Jiji la Arusha leo limeamka na mgomo wa daladala

Jiji la Arusha leo limeamka na mgomo wa daladala

HIPPO

Member
Joined
May 4, 2012
Posts
79
Reaction score
16
Wana jf leo kuna mgomo wa mabasi ya abiria yaani daladala katika jiji la Arusha hali ni tete kwa wasafiri
 
Ni kweli ndiyo nilikuwa najiandaa kupandisha uzi, hali ni tete sana
 
yeah mgomo upo na tumewaambia vijana wetu wapaki magari pembeni na matrafiki wapeleke watu makazini..ni ule utaratibu wa kila trafiki akitoka kituoni anaambiwa apeleke magari matano kituoni...kwa hiyo wanachokifanya ni kukamata Hiace hata kama haina kosa kabisa wanapeleka kituoni..
 
Asubuhi ya leo wakazi wa jiji la Arusha wameamka na kukumbana na mgomo wa mabasi madogo ya Abiria maarufu mjini hapa kwajina la "vifodi" au "Vihaisi". makundi makubwa ya watu yameonekana yaki tembea kwa miguu huku wengine wakisimama kandokando mwabarabara kwa matumaini kwamba huenda pakatokea usafiri mbadala.,
aidha hiii imekua ni fursa kwa wafanya biashara ya usafiri wa pikipiki maarufu kama "Bodaboda" na wale wa magari madogo "Taxi" kufanya biashara kubwa zaidi.,

bado haija julikana kwa haraka nini chanzo cha mgomo huo, na madai ya wafanya biashara hao wa daladala.
 
Kweli leo arusha kuna mgomo mkali wa daladala hasa njia ya kisongo.kwamrombo na mbauda,hakuna hata daladala inayotoa huduma asubuhi na mapema mgomo umeanzia maeneo hayo kadiri muda ulivyoendelea kufika saa 1.20 sehemu zote wakasitisha na kuna vitisho kwa daladala yoyote itakayoonekana inapasuliwa vioo kwa mawe na masela wengi wana mawe kando ya barabara,kuna misururu mirefu ya watu wanachapa laoa kwa miguu kuelekea maofisini na bodaboda ndo hazishikiki na bei wamepandisha elfu tatu kwa umbali wowote,kisa hawa jamaa wanalalamika kuwa polisi wanawakamata sana na kuwatoza faini sana .nawakilisha toka A- town
 
Duh! Mara kisa hawa jamaa wanalalamika kuwa polisi wanawakamata sana na kuwatoza faini na wengine kisa ni ongezeko la nauli? Hapo mkweli nani? Nahofia karibu JF itageuka kuwa kokolo, kuzoa kila kitu!
 
Duh! Mara kisa hawa jamaa wanalalamika kuwa polisi wanawakamata sana na kuwatoza faini na wengine kisa ni ongezeko la nauli? Hapo mkweli nani? Nahofia karibu JF itageuka kuwa kokolo, kuzoa kila kitu!

Wanalalamika kukamatwa na polisi wa barabarani kwa makosa yanayosababishwa na mamlaka ya mji haswa ni vituo, mamlaka haijaweka vituo maalum au madereva hawajui vituo halaf wakisimama sehemu wanayoamini ni vituo wanakamatwa kwa kutosimama kituoni.
 
No, ukweli ni kuwa wanadai wanakamatwa sana na kutozwa faini huo ndo ukweli,manake kama ni nauli sikuna utaratibu wake na bei za daladala sehemu zote ni kama zipo sawa arusha hawawezi kukomalia hilo wakati wala hakuna foleni kali kama dar.
 
Niliwahi kuandika hapa jamvini kuhusu trafiki kutanda Barbara kusumbua wenye magari kuomba hongo, pia kufanya kazi za Tra hicho ndo chanzo cha mgomo
 
Hali ni mbaya sana njia zote!
Zaidi sana tabu ni kwa wanafunzi ambao wengi wamerudi majumbani baada ya kukosa namna ya kwenda mashuleni.
 
Chapeni lapa!. Tz hii inaelekea zama mpya yawezekana wanadai fly-over.
 
Trafick wa Ar ni aibu tupu. Ni omba omba hadi basi. Ajabu unampa halafu anaenda kituo kingine ukipita anakupiga mkono anaomba tena. Hivi ni lazima wawepo baarabarani kila siku ? Si wameshakagua yote ?
 
poleni ndugu zangu wa arusha

Mimi nimechapa lapa na nimeshuhudia abiria wakishushwa kwenye suzuki. Nawasikitikia watoto wa shule kukosa masomo kutokana na mgomo huo.

SUMATRA haina meno? Kweli ni udhaifu wa Serikali kwani inaendeshwa hata na wenye madaladala!
 
Back
Top Bottom