Jihadhari, utakufa mapema bure kwa sababu ya uchungu ulio nao!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,128
Reaction score
8,058
Watu wengi wamejaa uchungu kwa sababu ya mambo yanayotokea huku na kule duniani. Kuna mtu ana uchungu kwa sababu ya madeni, kukosa kazi, biashara kufilisika au maisha kuwa magumu. Mwingine ana uchungu kwa sababu ya kuachwa na mke/mume, au kusalitiwa, kukataliwa au kufiwa na mtu anayempenda. Wengine wana uchungu kwa sababu ya migogoro ya kifamilia, kijamii na kiuchumi. Na wengine wamejaa uchungu kwa sababu wanahisi wanaonewa. Wenye uchungu kwa sababu wanaishi katika nchi zenye vita na majanga ya asili hao nao ni wengi.

Mwingine ana uchungu kwa sababu amesikia eti Netanyahu ataiangamiza Iran au Iran imezipiga kambi za wanajeshi wa Marekani. Na usishangae nikikuambia kuna mtu ana uchungu kwa sababu ameambiwa asikae 'siti' ya mbele kwenye sherehe! Na humu JF kuna wengine wana 'mapovu ya uchungu' kwa sababu wamewekwa kwenye "ignore list" au fulani ame-comment "nonsense" kwenye uzi wake!

Ukibeba uchungu moyoni siku nzima, unajiumiza wewe mwenyewe. Uchungu, hasira na msongo wa mawazo vinaweza kuufanya mwili wako ubaki katika hali ya "stress" na kukuongezea mapigo ya moyo na shinikizo la damu, au kuvuruga usingizi wako na kuathiri afya yako kwa ujumla. Kwa hiyo, usiruhusu mambo ambayo huwezi kuyabadilisha yaanze 'kukuua' kidogo kidogo, ndani kwa ndani, hadi upoteze maisha yako kabla ya wakati.

Mtume Paulo alituasa akisema: "...jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka" (Waefeso 4:26).
Vile vile, Yesu Kristo kabla hajapaa mbinguni alituambia wazi kwamba ulimwenguni tunayo dhiki; lakini tujipe moyo...(Yohana 16:33).

Kwahiyo, usikubali uchungu utawale maisha yako. Usilale ukiwa umebeba uchungu, hasira na chuki. Usiuache moyo wako ujae mawazo ya kulipiza kisasi.

Badala yake sote tunapaswa kufurahi katika Bwana siku zote kama tulivyoagizwa katika Wafilipi 4:4. Tunapaswa kufurahi kwa sababu siku inakuja upesi ambapo Mungu atafuta kabisa machozi katika macho yetu, atakapofanya mbingu mpya na nchi mpya. Mambo yanayotuletea uchungu, huzuni, maumivu na machozi, hayatakuwepo tena (Ufunuo 21:4).

Dalili zinaonesha wazi tuko ukingoni. Karibu sana Yesu atakuja kutuchukua na kutupeleka mbinguni kwenye raha ya milele. Hivyo huu ni muda mwafaka wa kutubu na kuomba Mungu atusamehe makosa yetu na sisi pia tuwasamehe waliotukosea (Mt 6:12). Ni muda mzuri wa kukiri kuwa Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili yetu. Ni muda sahihi wa kukubali Yesu atuokoe na kutawala maisha yetu, kabla neema haijafungwa.

Kinyume na hapo, ukiendelea kujaa hasira, uchungu, ghadhabu na mawazo yasiyompendeza Mungu, unaweza kujisababishia kifo cha mapema. Na ukifa katika hali hiyo ya dhambi, utaendelea kuteseka kwa uchungu katika moto wa milele.

Mungu akusaidie kuwa msomaji na mtendaji wa hayo niliyokushauri leo. Blessings to you!
 
Watu wengi wamejaa uchungu kwa sababu ya mambo yanayotokea huku na kule duniani. Kuna mtu ana uchungu kwa sababu ya madeni, kukosa kazi, biashara kufilisika au maisha kuwa magumu. Mwingine ana uchungu kwa sababu ya kuachwa na mke/mume, au kusalitiwa, kukataliwa au kufiwa na mtu anayempenda. Wengine wana uchungu kwa sababu ya migogoro ya kifamilia, kijamii na kiuchumi. Na wengine wamejaa uchungu kwa sababu wanahisi wanaonewa. Wenye uchungu kwa sababu wanaishi katika nchi zenye vita na majanga ya asili hao nao ni wengi. Mwingine ana uchungu kwa sababu amesikia eti Netanyahu ataiangamiza Iran au Iran imezipiga kambi za wanajeshi wa Marekani. Na usishangae nikikuambia kuna mtu ana uchungu kwa sababu ameambiwa asikae 'siti' ya mbele kwenye sherehe! Na humu JF kuna wengine wana 'mapovu ya uchungu' kwa sababu wamewekwa kwenye "ignore list" au fulani ame-comment "nonsense" kwenye uzi wake!

