Jihadharini wizi mpya wa fedha zilizoko kwenye m-pesa

Nashukuru kwa taarifa mkuu, wanaokejeli wajue kujua kusoma na kuandika siyo kujua kutumia simu na simu zinatofautiana.


Nimewashuhudia watu wengi,wakiwakabidhi simu zao wahudumu wa M-PESA,na kuwatajia namba zao za siri,wakati wa kutoa fedha kwenye simu zao!
Hilo,ni fundisho,hivyo tuwe na tahadhari na hilo!
Pole yake sana!
 
Si huwa tunaambiwa tusitoe namba zetu za siri, inakuwaje unamwambia mwengine?

Ni sawa na kutoa PIN yako kwenye ATM
Kutoa simu kwa muhudumu wa m-pesa na kumwambia akutolee fedha ambazo unamtajia kisha anakuuliza namba yako ya siri ili aweze kuto fedha hizo ni kutu cha kawaida sana kwa maeneo ya huku bushi. Nimefuatilia kwa umakini sana na kuna siku ya jana na leo nimetumia muda mwingi kwenye sehemu za kutoa huduma za mpesa kati ya watu kumi waliokuwa wanakuja kutoa fedha 7 wanatoa simu zao kwa wahudumu na watatu ndio wanafuata taratibu kwa kutoa fedha wenyewe baada ya kuweka namba ya wakala. Na wengi wao ni wa jinsia ya kike, kwa wanaume ni wababa wa makamo na wazee ndio walikuwa wanatoa simu zao kwa mhudumu. Hawa wanakuwa na imani na mhudumu kwni wanajua simu anaondoka nayo baada ya kutoa fedha hivyo mhudumu hawezi kufanya lolote baya kwenye akaunti yake
 
Nimewashuhudia watu wengi,wakiwakabidhi simu zao wahudumu wa M-PESA,na kuwatajia namba zao za siri,wakati wa kutoa fedha kwenye simu zao!
Hilo,ni fundisho,hivyo tuwe na tahadhari na hilo!
Pole yake sana!
Pamoja sana, wengine wanabisha kitu ambacho kipo ilimradi abishe tu
 
poleni sana mkuu.ila polisi nao 40000, mmh!!
Unashangaa!!!! mtu amebiwa 35,000 anaambiwa atoe tshs 40,000. ni kawaida ya polisi. Walimwambia fedha hizo ni pamoja na za kuweka mafuta ya kwenda kwa wakala aliyetajiwa na watu wa vodacom ambapo fedha yake ilichukuliwa, japo jana jioni nilienda nae lakini alikuwa mtu mwingine na akasema yule aliyekuwa juzu (siku ya kutoa fedha) ni mwanafunzi na hayupo
 
Na nyie wa Mwandiga, Manyovu mjifunze bwana! Utatoaje PIN na wewe? Tena hadharani! Aliyataka mwenyewe.
Unajua hii teknolojia bwana sio yetu, huwa tunadhani tunaweza kukosea na fedha zote kupotea wakati wa kutoa kwani kuna mlolongo wa kubonyeza namba, hii ndo sababu kubwa, wengi wetu shule hakuna kabisa ila tunajifunza kupitia makosa. Nafanya mpango nihame huku mwandiga nisogee hata morogoro sasa
 
Hakuna cha kujihadhari hapo! kitu kipo wazi... nywila(password) yako inatakiwa iwe yako mwenyewe
 
