamuzi na matumizi ya pesa za walipa kodi. Ukiangalia utaona maamuzi mengi na utekelezaji wake katika nchi hii yanafanywa KISIASA. Kwa stahili hii tunasafari ndefu sana kufikia maendeleo.
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Wazri Mkuu amefafanua vyema kuwa sheria za barabara zimekuta tayari nyumba zimejengwa katika maeneo hayo kwa ardhi husika kutolewa na Serikali, hivyo ni uhuni wa hali ya juu kuwaita ni wavamizi wa hifadhi za barabara. Waziri mhusika badala ya kutafuta sifa kwa kubomolea watu kiholela anatakiwa kuwa na road expansoiion project in hand ndipo nyumba zilizoko katika hifadhi husika zibomolewe. kwa kufanya hivyo Sertikali itaweza kuwalipa fidia wahuiska sio kama ilivyokuwa imefanyika kutaka kubomoa nyumba nchi nzima.
   
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Muheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. JK. aliwahi kuwaambia kithibitisho cha maisha bora kwa kila MTZ.. angalieni idadi ya magari yaliotapakaa kila kona ya jiji... thetehehe.. Mimi Ni CCM But that comment was very low from him
   
 20. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hatuwezi kuwa na jiji la kisasa mpaka pale Taaluma itakapo heshimika na kuachana na siasa katika mambo ya kitaalamu.
   
Loading...