Ukibeba uchungu moyoni siku nzima, unajiumiza wewe mwenyewe. Uchungu, hasira na msongo wa mawazo vinaweza kuufanya mwili wako ubaki katika hali ya "stress" na kukuongezea mapigo ya moyo na shinikizo la damu, au kuvuruga usingizi wako na kuathiri afya yako kwa ujumla. Kwa hiyo, usiruhusu mambo ambayo huwezi kuyabadilisha yaanze 'kukuua' kidogo kidogo, ndani kwa ndani, hadi upoteze maisha yako kabla ya wakati.

Mtume Paulo alituasa akisema: "...jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka" (Waefeso 4:26).
Vile vile, Yesu Kristo kabla hajapaa mbinguni alituambia wazi kwamba ulimwenguni tunayo dhiki; lakini tujipe moyo...(Yohana 16:33).

Kwahiyo, usikubali uchungu utawale maisha yako. Usilale ukiwa umebeba uchungu, hasira na chuki. Usiuache moyo wako ujae mawazo ya kulipiza kisasi.

Badala yake sote tunapaswa kufurahi katika Bwana sikuzote kama tulivyoagizwa katika Wafilipi 4:4. Tunapaswa kufurahi kwa sababu siku inakuja upesi ambapo Mungu atafuta kabisa machozi katika macho yetu, atakapofanya mbingu mpya na nchi mpya. Mambo yanayotuletea uchungu, huzuni, maumivu na machozi, hayatakuwepo tena (Ufunuo 21:4).

Dalili zinaonesha wazi tuko ukingoni. Karibu sana Yesu atakuja kutuchukua na kutupeleka mbinguni katika raha ya milele. Hivyo huu ni muda mwafaka wa kutubu na kuomba Mungu atusamehe makosa yetu na sisi pia tuwasamehe waliotukosea (Mt 6:12). Ni muda mzuri wa kukiri kuwa Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili yetu. Ni muda sahihi wa kukubali Yesu atuokoe na kutawala maisha yetu, kabla neema haijafungwa.

Kinyume na hapo, ukiendelea kujaa hasira, uchungu, ghadhabu na mawazo yasiyompendeza Mungu, unaweza kujisababishia kifo cha mapema. Na ukifa katika hali hiyo ya dhambi, utaendelea kuteseka kwa uchungu katika moto wa milele.

Mungu akusaidie kuwa msomaji na mtendaji wa hayo niliyokushauri leo. Blessings to you!
Amen...
 
Watu wengi wamejaa uchungu kwa sababu ya mambo yanayotokea huku na kule duniani. Kuna mtu ana uchungu kwa sababu ya madeni, kukosa kazi, biashara kufilisika au maisha kuwa magumu. Mwingine ana uchungu kwa sababu ya kuachwa na mke/mume, au kusalitiwa, kukataliwa au kufiwa na mtu anayempenda. Wengine wana uchungu kwa sababu ya migogoro ya kifamilia, kijamii na kiuchumi. Na wengine wamejaa uchungu kwa sababu wanahisi wanaonewa. Wenye uchungu kwa sababu wanaishi katika nchi zenye vita na majanga ya asili hao nao ni wengi.

Mwingine ana uchungu kwa sababu amesikia eti Netanyahu ataiangamiza Iran au Iran imezipiga kambi za wanajeshi wa Marekani. Na usishangae nikikuambia kuna mtu ana uchungu kwa sababu ameambiwa asikae 'siti' ya mbele kwenye sherehe! Na humu JF kuna wengine wana 'mapovu ya uchungu' kwa sababu wamewekwa kwenye "ignore list" au fulani ame-comment "nonsense" kwenye uzi wake!

Ukibeba uchungu moyoni siku nzima, unajiumiza wewe mwenyewe. Uchungu, hasira na msongo wa mawazo vinaweza kuufanya mwili wako ubaki katika hali ya "stress" na kukuongezea mapigo ya moyo na shinikizo la damu, au kuvuruga usingizi wako na kuathiri afya yako kwa ujumla. Kwa hiyo, usiruhusu mambo ambayo huwezi kuyabadilisha yaanze 'kukuua' kidogo kidogo, ndani kwa ndani, hadi upoteze maisha yako kabla ya wakati.

