Jihadharini na mbinu hii - ni hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jihadharini na mbinu hii - ni hatari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Mar 31, 2011.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  wAPENDWA, TAFADHALI SOMENI HII
  ( Nimetumiwa tu na sihusiki kwa kuona au kisikia mimi mwenyewe hivyo msiniulize ilikuwaje maana sina majibu.Nimeona ni vizuri kushirikishana:
  Wizi wa kupulizia dawa za kulevya kwenye vipeperushi jijini Dar es Salaam

  Kufuatia ugumu wa maisha, kuna wizi umeingia Dar es salaam na inawezekana ukasambaa hata kwenye miji mingine mikubwa. Wizi huo uko hivi

  1. Unaweza kupewa kipeperushi ambacho kimepuliziwa dawa na baada ya kupokea aliyekupatia ambaye anajifanya anauza bidhaa anazozitangaza kwenye kipeperushi hicho anakufwatilia kwa nyuma na gari nyingine na kukupora kila kitu baada ya wewe kupoteza fahamu.

  AU

  2. Ukiwa unaendesha gari vijana wanakufuata na kukushitua kuwa gari inawaka moto then utafungua dirisha kutaka kuona na pengine kusimama. Watakwambia hakuna kitu vijana wanakudanganya hao. Ndani ya muda huo mfupi kwa namna ya ajabu ukifungua tu dirisha wanakupulizia madawa yenye Ladha na harufu kama pipi tamuu na kukufuatilia kwa matumaini kwamba utapoteza fahamu na wao kukunyang’anya mali zako including kupora vitu kwenye gari.

  HIVYO KUWENI MAKINI UNAPOENDESHA GARI USIFUNGUE VIOO WALA KUPOKEA KIPEPERUSHI AU KUNUNUA NUNUA HOVYO CHOCHOTE KWENYE HIZO FOLENI ZA DAR. PIA WANAFANYA HUO UCHAKACHUZI WA FAHAMU HASA MAENEO YA PETROL STATION NA MAENEO YA MAEGESHO YA MAGARI KAMA MLIMANI CITY.


  TRUE STORY:
  Kuna jamaa yangu kama wiki mbili zilizopita, alikuwa anatoka kupata moja mbili kutoka baa moja inayojulikana kama BREAKPOINT kati muda wa saa moja hivi jioni, akaja kijana mmoja alionekana anashida sana ya kutaka kusaidiwa nauli, rafiki yangu akawa msamaria mwema akachomoa noti ya 1,000 na kumpatia kijana, rafiki yangu alipokosea ni kumuuliza kijana kwani unaelekea mitaa ya wapi? Kijana akasema anaelekea kimara, jamaa akasema basi twende nitakuacha manzese maana mimi naelekea Sinza. My friend says the guy dressed very smart and he was looking as a graduate who for that day alikwama kweli nauli, and you can’t even think if he is a criminal.

  They started the journey from Posta via Jangwani, alipofika Jangwani anasema aliaanza kujisikia kizunguzungu na kichefuchefu na kulikuwa na foleni kali sana . Akaamua alipofika Magomeni achepuke kushoto ili apate pumzi kidogo nje, then he did not remember what went on until he found himself at muhimbili akiwa hajitambui na wala hajui gari yake ipo wapi (he was driving a Mark X), na yeye mwenyewe akiwa bado na mawenge.

  Jamani zikumbukeni namba za wenzi wenu kichwani, usiku huo mnamo saa saba za usiku alipopata fahamu vizuri alikumbuka namba ya mke wake, akampigia na akaja hapo hospitali. Gari yake iliyokuwa na vitu vyake kama Laptop, bank cards, simu, etc havijaonekana mpaka tunavyoongea leo.

  Madaktari wanasema, alivuta sumu, sasa swali ni je kwa nini yule kijana hakudhurika na sumu hiyo kwa kuwa walikuwa naye mpaka Magomeni alipoanza kujisikia vibaya? Au ni wimbi la vijana ambao wanakuwa wanakufuatilia na mmoja wao anajitoa muhanga wa kuvuta sumu hiyo na wengine wanakuwa wanakufuatilia kwa nyuma, na wakishakukamata wanakutupa na kumuokoa mwenzao, which I think it is possible.

  WATCH OUT!!!
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Shukrani kwa taarifa WOS....:disapointed:
   
 3. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Kaka thanks kwa hii taarifa! Real imetokea sehemu nyingi!
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Asante maana unatusaidie na wengine kujilinda na huo tapeli.
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  ubarikiwe sana kwa taarifa hii
   
 6. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mungu ndiye kimbilio kila wakati. Kwa nguvu/akili zetu hatuwezi kuyakwepa haya.
   
 7. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii imekuja wakati muafaka nikifika tu hakuna kufungua vioo asante sana dear
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Asante sna hali inatisha siku hizi duh
   
 9. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Dunia inakwenda wapi hii? Anyway tutapambana nao.
  Hv ule uzushi wa yale majini walemavu pale salender bridge nao uliishia wapi?
   
 10. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hizi zipo nyingi. Ni sisi wenyewe tuwe makini. Nyingine unaweza kukutana na mtu akataka kukusalimia,lakini anakuwa na kasi ya ajabu ya kutaka akupe mkono. Tahadhali! Mkono huo huwa unakuwa na madawa ya kulevya! Mkishaachana yeye na wenzake huwa nyuma yako wanakufatilia. Si mwendo utasikia kizunguzungu na kupoteza fahamu. Wao wakikukuta watakudaka harakaharaka na watawaambia wapita njia wanao doubt kwamba ww ni ndugu yao wanakupeleka hospital. Watakusafisha kwa raha zao kila kitu!. Nyingine inaitwa doloree na inapatikana sehemu za vinywaji. Ukiacha tu glass yako ya kinywaji mezani bila mtu wako unaemjua kukuangalizia inawekwa madawa na ukirudi na kuendelea kuitumia,utakuja kuamshwa wakati wanafunga bar/restaurant au kesho yake ukiwa hauna hata kitu,hata kama ulikuwa unakunywa soda tu. Nyingine kwa mnaopenda kukiuka misingi ya ndoa zenu kwa kuchukua vyangudoa na kwenda guest. Ishue huwa inapakwa kwenye chuchu za matiti mwanzoni kabisa akikuambia anaenda kuoga watchout!. Ukijifanya unajua mapenzi sana kwa kunyonya sehemu hizo tu,utakuja kuamshwa kesho yake mchana ukiwa haujitambui. Tuwe waangalifu!
   
 11. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ubarikiwe.. Ahsante kwa angalizo
   
 12. l

  lumimwandelile Senior Member

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  haya wenye masikio sikieni. hawa ombaomba tuwaogope sasa
   
Loading...