Jihadharini wizi mpya wa fedha zilizoko kwenye m-pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jihadharini wizi mpya wa fedha zilizoko kwenye m-pesa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwandiga, Mar 7, 2012.

 1. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Hii imemtokea rafiki wangu wa karibu sana jana 06/3/2012 saa tisa mchana. Kwenye akaunti yake ya M-pesa alikuwa na tsh 35,000 ambazo kwake ni kiasi kikubwa sana cha fedha na alikuwa anauhitaji nazo ndio maana akazihifadhi. Jana mnamo saa tisa simu anayotumia ikaonyesha ujumbe unaosomeka SIMcard registered failed ikapoteza mawasiliano, aliizima na kuiwasha tena lakini ujumbe ukawa huo huo.

  Alidhani simu imeharibika akaipeleka kwa fundi na fundi alipoiangalia tu akamwambia simu sio mbovu laini ndio mbovu hivyo ajaribu kuweka laini nyingine naye alivyofanya hivyo ilifanya kazi vizuri tu. Ilibidi apige simu vodacom customer care leo asubuhi na kuwauliza kuhusu hil0 jambo. walimwambia hiyo namba ipo hewaniba. Baada ya yeye kuwaelezea ilivyokuwa jana walimwuuliza maswali mawili matatu ndipo wakamwambia hiyo namba jana ilitoa fedha zilizokuwemo tsh 35,000 na wakataja jina la wakala aliyetoa hizo fedha, huyu bwana kwenda kumuuuliza huyo wakala akakataa kuwa hajatoa hizo fedha.


  Kilichofanyika ni hivi huyu aliyeibiwa fedha kwenye M-pesa juzi tarehe 05/3/2012 alienda kwa huyo wakala akampa simu ili atoe fedha kidogo kwa ajili ya matumizi yake, yeye hajui jinsi ya kutoa fedha Mpesa, wakala akamuuliza namba yake ya siri PIN number naye akamtajia kisha akamkabidhi simu na fedha akaondoka zake.

  Yule wakala au mtu mwingine aliyekuwepo eneo hilo alisikia ile namba ya siri na kujua namba ya simu ya huyo mteja kishwa akaswap ile namba, wakati huyu mwizi ameswap ile namba ndipo meseji kwenye simu ya aliyeibiwa ikatokea SIMCARD REGISTRATION FAILED nahuyu mwizi akafanikiwa kuwa mmliliki wa namba hiyo na kutoa kiasi chote cha fedha zilizokuwa kwenye akaunti yake hiyo, na vodacom wamemwambia hawana msaada zaidi wa kumsaidia ila aende polisi, alivyoenda polisi akaambiwa atoe fedha tshs 40000 ili waweze kumsaidia.

  *Hivi haya makampuni ya simu hayawezi kuweka utaratibu mzuri wa kuswap line za simu badala ya ule wa kutaja namba tano unazopiga sana???????

  *Wananchi wengi hawajui au hawaelewi jinsi ya kotoa fedha kwenye akaunti ya mpesa hivyo wanawapa wakala simu zao na kuwatajia namba za siri ili waweze kutoa fedha na huo ndo mwanya wa tamaa na wizi kwani akiona salio kubwa atakuwa na tamaa na pia mara nyingine wanaokaa kwenye huduma za mpesa ni deiwaka tu mara nyingi watoa fedha hawasaini kwenye ledger kama inayotakiwa. Hapa wizi utaendelea sana Kuweni makini.

  Soma huu ujumbe na mweleze mwenzio ili achukue tahadhari.
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, nashukuru kwa taarifa.
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Si huwa tunaambiwa tusitoe namba zetu za siri, inakuwaje unamwambia mwengine?

  Ni sawa na kutoa PIN yako kwenye ATM
   
 4. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kumbe aliyataka mwenyewe!kila siku wanatangaza tunza namba yako ya siri!huwa haelew?ilibd huyo mtu wa m pesa angemrejeshea simu yake ili aweke namba yake ya siri!mpe pole tu huyo jamaa yako!
   
 5. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  kutokana na soko huria kwa sasa,ata manzese unaweza fanya sim swap,so hapo ni kuwa makini na Password yako tu na sio vinginevyo,MPesa ni english na Kiswahili iweje mtu anaomba kutolewa ata pesa?huyu ndugu yako ajui soma?mpe pole yake
   
 6. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wala simuonei huruma huyo jmaa yako. Yaani kajipeleka yeye mwenyewe kuibiwa
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pamoja na stori yote lakini kuna element ya uzembe katika tukio zima hasa pale alipokabidhi pin number kwa huyi jamaa wa m pesa.