Atakua amejifunza nini maana ya namba ya siri.
Atakuwa hajajifunza lolote kwani wakati anasajili namba yake hiyo namba ya siri alipewa na mtoa huduma hivyo hata kuibadilisha hajui na kwa kuwa alipwewa na mtoa huduma haoni ugumu kumpa ili aweze kutoa fedha kwenye akaunti yake, Alipoambiwa asitoe namba kwa mtu yeyote alidhani watoa huduma wa mpesa hawapo katika hiyo category ya wasiotakiwa kupewa namba
 
si rahisi kuibiwa hivyo. Hapo kwenye KUSWAP kuna utata mkubwa. Akienda Voda atapata full data za nani aliswap. Kama hakuna basi kuna conspiracy hapo kati. Fuatilia hiyo swap, wakileta mizengwe nenda juu, polisi haihusiki kabisa na swap.
Huku ni ukanda wa bonde la ufa, hivyo kunakuwa na radi sana ambazo huwa zinaunguza simu hata tv, na vifaa vingine vya electronics, huyu bwana alizima simu wakati mvua inanyesha kwani iliambaatana na radi kali na baada ya nusu saa alivyowasha ndio alipata ujumbe huo wa sim card register failed. aliwapigia vodacom na walichomwambia ni kuwa hiyo namba haina fedha kwa muda huo na zilotolewa kwa wakala ambaye alitajiwa jina na muda na mkoa huu huu, msaada mwingine hawakumpa. ila chip yake anayo mkononi hadi sasa
 
Pamoja na kutuomba tufikishe ujumbe kwa ndugu na marafiki zetu, na wewe tunakusihi elimisha ndugu na marafiki zako. Ni aibu sana kwa mtu wa kizazi hiki kushindwa kujifunza hata mambo mepesi kama kutoa pesa kwa huduma ya M-pesa au kutumia ATM. Nasema ni aibu, tena ni ujinga usio na msamaha kabisa...!, kwa sababu maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hizi yanafundishika, na tahadhari juu ya kutunza namba za siri huwa zinatolewa kila siku kwenye redio. Au hata redio nazo ni issue kwake kusikiliza? Kama ni hivyo basi mpe pole sana, wakati umesha mpita.
Unachosema ni ukweli ila mshukuru mungu kwa kuwa upo sehemu za mjini au umebahaatika kusoma. Kukaa mjini pekee inakufanya uwe mjanja na kuwa na uelewa wa mambo fulani ambayo mtu wa bushi kuyajua ni ngumu sana, Wapo ambao hawana bahati uliyonayo wewe, hata uelewa wa vitu vidogo ni shida sana na ndio hao waliopo huku, Kutoa simu na namba ya siri kwa mhudumu wa mpesa ni kitu cha kawaida sana huku, ila baada ya mambo kama hayo kumfika ndo anapaata akili ya kubadilika, redio yenyewe wakati mwingine unakuta ni moja na inakaa chumba cha mdingi na maza na ndio wanaoifungua na kuifunga mtoto utaisikia saa ngapi? Na ndio maana hizo 35,000 zilimuuma sana kwani alikuwa anakusanya mtaji hivyo
 
Vodacom watashangaza kama waliruhusu sim card swapping bila kupewa vielelezo maalamu la kitambulisho na fomu ya usajili. kwa upande wao walichemsha kwa hilo
Kosa kubwa lipo kwa mmiliki wa simu, tena alimwamchia simu na namba ya siri wakala, Hivi ukimpatia mtu ATM card yako na PIN wewe unategemea nini kitafanyika? mmiliki wa line nae alichemsha kivyake
Ndugu yangu unavyoenda kufanya sim card swappin huwa hawaulizi vitambulsho, wanachokuomba ni shilingi elfu mbili na namba tano ulizopiga mara kwa mara au mara ya mwisho basi. Na siku hizi hata hawa wanaokaa na miavuli ya vodacom, tigo na mpesa vibanda wanaswap kama kawa. Udhibiti kwenye hilo haupo hata kidogo, na hizi sehemu mara nyingi unakuta ni hawa vijana wamemaliza kidato cha nne tena wapo kikundi cha watu 6 ni washkaji wamekaa wanapiga stori huku kazi ikiendelea
 
Hii imemtokea rafiki wangu wa karibu sana jana 06/3/2012 saa tisa mchana. Kwenye akaunti yake ya M-pesa alikuwa na tsh 35,000 ambazo kwake ni kiasi kikubwa sana cha fedha na alikuwa anauhitaji nazo ndio maana akazihifadhi. Jana mnamo saa tisa simu anayotumia ikaonyesha ujumbe unaosomeka SIMcard registered failed ikapoteza mawasiliano, aliizima na kuiwasha tena lakini ujumbe ukawa huo huo.