Mtume Paulo alituasa akisema: "...jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka" (Waefeso 4:26).
Vile vile, Yesu Kristo kabla hajapaa mbinguni alituambia wazi kwamba ulimwenguni tunayo dhiki; lakini tujipe moyo...(Yohana 16:33).

Kwahiyo, usikubali uchungu utawale maisha yako. Usilale ukiwa umebeba uchungu, hasira na chuki. Usiuache moyo wako ujae mawazo ya kulipiza kisasi.

Badala yake sote tunapaswa kufurahi katika Bwana sikuzote kama tulivyoagizwa katika Wafilipi 4:4. Tunapaswa kufurahi kwa sababu siku inakuja upesi ambapo Mungu atafuta kabisa machozi katika macho yetu, atakapofanya mbingu mpya na nchi mpya. Mambo yanayotuletea uchungu, huzuni, maumivu na machozi, hayatakuwepo tena (Ufunuo 21:4).

Dalili zinaonesha wazi tuko ukingoni. Karibu sana Yesu atakuja kutuchukua na kutupeleka mbinguni katika raha ya milele. Hivyo huu ni muda mwafaka wa kutubu na kuomba Mungu atusamehe makosa yetu na sisi pia tuwasamehe waliotukosea (Mt 6:12). Ni muda mzuri wa kukiri kuwa Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili yetu. Ni muda sahihi wa kukubali Yesu atuokoe na kutawala maisha yetu, kabla neema haijafungwa.

Kinyume na hapo, ukiendelea kujaa hasira, uchungu, ghadhabu na mawazo yasiyompendeza Mungu, unaweza kujisababishia kifo cha mapema. Na ukifa katika hali hiyo ya dhambi, utaendelea kuteseka kwa uchungu katika moto wa milele.

Mungu akusaidie kuwa msomaji na mtendaji wa hayo niliyokushauri leo. Blessings to you!
Mama mchungaji habari.

Mimi nina uchungu moyoni mwangu.
Nina mpenzi wangu ambaye nampenda sana, ila tatizo lake amekuwa mtu wa kurudia makosa yale kila mara.

Natumia nguvu kubwa kumuelekeza ila ni mtu wa dharau, mfano kwa sasa yuko mbali na mimi naweza kupiga simu mara kumi asipokee na muda akinitafuta anatuma message tano kwa wakati mmoja yani dakika moja kuonyesha kwamba amekutafuta kitu ambacho ni unafki.

Tukigombana anakimbilia kuwatafuta x wake ambao wameachana miaka 3 iliyopita.

Hajui kupika vizuri nilimwambia tafuta mgahawa ujifunze kupika ila alienda mara moja tu

Hana uwezo mkubwa wa kushauri au kutoa mawazo yoyote nikamnunulia kitabu kimoja cha nguvu ya Mwanamke ila hajakimaliza wala hajawahi kuomba kitabu kingine asome

Makosa mengi huwa yanatokea tukiwa mbalimbali hasa kwenye mawasiliano anadai kwao majukumu ni mengi.

Mfano jana nimempigia simu zaidi ya mara 15 akajibu anaumwa nikamwambia siku nzima ulikuwa unafanya nini akasema alikuwa amelala

Nikamuuliza kama ulikuwa umelala unashindwa kupokea wala kutuma message??

Mama mtumishi em naomba ushauri mana mpaka namba yake nimeikalili
Nina miaka 26

Naomba nishauri kama mtoto wako na haya utakayonishauri nitafanyia kazi

Ahsante
 
Daah pole sana umekuwa dhaifu kwake ndo maana anakufanyia hivyo pha jua kuwa ameshapata mwingine upendo kwako umekufa acha kupiga simu nyingi hivyo wekeza kujijenga mwenyewe
.

Mimi nina uchungu moyoni mwangu.
Nina mpenzi wangu ambaye nampenda sana, ila tatizo lake amekuwa mtu wa kurudia makosa yale kila mara.

Natumia nguvu kubwa kumuelekeza ila ni mtu wa dharau, mfano kwa sasa yuko mbali na mimi naweza kupiga simu mara kumi asipokee na muda akinitafuta anatuma message tano kwa wakati mmoja yani dakika moja kuonyesha kwamba amekutafuta kitu ambacho ni unafki.

Tukigombana anakimbilia kuwatafuta x wake ambao wameachana miaka 3 iliyopita.

Hajui kupika vizuri nilimwambia tafuta mgahawa ujifunze kupika ila alienda mara moja tu

Hana uwezo mkubwa wa kushauri au kutoa mawazo yoyote .

Mfano jana nimempigia simu zaidi ya mara 15
 
Back
Top Bottom