  Hilo ni angalizo awe makini siku zijazo.
   
 8. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Vodacom watashangaza kama waliruhusu sim card swapping bila kupewa vielelezo maalamu la kitambulisho na fomu ya usajili. kwa upande wao walichemsha kwa hilo
  Kosa kubwa lipo kwa mmiliki wa simu, tena alimwamchia simu na namba ya siri wakala, Hivi ukimpatia mtu ATM card yako na PIN wewe unategemea nini kitafanyika? mmiliki wa line nae alichemsha kivyake
   
 9. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,449
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Poa mkuu fikisha ujumbe kwa mwenzako
   
 10. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Roja tht ntamtafuta huyo mwizi kimya kimya nimchinje
   
 11. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa taarifa mkuu, wanaokejeli wajue kujua kusoma na kuandika siyo kujua kutumia simu na simu zinatofautiana.
   
 12. uronu

  uronu Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 5
  mtoa taarifa hana maana ya kuhitaji lawama mnazo toa, pengine hili linaweza lisikukute wewe badala yake likamkuta ndugu yako wa karibu tena uliye mtumia pesa kwa hitaji muhimu.
  2nachotakiwa kuipokea na kutoa pole kwa muhusika na sio ku analyze uzembe alioufanya

  hili ni angalizo kwangu mimi nimelipokea na nitalitolea ufafanuz kwa watumiaji wengine kutunza PIN namba zao
  mpe pole huyo ndg....
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  alipokubali kutoa pin namba yake, alikuwa amekubali kuibiwa. Hilo ni kosa lake.............
   
 14. aye

  aye JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  tatizo lililopo watu wengi hasa mpesa namba zao za siri ni miaka yao ya kuzaliwa kitu ambacho ni riski sana hata mtu wakaribu akijua mwaka wako wa kuzaliwa akijaribu hata angalia salio inakubali,nawakubali tigo sana huweziweka mwaka wa kuzaliwa kama namba ya siri, kwa wale ambao hawajui kutoa au kutuma ni vizuri wakati wa kuweka namba ya siri waweke wenyewe bila kutaja kwa wakala wengi wanaumia sana kwa ilo na makampuni haya hayana msaada wowote pale inapotokea unaibiwa ivyo ndo mana wanasisitiza tunza namba yako ya siri maana ni siri yako mwenyewe usimwamini mtu
   
 15. faizah

  faizah Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Sio kosa la kampuni lakini Ahsante kwa taarifa
   
 16. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  1.Atoe taarifa polisi.
  2.Aende Vodacom HQ kutoa malalaliko yake ambaya yatafanyiwa kazi na wakala aliyetoa hiyo hela atawajibika kumrudishia hela iliyotolewa, maana kila wakala ana log book (kitabu cha kumbukumbu) ambapo mteja anayetoa hela lazima asign na kuonyesha kitambulisho
  3.Aombe afundishwe namna ya kutumia huduma za kifedha za Vodacom
   
 17. Kipeperushi

  Kipeperushi Senior Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kutuomba tufikishe ujumbe kwa ndugu na marafiki zetu, na wewe tunakusihi elimisha ndugu na marafiki zako. Ni aibu sana kwa mtu wa kizazi hiki kushindwa kujifunza hata mambo mepesi kama kutoa pesa kwa huduma ya M-pesa au kutumia ATM. Nasema ni aibu, tena ni ujinga usio na msamaha kabisa...!, kwa sababu maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hizi yanafundishika, na tahadhari juu ya kutunza namba za siri huwa zinatolewa kila siku kwenye redio. Au hata redio nazo ni issue kwake kusikiliza? Kama ni hivyo basi mpe pole sana, wakati umesha mpita.
   
 18. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  si rahisi kuibiwa hivyo. Hapo kwenye KUSWAP kuna utata mkubwa. Akienda Voda atapata full data za nani aliswap. Kama hakuna basi kuna conspiracy hapo kati. Fuatilia hiyo swap, wakileta mizengwe nenda juu, polisi haihusiki kabisa na swap.
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  shukuru mungu wewe unajua kusoma na kuandika zaidi ya hapo ungekuwa kama aliyeibiwa..
   
 20. d

  dmatemu JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 591
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  Atakua amejifunza nini maana ya namba ya siri.
   
Loading...