Alidhani simu imeharibika akaipeleka kwa fundi na fundi alipoiangalia tu akamwambia simu sio mbovu laini ndio mbovu hivyo ajaribu kuweka laini nyingine naye alivyofanya hivyo ilifanya kazi vizuri tu. Ilibidi apige simu vodacom customer care leo asubuhi na kuwauliza kuhusu hil0 jambo. walimwambia hiyo namba ipo hewaniba. Baada ya yeye kuwaelezea ilivyokuwa jana walimwuuliza maswali mawili matatu ndipo wakamwambia hiyo namba jana ilitoa fedha zilizokuwemo tsh 35,000 na wakataja jina la wakala aliyetoa hizo fedha, huyu bwana kwenda kumuuuliza huyo wakala akakataa kuwa hajatoa hizo fedha.


Kilichofanyika ni hivi huyu aliyeibiwa fedha kwenye M-pesa juzi tarehe 05/3/2012 alienda kwa huyo wakala akampa simu ili atoe fedha kidogo kwa ajili ya matumizi yake, yeye hajui jinsi ya kutoa fedha Mpesa, wakala akamuuliza namba yake ya siri PIN number naye akamtajia kisha akamkabidhi simu na fedha akaondoka zake.

Yule wakala au mtu mwingine aliyekuwepo eneo hilo alisikia ile namba ya siri na kujua namba ya simu ya huyo mteja kishwa akaswap ile namba, wakati huyu mwizi ameswap ile namba ndipo meseji kwenye simu ya aliyeibiwa ikatokea SIMCARD REGISTRATION FAILED nahuyu mwizi akafanikiwa kuwa mmliliki wa namba hiyo na kutoa kiasi chote cha fedha zilizokuwa kwenye akaunti yake hiyo, na vodacom wamemwambia hawana msaada zaidi wa kumsaidia ila aende polisi, alivyoenda polisi akaambiwa atoe fedha tshs 40000 ili waweze kumsaidia.

*Hivi haya makampuni ya simu hayawezi kuweka utaratibu mzuri wa kuswap line za simu badala ya ule wa kutaja namba tano unazopiga sana???????

*Wananchi wengi hawajui au hawaelewi jinsi ya kotoa fedha kwenye akaunti ya mpesa hivyo wanawapa wakala simu zao na kuwatajia namba za siri ili waweze kutoa fedha na huo ndo mwanya wa tamaa na wizi kwani akiona salio kubwa atakuwa na tamaa na pia mara nyingine wanaokaa kwenye huduma za mpesa ni deiwaka tu mara nyingi watoa fedha hawasaini kwenye ledger kama inayotakiwa. Hapa wizi utaendelea sana Kuweni makini.

Soma huu ujumbe na mweleze mwenzio ili achukue tahadhari.
Mkuu nimecheka sana hasa pale jamaa yako alipotoa namba ya siri hadharani. Hivi namba ya siri maana yake si ni SIRI sasa kilanga cha kwenda kuitamka hadharani cha nini? Atakuwa wa Mwandiga kuelekea manyovu huyu!

Lakini kitu kingine ambacho ni tatizo ni kuhusu kuswap number: Yaani jamaa alienda tu na ku swap na kuwa proud owner wa namba ya mshikaji? Hakuuliwa kutoa kitambulisho chochote? Hapa kuna shida inabidi Vodacom wamtrace mfanyakazi wao aliyeruhusu hiyo swap na atoe uthibitisho wa kitambulisho alichotumia kufanyia swap, kama hana ama anacho ambacho si cha mwenye simu basi awe naye ni mwizi tu. Mimi nilikuwa nadhani kwa kusajili namba basi ukora wa namna hiyo ulikuwa umeisha kumbe bado upo!
 
Back
Top Bottom